Ndiyo,mwanzoni ukitengeneza hizo sakitii inakuwa rahisi kubadili maamuzi, mfano ukijifunza leo umalaya, ni rahisi kuacha ila kwa mtu ambaye tokea azaliwe anakulia kwenye umalaya ni ngumu kuacha...ndomaana kuna msemo 'you cant turn a ho into a housewife' 'you cant teach an old dog new tricks'..Kuna stage zile circuit zinakuwa zimekomaa kiasi kwamba kuzibadili ni near impossible (kama extrovert kuwa introvert au vice versa)
Ni ngumu ila haina maana haiwezekani, mkuu malaya anaweza kuwa mke mzuri tu nazungumza hii nikimaanisha. Leo mtu kuwa A haina maana hawezi kuwa B.
‘Introvert’ kuwa ‘Extrovert’ inawezekana kabisa japo ni ngumu ila haimaniishi haiwezekani, mkuu usitafsiri ugumu wa kufanya jambo kuwa ni kukosa uhuru wa kulifanya, la.
Mtu yeyote akifanya jitihada sahihi anaweza kuwa yoyote.
Wewe kujihisi uko huru haimaanishi uko huru, huko kujihisi huru kunaweza kuwa ni illusion ubongo wako unakutengenezea.
Ni kweli.
Unaweza kuamua kuwa daktari halafu ile umemaliza kusoma diploma ya CO unataka kuapply degree, serikali ikasema udaktari lazima upite form 6, na kufaulu bado ni ishu ya bahati maana unaweza kusoma Organic chemistry mtihani ukatoka inorganic.
Ikiwa kweli unataka kuwa daktari basi unaweza kwenda nchi nyingine kukamilisha ndoto zako.
Kuwepo kwa ugumu haina maana mtu kakosa uhuru.
Na mwingine anaweza asipende kuwa mwalimu ila akashangaa mambo yalivyoenda mpaka akawa mwalimu (walimu wengi hawakupanga kuwa walimu)
Sasa huyu mtu ni kwamba KAAMUA KWA MOYO WAKE kuwa mwalimu lakini sababu ndiyo hutofautiana, ila ANGEAMUA KWA MOYO wake kuwa anachotaka nina hakika asingekuwa mwalimu.
Tusitumie mazingira kama ‘excuse’ ya kutofanya jambo fulani kiasi tukasema hatuna ‘free will’
Leo tungesingizia mazingira kuwa sisi hatuwezi kupaa sidhani kama kuna mtu angegundua ndege, MAZINGIRA NI YETU KUYAKABILI ILI TUWE TUNACHOTAKA.
Nioneshe harakati moja ambayo ilikuwa ni rahisi kupata matokea, tazama Uhuru wa kitaifa, Fikra za kikomunisti na Kiliberali, Ufeministi, Udini n.k hawa wote wangesingizia mazingira kamwe tusingekuwa na hivyo vitu.
Yesu (AS) angesingizia ufinyu wa fursa kwenye utawala wa Roma kamwe asingeweza hubiri amani ungesema “mtu akihubiri anatundikwa msalabani” ile ni ‘consequences’ ambayo yesu (as) alichagua maana angeweza kukaa kimya ila akaona hapana, ana wajibu wa kusema ukweli na matokeo yake dunia karibia yote inafuata mafundisho yake.
Vile vile kwa Muhammad (pbuh) mazingira hayakuruhusu ahubiri uislam lakini tazama alivyoyakabili, Vile vile kwa Mussa (as), Remus na kaka yake wasingeyakabili mazingira Himaya ya Roma ingetoka wapi, Osman na Orhan nao wangesingizia mazingira Ottoman ingetoka wapi?, Xenophon angesingizia mazingira wangerudi hai? Wagiriki wangesingizia mazingira wangewezaje kulikabili jeshi lenye nguvu la Uajemi?
Wewe unajuaje kama haupo kwenye algorithm??
Kwa sababu mimi ni mwanaadamu, mimi ndiye ninaetengeneza hiyo algorithm.
Roboti anajijuaje kuwa anafata algorithm??
Sijui mkuu, Hili swali tuyaulize maroboti, tena tupate bahati kuyauliza yenye akili za kutosha kulijua hilo.
Kuna experiment unaweza kuifanya kuprove kuwa huu ulimwengu sio simulation au sio scripted?
Vizuri sana, kuna ‘experiment’ unaweza fanya kuthibitisha kuwa hii dunia ni ‘scripted’ au ‘simulation’?
Nina uhakika huwezi na mimi siwezi, hayo maswali yanalenga kuvuruga mada kwa kupandikiza mashaka na hofu kwa kila kitu hapa duniani.
Nadhani vitu kama coincidence,karma,deja vu,destiny,prophesies nk. vinaprove huu ulimwengu ni scripted
Unadhani, unaweza thibitisha kwa ushahidi jadidi mkuu?
Maana hata mimi naeza kudhani chochote kile. Mf. Naweza kudhani wewe ni muongo.
Haya 'maadili' yanategemea vingi ikiwemo emotions (sio logic tu)nukiona mtoto wa primary kuna emotion unapata na ukiona bibi kizee kuna emotion unapata..maamuzi meng hufanywa kwa kufuata emotions kali zimeegemea upande upi.
Hapana, Maadili hayahusiani na hisia binafsi.
Jambo haliwi sahihi kimaadili kwa sababu kuna mtu ana’feel’ kitu fulani, japo ni lazima nikubali kuwa hakuna ‘consensus’ kwenye hili ila ni mada pana ambayo haina mwisho.
Ukisema hisia kila mtu ana namna anavyohisi kuhusu jambo fulani, Hitler alihisi wayahudi hawafai kuishi, je alikuwa sahihi?
Ndiyo, alikuwa sahihi kwa upande wake lakini vipi kuhusu wayahudi wenyewe?
Wapo wazungu walihisi watu weusi si wanaadamu bali ni wanyama, je walikuwa sahihi?
Maadaili kamwe huwezi yanasibisha na hisia.
Hizi emotions zinatengenezwa na kuwa controlled na sehemu ya ubongo inaitwa amygdala..Kwahyo Amygdala ndio inayokucontrol wewe na maadili yako...sio wewe
Mkuu unajua kuwa hii njia uliyoichagua inakwenda shimoni?
Haya ukisema “wewe” unamaanisha MIMI, nakuuliza MIMI ni nani? (Usinitajie jina, nataka nione ni kwa namna gani unaweza nitenganisha mimi na ubongo wangu)
By the way mkuu...je, kuna experiment au kuna proof yoyote inayoweza kuelezea how hizi brains zetu zilizotengenezwa kwa neurones ambazo zimetengenezwa kwa atoms ambazo ni electrons,nucleons na protons tu...zimewezaje kuwa na free will??
Mpaka sasa sijakutana na ripoti kuhusu jaribio lolote ulilotaja, ila naweza kukwambia kwa uhakika ktk kila jambo unalotaka kufanya ni lazima akili yako ikupe ‘options’, na wewe aidha kwa kujua au kutojua (na kutojua mara nyingi ni kutotaka kufikiri) utachagua mojawapo ya ‘option’ iwe utatumia hisia kuchagua ama ‘reasoning’ hiyo ni juu yako lakini kila kitu kinakupa nafasi ya kuchagua.
Hata ukisoma maneno haya una nafasi ya kuchagua aidha kubonyeza ‘Like’ ama kuacha au kujibu ama kupuuza.
UKO HURU MKUU CHAGUA CHOCHOTE UTAKACHO ILA JUA KINA ‘consequences’ hili USISAHAU.