Forgotten
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,518
- 10,839
Leo nimekaa nikawaza kama Dinosaurs waliweza kupotea kabisa kwenye uso wa Dunia ikikaridiwa namba yao ilikuwa 2.5 billion, miaka milioni 65 iliyopita basi kuna uwezekano mkubwa wa binadamu nao kutoweka kabla Yesu hajarudi.
Dunia inakadiriwa kuwa na umri wa miaka bilioni 4.5 na katika miaka yote hiyo kumetokea mabadiliko makubwa katika viumbe hai waliokanyaga uso wa Dunia, wengi wakiwa wametoweka kabisa.
Mamalia wa kwanza inakadiriwa alionekana kwenye uso wa Dunia miaka 200 iliyopita na walikuwa siyo dominant species. Paleocene Epoch ilikuwa kipindi mfumo wa ikolojia ulianza kuimarika tena baada ya Dinosaurs kutoweka kabisa baada ya mawe makubwa kutoka angani kuanguka Duniani. Dinosaurs walikuwa dominant kwa kipindi chote hicho na kutoweka kwao ndiyo kukachangia ukuaji na ustawi wa viumbe hai wengine ikiwemo binadamu ambao baada ya miaka takribani 300,000 tumeweza kufika hapa tulipo.
Sababu ninazoamini zinaweza kupelekea binadamu kutoweka kabisa katika sayari hii nzuri na ya kuvutia ni:
1. Mabadiliko ya Tabianchi: Kwasasa kuna mabadiliko makubwa katika hali ya hewa ya Dunia na ikiendelea hivi kwa muda mrefu sayari hii itakuwa siyo nyumbani kwa viumbe hai tena. Ikiwa hali ya hewa ya Dunia itakuwa ngumu kwa wanadamu kuishi, kama vile joto kali, baridi, au hali ya hewa isiyotabirika, inaweza kuhatarisha maisha yetu.
2. Magonjwa: Ikiwa ugonjwa hatari sana utaibuka na wanadamu hawataweza kuutibu au kudhibiti, inaweza kupunguza idadi ya watu au kusababisha kuangamia kwa wanadamu. Wengi tunakumbuka kilichotokea wakati wa Pandemia ya kimataifa, COVID-19.
3. Vita vya Nyuklia: Silaha za nyuklia zina nguvu na zinaweza kufanya uharibifu mkubwa. Ikiwa nchi zitashiriki katika vita vya nyuklia, matokeo yanaweza kuwa mabaya: kusababisha uharibifu wa mazingira wa kudumu, na kufanya Dunia kuwa ngumu kuishi kwa wanadamu.
4. Athari ya Asteroid: Mawe makubwa kutoka angani ambayo yanaweza kugonga uso wa Dunia. Athari kubwa inaweza kusababisha uharibifu mkubwa, moto, na mabadiliko ya tabianchi ambayo yanaweza kufanya kuwa vigumu kwa wanadamu kuishi au kutoweka kabisa kama ilivyotokea kwa Dinosaurs.
5. Akili Mnemba (AI): Akili Mnemba inahusu mashine au programu ambazo zinaweza kujifunza na kufanya maamuzi kwa kujitegemea. Ikiwa teknolojia ya AI itakua haraka na kuwa ngumu kudhibiti, inaweza kusababisha madhara kwa wanadamu: kwa makosa, ajali, au vitendo vya uharibifu. Tumeanza kuyaona madhara ya AI mwanzo kabisa na inatabiriwa itakuja kuwa tishio kwa miaka ya mbeleni.
6. Kupotea kwa utofauti wa maisha: Ikiwa spishi nyingi zitapotea (kama vile mimea, wanyama, wadudu, n.k.), inaweza kuvuruga mifumo ya ikolojia na usawa wa maumbile, na kufanya maisha kuwa magumu kwa wanadamu kuishi. Shukrani kwa wanasayansi na tafiti walizofanya kuja na wazo la Svalbard Global Seed Vault ambalo ni tumaini kwa wanadamu iwapo mimea yote itatoweka Duniani.
7. Idadi kubwa ya watu kupita kiwango: Ikiwa idadi ya watu itaendelea kuongezeka bila rasilimali au mipango bora, tunaweza kukutana na matatizo makubwa kama vile uhaba wa chakula, ukosefu wa maji safi, na hali ya maisha isiyo ya kuvumilika, ambayo mwishowe inaweza kusababisha kuanguka kwa jamii ya wanadamu.
Tumaini pekee la mwanadamu ni akili na upeo mkubwa alionao. Naweza kusema Sayansi ndiyo iliyomuwezesha binadamu kuweza ku-survive miaka yote hiyo katika sayari hii iliyojaa mabalaa, bila hivyo huenda tusingeweza kufika hata 8 billion.
Naamini Dinosaurs walitoweka kwenye uso wa Dunia kwasababu hawakuwa na akili kama aliyonayo binadamu. Tafiti zinazoendelea kufanywa na mashirika kama NASA, Space X, na watu kama Elon Musk ni ya kukumbukwa na vizazi kwasababu wakifanikiwa kupata sehemu nyingine itakayo-support maisha kwa binadamu kwenye The Milky Way Galaxy basi spishi ya binadamu inaweza kuja kuwa spishi itakayodumu kwa muda mrefu zaidi.
Thank God I'm an Atheist!