Je, binadamu wapo katika hatari ya kutoweka kwenye uso wa Dunia?

Je, binadamu wapo katika hatari ya kutoweka kwenye uso wa Dunia?

dinosaurs walikuwa na maumbile makubwa kwahiyo mahitaji yao ya kiikolojia yalikuwa makubwa pia(haswa chakula)

hivyo walipata tabu sana
Ulisema pia hizo Asteroids zilileta milipuko.

Kama Dinosaurs walishindwa kuhimili milipuko ya Asteroids, Je viumbe wengine waliwezaje kuhimili hiyo milipuko ya Asteroids?

Au hao viumbe wengine walikuwa hawashiki moto?
 
Ulisema pia hizo Asteroids zilileta milipuko.

Kama Dinosaurs walishindwa kuhimili milipuko ya Asteroids, Je viumbe wengine waliwezaje kuhimili hiyo milipuko ya Asteroids?

Au hao viumbe walikuwa hawashiki moto?
mlipuko ulikuwa karibu tu na eneo la tukio

sehemu zingine zilipata madhara tofauti
 
Hizo Asteroids zilileta milipuko.

Sasa ni viumbe gani wenye uwezo wa kuhimili milipuko?

Kama Dinosaurs walishindwa kuhimili milipuko ya hizo Asteroids, Viumbe wengine waliwezaje?

Kama viumbe wengine waliweza kuhimili milipuko ya hizo Asteroids wakaendelea kuwepo, Dinosaurs walishindwaje na wao kuhimili hiyo milipuko?
Top of the food chain = more vulnerable.

Eneo walilokuwepo Dinosaurs ndiyo kulikuwa na impact kubwa zaidi kwahiyo wengi waliangamia na wachache waliobaki wakashindwa kubadilika kuendana na mazingira ikilinganishwa na spishi ndogo na zenye ustahimilivu ambazo ziliweza kuishi na baadaye kustawi katika Dunia baada ya kutoweka kwa Dinosaurs.

Dinosaurs waliosalia eneo lao lilikuwa tayari limeathirika na kuna limited resources hivyo walihimili kwa muda mfupi na wao wakapotea kabisa.
 
Niletee kwanza orodha ya species zote zilizowahi kuwepo duniani na kipindi zilichoishi ili niweze kukuchambulia.
Mimi siwezi kukuletea hizo species zote zilizowahi kuwepo duniani. Maana ni nyingi sana na nyingine bado hata hazijfahamika kama zipo.

Hapa mada imejikita kwenye hawa dinosaurs.

Ilikuwaje wao tu watoweke kutokana na hizo athari za Asteroids?

Je viumbe wengine waliwezaje ku survive hizo athari za Asteroids?

Kama viumbe wengine waliweza ku survive athari za Asteroids, Dinosaurs walishindwaje?
 
Leo nimekaa nikawaza kama Dinosaurs waliweza kupotea kabisa kwenye uso wa Dunia ikikaridiwa namba yao ilikuwa 2.5 billion, miaka milioni 65 iliyopita basi kuna uwezekano mkubwa wa binadamu nao kutoweka kabla Yesu hajarudi.

Dunia inakadiriwa kuwa na umri wa miaka bilioni 4.5 na katika miaka yote hiyo kumetokea mabadiliko makubwa katika viumbe hai waliokanyaga uso wa Dunia, wengi wakiwa wametoweka kabisa.

Mamalia wa kwanza inakadiriwa alionekana kwenye uso wa Dunia miaka 200 iliyopita na walikuwa siyo dominant species. Paleocene Epoch ilikuwa kipindi mfumo wa ikolojia ulianza kuimarika tena baada ya Dinosaurs kutoweka kabisa baada ya mawe makubwa kutoka angani kuanguka Duniani. Dinosaurs walikuwa dominant kwa kipindi chote hicho na kutoweka kwao ndiyo kukachangia ukuaji na ustawi wa viumbe hai wengine ikiwemo binadamu ambao baada ya miaka takribani 300,000 tumeweza kufika hapa tulipo.

Sababu ninazoamini zinaweza kupelekea binadamu kutoweka kabisa katika sayari hii nzuri na ya kuvutia ni:

1. Mabadiliko ya Tabianchi: Kwasasa kuna mabadiliko makubwa katika hali ya hewa ya Dunia na ikiendelea hivi kwa muda mrefu sayari hii itakuwa siyo nyumbani kwa viumbe hai tena. Ikiwa hali ya hewa ya Dunia itakuwa ngumu kwa wanadamu kuishi, kama vile joto kali, baridi, au hali ya hewa isiyotabirika, inaweza kuhatarisha maisha yetu.

2. Magonjwa: Ikiwa ugonjwa hatari sana utaibuka na wanadamu hawataweza kuutibu au kudhibiti, inaweza kupunguza idadi ya watu au kusababisha kuangamia kwa wanadamu. Wengi tunakumbuka kilichotokea wakati wa Pandemia ya kimataifa, COVID-19.

3. Vita vya Nyuklia: Silaha za nyuklia zina nguvu na zinaweza kufanya uharibifu mkubwa. Ikiwa nchi zitashiriki katika vita vya nyuklia, matokeo yanaweza kuwa mabaya: kusababisha uharibifu wa mazingira wa kudumu, na kufanya Dunia kuwa ngumu kuishi kwa wanadamu.

4. Athari ya Asteroid: Mawe makubwa kutoka angani ambayo yanaweza kugonga uso wa Dunia. Athari kubwa inaweza kusababisha uharibifu mkubwa, moto, na mabadiliko ya tabianchi ambayo yanaweza kufanya kuwa vigumu kwa wanadamu kuishi au kutoweka kabisa kama ilivyotokea kwa Dinosaurs.

5. Akili Mnemba (AI): Akili Mnemba inahusu mashine au programu ambazo zinaweza kujifunza na kufanya maamuzi kwa kujitegemea. Ikiwa teknolojia ya AI itakua haraka na kuwa ngumu kudhibiti, inaweza kusababisha madhara kwa wanadamu: kwa makosa, ajali, au vitendo vya uharibifu. Tumeanza kuyaona madhara ya AI mwanzo kabisa na inatabiriwa itakuja kuwa tishio kwa miaka ya mbeleni.

6. Kupotea kwa utofauti wa maisha: Ikiwa spishi nyingi zitapotea (kama vile mimea, wanyama, wadudu, n.k.), inaweza kuvuruga mifumo ya ikolojia na usawa wa maumbile, na kufanya maisha kuwa magumu kwa wanadamu kuishi. Shukrani kwa wanasayansi na tafiti walizofanya kuja na wazo la Svalbard Global Seed Vault ambalo ni tumaini kwa wanadamu iwapo mimea yote itatoweka Duniani.

7. Idadi kubwa ya watu kupita kiwango: Ikiwa idadi ya watu itaendelea kuongezeka bila rasilimali au mipango bora, tunaweza kukutana na matatizo makubwa kama vile uhaba wa chakula, ukosefu wa maji safi, na hali ya maisha isiyo ya kuvumilika, ambayo mwishowe inaweza kusababisha kuanguka kwa jamii ya wanadamu.

Tumaini pekee la mwanadamu ni akili na upeo mkubwa alionao. Naweza kusema Sayansi ndiyo iliyomuwezesha binadamu kuweza ku-survive miaka yote hiyo katika sayari hii iliyojaa mabalaa, bila hivyo huenda tusingeweza kufika hata 8 billion.

Naamini Dinosaurs walitoweka kwenye uso wa Dunia kwasababu hawakuwa na akili kama aliyonayo binadamu. Tafiti zinazoendelea kufanywa na mashirika kama NASA, Space X, na watu kama Elon Musk ni ya kukumbukwa na vizazi kwasababu wakifanikiwa kupata sehemu nyingine itakayo-support maisha kwa binadamu kwenye The Milky Way Galaxy basi spishi ya binadamu inaweza kuja kuwa spishi itakayodumu kwa muda mrefu zaidi.

Thank God I'm an Atheist!
Hata Biblia imezungumzia kuhusu mwisho wa Dunia.
 
Kama viumbe wengine viliweza kuwepo duniani baada ya hayo mawe makubwa kuanguka duniani, Inakuwaje Dinosaurs wapotee tu wao wenyewe?

Je ina maana kwamba kabla ya hayo mawe makubwa kuanguka duniani, Kulikuwa hakuna viumbe wengine?

Je dinosaurs pekee ndio viumbe vilivyo toweka duniani vyenyewe tu?

Je dinosaurs pekee ndio viumbe pekee kuishi duniani kabla ya viumbe wengine wote?

Je dinosaurs ndio viumbe pekee kuishi duniani kabla ya species zote za mimea?

Kama viumbe wengine viliweza kuwepo duniani baada ya hayo mawe makubwa kuanguka duniani, Dinosaurs walishindwaje na wao kuendelea kuwepo duniani?

Iweje dinosaurs tu, wapotee halafu viumbe wengine waendelee kuwepo?

Sasa kama madhara ya hayo mawe makubwa yaliyoanguka duniani yalikuwa makubwa kiasi hiki, Viumbe wengine waliwezaje kutokea duniani?

Kama viumbe wengine waliweza kutokea duniani licha ya hayo mawe makubwa na athari zake, Dinosaurs na wao walishindwaje kuendelea kuwepo?

Mbona hizo athari za hayo mawe hazikuzuia viumbe wengine kuendelea kuwepo duniani?

Kama viumbe wengine viliweza kuwepo duniani licha ya hizo athari za mawe, Dinosaurs walishindwaje na wao kuendelea kuwepo?
ili tokea mass extinction spicies kadha wa kadha ambazo zilishindwa kuadapt mazingira mapya zilipotea akiwemo dinouser
 
Mimi siwezi kukuletea hizo species zote zilizowahi kuwepo duniani. Maana ni nyingi sana na nyingine bado hata hazijfahamika kama zipo.

Hapa mada imejikita kwenye hawa dinosaurs.

Ilikuwaje wao tu watoweke kutokana na hizo athari za Asteroids?

Je viumbe wengine waliwezaje ku survive hizo athari za Asteroids?

Kama viumbe wengine waliweza ku survive athari za Asteroids, Dinosaurs walishindwaje?
Sasa kama huwezi unatakaje mimi nikuletee orodha ya viumbe wote waliokuwepo kabla ya ajali ya kimondo na baada ya ajali!!?

Kwanza tambua kuwa walioangamia si dinosaurs tu. Viumbe wengi waliangamia. Na kilichochangia hasa kuangamia kwao ni baridi iliyofuatia baada ya mlipuko. Pengine ufanye utafiti juu ya athari za baridi inayotokea baada ya mlipuko mkubwa kama wa Volcano, Kimondo au wa nyuklia.
 
Mungu ni Mwema ,haitopotea tutaishi mpaka mwisho wa dunia...mambo ya dayanasori ni myths tu.
 
dunia nzima
Lakini kulingana na mleta mada amesema kwamba hizo Asteroids hazikuanguka eneo lote la dunia.

Kwamba zilianguka baadhi ya sehemu tu.

Sasa kama Dinosaurs walikuwepoDunia nzima. Na hizo Asteroids zilianguka baadhi ya sehemu tu, Inakuwaje sasa Dinosaurs wote duniani walipotea?

Kama Dinosaurs walikuwepo dunia nzima na hizo Asteroids zilianguka baadhi ya sehemu tu, Kwa nini Dinosaurs wa maeneo ambayo Asteroids hazikuanguka na wao walitoweka?

Kama Dinosaurs wa maeneo ambayo Asteroids hazikuanguka walitoweka, Viumbe wengine waliwezaje kuhimili athari za Asteroids wakaendelea kuwepo?
lakini wao waliathirika zaidi kwasababu ya maumbile
Lakini ulisema kwamba Asteroids zilianguka baadhi ya sehemu tu. Na dinosaurs walikuwepo dunia nzima.

Sasa ilikuwaje Dinosaurs wa maeneo mengine ya mbali na eneo la mlipuko na wao wakafa?
kuna dinosaurs walibaki ambao inasemekana waligeuka kuwa ndege wa hivi leo
Ina maana Dinosaurs walianza mabadiliko ya kuwa ndege baada ya hiyo milipuko ya Asteroids?

Au hata kabla ya hiyo milipuko walikuwa wakibadilika na kuwa ndege?
nadhani ni wale wadogo dogo, ambao ni omnivores na scavengers
 
ili tokea mass extinction spicies kadha wa kadha ambazo zilishindwa kuadapt mazingira mapya zilipotea akiwemo dinouser
Hizo species zingine ziliwezaje ku adapt mazingira?

Zili adapt mazingira kivipi maana kulikuwa na athari za Asteroids duniani na hiyo milipuko iliathiri dunia sana?
 
Sasa kama huwezi unatakaje mimi nikuletee orodha ya viumbe wote waliokuwepo kabla ya ajali ya kimondo na baada ya ajali!!?

Kwanza tambua kuwa walioangamia si dinosaurs tu. Viumbe wengi waliangamia. Na kilichochangia hasa kuangamia kwao ni baridi iliyofuatia baada ya mlipuko. Pengine ufanye utafiti juu ya athari za baridi inayotokea baada ya mlipuko mkubwa kama wa Volcano, Kimondo au wa nyuklia.
Viumbe wengi waliangamia wapi hao?

Hawa viumbe walio survive, waliwezaje ku survive?

Na hao viumbe waliotoweka, Walishindwaje ku survive?
 
Lakini kulingana na mleta mada amesema kwamba hizo Asteroids hazikuanguka eneo lote la dunia.

Kwamba zilianguka baadhi ya sehemu tu.

Sasa kama Dinosaurs walikuwepoDunia nzima. Na hizo Asteroids zilianguka baadhi ya sehemu tu, Inakuwaje sasa Dinosaurs wote duniani walipotea?

Kama Dinosaurs walikuwepo dunia nzima na hizo Asteroids zilianguka baadhi ya sehemu tu, Kwa nini Dinosaurs wa maeneo ambayo Asteroids hazikuanguka na wao walitoweka?

Kama Dinosaurs wa maeneo ambayo Asteroids hazikuanguka walitoweka, Viumbe wengine waliwezaje kuhimili athari za Asteroids wakaendelea kuwepo?

Lakini ulisema kwamba Asteroids zilianguka baadhi ya sehemu tu. Na dinosaurs walikuwepo dunia nzima.

Sasa ilikuwaje Dinosaurs wa maeneo mengine ya mbali na eneo la mlipuko na wao wakafa?

Ina maana Dinosaurs walianza mabadiliko ya kuwa ndege baada ya hiyo milipuko ya Asteroids?

Au hata kabla ya hiyo milipuko walikuwa wakibadilika na kuwa ndege?
Mkuu unavyo wabana kila pembe utadha hao dinozo walikuwa wa kwako.
 
asteroid ni moja tu. ila ilileta maafa makubwa dunia nzima kama matetemeko ya ardhi na milipuko ya volcano

mageuzi ni mchakato endelevu, hata sasa tunapitia mageuzi. dinosaurs walifanana sana na ndege, walikuwa endothermic, walikuwa na manyoya, walitaga nk
 
Hizo species zingine ziliwezaje ku adapt mazingira?

Zili adapt mazingira kivipi maana kulikuwa na athari za Asteroids duniani na hiyo milipuko iliathiri dunia sana?
yaani ukiambiwa mass extinction elewa, maana yake zidi asilimia 75 ya spicies zote zilizokwepo miaka hiyo zilitoweka na saivi hazipo,

hizo 25 zilizobaki ni kwasababu maalum zilizo wa favour mfano spicies zenye viumbe wadogo ndege nk, spicies ambazo zinaweza kula vyakula vya aina tofauti tofauti, spicie zilizokua zinakaa ndani ya maji, na zingine zilibahatika kutokana na ukanda zinapopatikana ambapo hapakua na madhara makubwa sana

spicie zingine zilizopo sasa ni kutokana na evolution ya hizo zilizokwepo

huyo dinosaur ni mojawapo tu ya wahanga ambae yeye ni famous ila spicie zilitoweka karibu zote
 
Back
Top Bottom