Mimi nauliza kuna Mzee mmoja aliwahi kuwa bodyguard wa Kabila, siku hizi namuona kwenye detail ya mkulu je amerudi uwanjani maana alikuwa mezani. Je inahusiana na kuongezeka kwa ulinzi wa Mkulu? maana kipindi cha JK alikuwa mezani
Huyo jamaa niliwahi kusimuliwa jinsi alivyomuokoa Kabila na assasination attempt. Walikuwa kwenye mkutano, ghafla kuna jamaa kutoka nje akafungua mlango wa kuingia ndani kisha akaufunga haraka bila kuingia. Huyo Mzee ndani ya sekunde akaamuru wamtoe Kabila eneo hilo, mda haukupita mrefu watu walikuja wakavamia na mitutu na kuuwa wote waliomo mule ndani. Wanaojua hiki kisa wataeleza zaidi.