Je, 'Boko' hili la 'Kujiaibisha' Mchengerwa alilitoa kama Mkwe au Waziri au Mkwe Waziri?

Je, 'Boko' hili la 'Kujiaibisha' Mchengerwa alilitoa kama Mkwe au Waziri au Mkwe Waziri?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Waziri wa TAMISEMI, Mohammed Mchengerwa amesema hajashangaa kuona Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kati Singida Dkt. Cyprian Hilinti kumuomba Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan aridhie kuwa Mama wa Taifa la Tanzania ambapo Mchengerwa amesema Rais Samia ameingia kwenye fikra na maono ya Baba wa Taifa, Mwl. Julius Nyerere.

Chanzo: millardayo

Yaani Deiwaka katika Uongozi ( akiichukua nchi Kikatiba tu na siyo kwa Kupigiwa Kura na Wananchi ) ndiyo awe Mama wa Taifa? Badilisheni upesi aina ya Bange / Bangi mnazovuta kwa sasa sawa?

GENTAMYCINE "Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer" sikufundishwa na Chuo Kikuu changu Pendwa na Tukuka cha SAUT Mwanza 2006 - 2009 ( chini ya aliyekuwa Vice Chancellor wangu Genius Fr. Dk. Charles Kitima sasa Katibu Mkuu wa TEC ) kuja kuwa Mpumbavu Niliyetukuka na Mnafiki Niliyeshindikana katika Jamii ya Watanzania, Waafrika na ile inayonizunguka.
 
Ungejibu moja kwa moja kwa hilinti aliyetoa pendekezo hilo bila upembuzi yakinifu. Ni mapema mno kutoa hadhi hiyo, hata nyerere hakuitwa baba wa taifa wakati akiwa rais, aliitwa hivyo baadae sana baada ya kustaafu. Matokeo ya kazi zake zilizotukuka ndizo zilizomfanya aitwe baba wa taifa. Huyu kuitwa mama wa taifa bado sana, asubiri kwanza astaafu halafu kazi zake zipimwe na kuona kama anastahili kuitwa mama wa taifa. Vinginevyo askofu huyo wa kkkt anajipendekeza tu na kkkt yao.
 
Nikisikia tu KKKT najua hakuja Jipya.
 
Kizazi cha kusifu na kuabudu kilizaliwa rasmi mwaka 2015 hadi sasa watu wanapimwa utendaji wa kazi zao kwa kusifu na kuabudu limekuwa taifa la hovyo sana juhudi yako ya kusifu ndio inakupa uongozi sio uwezo
 
Back
Top Bottom