Tanzania Nchi Yetu Sote
JF-Expert Member
- Mar 12, 2017
- 505
- 872
Baada ya kusoma kwangu somo la historia ninashawishika kuamini kuwa bustani ya Eden ipo mkoani Arusha eneo la Olduvai gorge ambapo paligunduliwa fuvu la mtu wa kale duniani.
Sote tutakumbuka juu ya uvumbuzi uliofanywa na Dkt. Leakey na mkewe Mary Leakey wote hawa ni wazungu na uvumbuzi wao haujawahi kupingwa popote mpaka sasa. Kwa wao (wazungu) kuvumbua fuvu la mtu wa kale duniani kwangu mimi naona hilo ni fuvu la Adam kwani siamini kama kuna mtu wa kale zaidi ya Adam. Kutokana na kutopingwa kwa uvumbuzi wao na ukimya wa wazungu juu ya suala hilo ni dhahiri kuwa:
1. Ni kweli lile ni fuvu la mtu wa kale duniani.
2. Ni kweli lile ni fuvu la Adam.
3. Ni kweli kuwa bustani ya Eden ipo nchini Tanzania eneo.
lilipovumbuliwa fuvu la Adam.
Pamoja na maelezo katika kitabu cha Biblia juu ya Adam kufukuzwa bustanini baada ya kuasi lakini ni wazi kuwa kama bustanini ndipo Adam alipokuwa akijipatia riziki yake basi hawezi kuwa alikwenda kuishi mbali na bustani hata baada ya kufukuzwa.
Naomba tujadili ili tuupate ukweli na kuisimamisha historia ya kweli juu ya fuvu lililovumbuliwa Olduvai Gorge.