Je CCM imesheheni uzalendo?

Je CCM imesheheni uzalendo?

Pac the Don

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2021
Posts
6,170
Reaction score
7,710
Kuna mikataba mingi tang zaman imekua na makandokando mengi na ufisadi wa kutisha!! Swali langu ni... Kwann wahusika wanaingia mikataba isiyo na maslahi kwa Taifa na waisainisha? Mpaka bungeni inapitishwa kwa makofi ya kutosha mezani? Inamaana wao hua hawaoni mapungufu ya kimkataba mpaka walio nje nje ya mfumo ndio wapige kelele? Kibaya zaid wapiga kelele wana hoja. Je lengo hua ni nn? Hawana uzalendo bali huangalia zaid maslahi binafsi? NB; Unapogundua kuna ufisadi na ubadhirifu but hawachukuliwi hatua stahiki wahusika je hii inamaana gan!! Majibu toka kwa wana CCM wenzangu ni muhimu zaid.
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Done ✔️
 
Matatizo mkuu mawili
1. Ujinga, wanasheria wengi wa serikali ni mbumbumbu haswaa, hawa practice sheria kabisa. Ni rahisi kupigwa chenga na ndio maana hata tukishitakiwa wakati fulani serikali huwa inalipia mawakili binafsi kuitetea

2. Ubinafsi na kukosa uzalendo. Viongozi wengi huchukulia nafasi zao kama 'fursa', hivyo kwenye kila jambo wanaangalia maslahi yao kwanza. Na huu ni utamaduni wa watanzania wengi. Ndio maana ukipata uongozi kama hauibi na kufanya makubwa watu wanakucheka kuwa ni 'mjinga'.

Usitatjie miujiza Tanzania, watu wengi ni wezi na mafisadi, tofauti ni fursa za kupiga tu. Hata hao wapinzani ni wezi tu.
 
Usitatjie miujiza Tanzania, watu wengi ni wezi na mafisadi, tofauti ni fursa za kupiga tu. Hata hao wapinzani ni wezi tu.
Upo sahihi ✔️!! But ukiangalia ni nn kinafanya watu wawe wezi wakipata madaraka? Au mtu anataman apate nafas mahal nayeye aibe? Upande wa wanasheria wa serikali nadhan c kwamba hawana uelewa au sio wasomi!! Tatizo ni kutetea jambo ambalo ni uongo, issue ya mikataba tatizo lipo kwa wanaoitaka hiyo mikataba kwa maslah binafsi ambapo wakili hana nguv mbele yao!!
 
Uzalendo usipokuingizia pesa huo ni sawa na upuuzi tu. Fursa zote wanawapa watoto wao.
 
Back
Top Bottom