GE2025 Je, CCM inaimarisha utulivu wa nchi au inaunda kisima cha upinzani mkali kwa kizazi kijacho?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

its MalekoGJ

Senior Member
Joined
Aug 27, 2020
Posts
136
Reaction score
292
Je, CCM inaimarisha utulivu wa nchi au inaunda kisima cha upinzani mkali kwa kizazi kijacho?

Na… Je, CHADEMA ni sauti ya wananchi au ni chapa ya kisiasa inayofaidika na kukandamizwa?

Siasa ya Kimya ni Siasa ya Ukombozi: Athari za Kuzuia Mawazo Katika Taifa Linalozinduka

Katika Tanzania ya leo, ambapo vijana wanakaa kwenye mitandao ya kijamiii kama X zamani Twitter,Telegram na Ata Instagram kuliko kwenye mikutano ya Siasa wanasiasa wameingia kwenye vita ambavyo si tena vya kura bali vya taarifa.
Lakini taarifa ipi inamilikiwa? Ipi inazuiwa? Ipi inapewa spotlight?

UDHIBITI — UTAWALA AU UOGA?

Serikali inapozuia mikutano ya hadhara ya upinzani kama Ilivyofanya Hapo awawali , kufungia akaunti za mtandaoni, au kufungua kesi nzito dhidi ya wakosoaji kama Tundu Lissu, hoja inayotolewa mara nyingi ni “kulinda amani ya taifa.”

Lakini maswali yanazidi kujitokeza
Ni lini udhibiti wa taarifa unageuka kuwa ukandamizaji wa fikra?

Je, wananchi hawana haki ya kusikia pande zote na kuamua wenyewe?

Tunajenga taifa la raia huru au taifa la wapambe wa upande mmoja?

UPINZANI WA KUDHIBITIWA UNAGEUKA KUWA UPINZANI HALISI

Jaribio la kisiasa la kuifanya CHADEMA ionekane kama hatari linawafanya vijana wengi kuiona kama "chaguo lenye uhalisia."

Ukandamizaji Unaofanywa dhidi ya chama hiki umekuwa “ushahidi wa uthibitisho.”

Tundu Lissu anapofunguliwa kesi ya uhaini, anajengewa picha ya

Mzalendo mwenye msimamo

Mtu asiyeogopa mfumo

Shujaa wa mitandao ya vijana

Hili si jambo la bahati ni athari ya moja kwa moja ya The Streisand Effect katika siasa.

1. Je, udhibiti wa midahalo ya kisiasa unadhibiti migogoro au unaihifadhi kwa vizazi vijavyo?

2. Je, upinzani ukikosa jukwaa la hadhara, unazidi kudhoofika — au unapata ushawishi mpya mitandaoni?

3. Ni nani mwenye hofu zaidi — chama tawala au chama kinachonyamazishwa?

4. Je, Tanzania ina hofu ya upinzani au hofu ya wananchi kufikiri tofauti?

5. CCM inaamini bado iko madarakani kwa ridhaa ya wengi — au kwa nguvu ya mifumo?

Katika historia ya mataifa mengi, wakati ukandamizaji wa kisiasa unapozidi, ndipo uhalali wa upinzani unapoanza kujengwa.
Haitaji manifesto — inahitaji tu ishara ya kunyimwa nafasi.
Na kwenye zama za digitali, hilo linatosha kuunda mabadiliko.

Unakubaliana na hoja hizi?
Au unaamini kuna sababu halali za kuzuia baadhi ya sauti zisisikike?

👇 Acha comment yako hapa chini.
 
[emoji116] Acha comment yako hapa chini.
Umenena kweli wale hopeless people wa kijani ilitakiwa haya wayajadili kwenye vikao vyao.
 
Mimi mwana CCM ila napata mashaka sana na propaganda tunazojilisha wenyewe tunajidanganya wenyewe kwa faida ya nani? Hata mtoto mdogo wa darasa la pili anaweza kua anatushangaa chama ambacho kinasema kina wanachama milion 13 kinaogopa uchaguzi wa Usawa wakati kina mtaji wa watu milion 13 tufanye reform tuweke usawa kama kweli tuna hao wanachama milio 13 tunagopa nini? Ina maana viongozi hawafanyi vizuri kwa wananchi ndo maana wanogopa reforms CCM ni mda sasa tubadilike tuendane na wakati uliopo mambo ya kuishi kwa mzoea ni kubaya sana Tuleta viongozi wanaokubalika kwa wananchi sio wale tunaolazimisha wakubalike wakati ni kinyume chake
 
Subiri upewe names
 
Back
Top Bottom