Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition?

Ukomavu wa chama cha siasa hususani Tanzania unapimwa kwa vuwango vipi kaka?
Uchaguzi was EALA uligubikwa kisiasa zaidi bila kujali umuhimu wa ushiriki wetu katika shirikisho,kwa kuona hilo wenzetu jirani zetu walionyesha umakini na walichokikusudia tofauti na Tanzania.
Siasa za maagizo na mwingiliano wa mihimili ndiko kunako pelekea nchi kufikiri siasa zaidi kuliko utendaji.

Hata kama CDM wangempeleka malaika kwenye uchaguzi ule,kwa kuwa bunge ilijikita zaidi kwenye ushabiki wa kisiasa kuliko maslahi ya nchi lazima wangedhoofishwa kwa namna moja au nyingine.

Maturity ya upinzani ina sustain daily kutokana na aina ya siasa tunazofanya,serikali kupitia vyombo vyake vya dola inatumia kila njia kuhakikisha Uhuru unaminywa,hata wanahabari mmeambiwa msidhani mna freedom to that extent kwa aina hii utegemea maturity ipi ikiwa pamoja na makando kando haya serikali but they still prevailing.
 
Kwa kweli upinzani uliokuwaga chini ya Slaa niliupaga matumaini kuwa ungekuja kuwa serious zaidi na more credible kuongoza nchi, ila kitendo kilichofuata baada ya lowassa kukatwa sisiemu na kupokelewa kwa shangwe kama ndo mleta mabadiliko kilinipa alama kubwa ya kiulizo uwezo wa upinzani, na baada ya hapo kuna vitu vidogo ambavyo vimekuwa vikitokea, ambavyo kwa kweli vinahitaji busara tu ya viongozi ambayo busara hii huletwa na ukomavu ila wameshindwa kabisa kudili na hivi vitu vidogo, hivyo kuwapa nchi hawatoweza, upande mwingine tuseme wameshinda uchaguzi sababu watu wameichoka sisiemu bado mambo yataenda kuwa mabaya zaidi kuliko yalivyo simply sababu ya immaturity.
CCM licha ya kwamba imechokwa, bado haina mbadala! Mbadala atakapopatikana, tutaiweka pembeni waangalie gemu kwanza wakiwa nje ya ulingo.
 
Chama hakiwezi kuwa komavu kama wananchi ni legelege. Vyama vya upinzani vimefanya mambo mengi yakutosha isipokuwa tatizo ni watanzania tope kichwani
Mambo yapi? Kubadili gia? Kutumia matukio kujinadi? Kuacha kuelezea sera zao kwa wananchi bali kuvizia sisiemu wataenda kukosea wapi? Kurumbana wenyewe kwa wenyewe na kusingizia sisiemu inawavuruga??
Immaturity & hupocrisy are the words here that fit the bill!
 
"Toka ccm wamechukua utawala wa nchi kugoka kwa chadma mika 54 ili yopita ndio mnagundua leo ufisadi wa serikali iliyokuwa ya cdm ndio mnagundua leo wafanyakazi feki wenye vyeti fake waligushi vyeti na ambao vyeti vyak havikukamilika, miaka 54 umakini uko wapi basi serikali jliyokuwapo na utawala wa chadema haufai lakin zaidi na huu uliopokea ndio haufai zaidi.
 
Nmekuwa nikifuatilia sana post zako mkuu...... you are an asset kwakweli kwenye hili taifa

Big up mkuu
 
Hakuna aliyesema kuwa CDM is smart!! Labda kama umejito ufahamu, lakini ni muhimu kujua chochote kibaya kwa CDM, kwa CCM kitakuwa kibaya zaidi!!! Hivyo kama CDM in immaturity, CCM itakuwa more Immaturity. Kama CDM itakuwa Hypocrisy CCM itakuwa more hypocrisy. Wenye akili wanachagua chenye unafuu!! "choose the less evil". Wewe unachagua ipi?
 
Kushinda uchaguzi huwa ni referendum mbaya dhidi ya watawala siyo kura dhidi ya wapinzani.

Uchaguzi ni kuwapima watawala siyo wanaotaka kuwarithi.

Kwa hiyo huu uchambuzi umeteleza vibaya mno.

CCM hawawezi kuendelea madarakani kwa sababu ya mapungufu ya upinzani bali kwa kutekeleza ilani ya uchaguzi iliyowaweka madarakani.

Jikite juu ya hiyo ilani au kanywe togwa
 
Chama kinachopambana na vyombo vya ulinzi na usalama kinashindaje kwa mfano, haohao wenye dola unaotegemea wakupe Ikulu ndio unaowananga daily, hii ina maana huwaamini sasa kama huwaamini ndio wakupe nchi..sahau. Chama hakishindi Urais kirahisi kama mnavyodhani bila system kusema yes, wee unafanya upuuzi wote alaf utegemee maajabu sahau, nchii hii ni muhimu sana kuliko Mbowe na chama chake
 
endelea kuota
 


Mungu asaidie tu Mh achagua RC Wa Kilimanjaro, hizi RIWAYA hamtaziona tena.
 
Kilichotokea Kenya, ni matokeo ya kitu kinachoitwa uwepo wa serious and credible opposition.

Sisi Tanzania safari bado ni ndefu,

Paskali
 
Kilichotokea Kenya, ni matokeo ya kitu kinachoitwa uwepo wa serious and credible opposition.

Sisi Tanzania safari bado ni ndefu,

Paskali
Huku tuna wapiga kelele na wabinafsi tu.
Mtu anapanga mawakili wasuse kwa umakini mkubwa akitambuka siku ambayo anatakiwa kutetewa mahakamni,mtu mbinafsi kama huyo hawezi kutegemewa kuwavusha watu kuelekea nchi ya ahadi
 
Kilichotokea Kenya, ni matokeo ya kitu kinachoitwa uwepo wa serious and credible opposition.

Sisi Tanzania safari bado ni ndefu,

Paskali
Hawa ndio wanasheria wetu na hizi ndio hoja wanazojijenga. Kwa staili hii tusitegemee kuwa na demokrasia kama ya Kenya. Anachomekea maneno ya Kiingereza hapa na pale halafu anahisi kama ametoa hoja? Anashindwa kuzungumzia katiba ambayo inafanya uchaguzi uwe mchezo wa kuigiza! Anashindwa kuongelea Tume ya Uchaguzi ambayo viongozi wanachaguliwa na Rais na wapo pale kwa discretion ya Rais kitu ambacho kinapelekea kuwa na mgongano wa maslahi. Wakati huo huo, sheria ya uchaguzi inayosema matokeo ya uchaguzi yakishatangazwa na tume hakuna,mahakama inayoweza kutengua. Wakili/mwandishi makini angei-attack hii sheria kwani sio constitutional

.
 
Nimekusoma, nitakutembeza mitaa kadhaa.
P
 
Waona mbali wameangalia majaaliwa ya Chadema 2020, kama yanavyozungumzwa kwenye bandiko hili, wameamua bora wasepe mapema kama hivi.
Naendelea kusisitiza hawa wanaohama wasibezwe, kwanza ni haki yao, pili wanahoja za msingi, na tatu wameona mbali kuwa 2020, hakuna mpinzani atarudi bungeni, hivyo kuliko kusubiri 2020 upotee, wameamua bora wajihakikishie nafasi mapema, na kichocheo cha kuhama ni ile ile rushwa ya ahadi, ukihama, tutakusimamisha wewe.
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja? - JamiiForums
P.
 
Kama ni hivi kweli, mawakala wanyimwe vibali, na wakipewa wanaingia saa 6 mchana, jumuisho za kura watolewe kwa mtutu, na wakigoma wawekwe rumande, kwa haya watapita na nna wasiwasi 2020 turnover itakuwa ni ndogo sana, na kura nyingi zitakuwepo za kupandikiza, wangefantia la maana hizo pesa za marudio, wapelekewe vivuko wakerewe, majamha yasizidi kutokea manake visiwa vingi wanatumia mitumbwi ya mbao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…