Naomba kuanza na Msingi wa kisheria ( Legal principle) ya “Waiver of right principle” Waiving a right means that such a right cannot be claimed by that individual. Kwa tafsiri yangu isiyo rasmi ni kwamba, ukipewa haki na mamlaka au mtu na ukashindwa au ukasusa kutumia haki hiyo; huwezi kurudi kuidai haki hiyo wakati mwingine.
Bahati mbaya sana hiki hakisemwi na wenye maoni tofauti na haya, mimi naona ni mtego mkubwa sana ambao wanaojenga hoja kwamba Chama kiko sahihi kutokusaini Kanuni za Maadili jana tarehe 12.04.2025 wanaenda kukumbana nayo Mahakamani.
Kwa sababu nafahamu baadhi ya CSO/NGO zinapush kwenda Mahakamani kuishtaki Serikali ili Mahakama Kuu itamke kwamba Chama ambacho hakijasaini Kanuni za Maadili kina haki ya kushiriki uchaguzi.
Maswali ambayo Mahakama inaweza ikajiukiza au itawauliza wadaawa ni Je Waombaji walipewa taarifa ya kushiriki kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi!? Jibu litakuwa “Ndiyo”; kwa sababu ni kweli Tume ilipeleka mialiko kwa Vyama vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu kushiriki zoezi husika.
Kama jibu ni “Ndiyo”, Waombaji waliitikia mwaliko huo!? Jibu litakuwa “Hapana”.
Kwa Msingi wa “Waiver of right”tayari Waombaji watapoteza game ya kisheria kirahisi sana Mahakamani.
Kifungu cha 162 (2) Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024 kinatumia maneno lazimishi (mandatory terms “shall”) kwamba Tume, Serikali na Vyama vya Siasa vinalazimika kusaini Kanuni za Maadili.
Kifungu cha 162(3) kimeenda mbali kusema kwamba Kanuni hizo za Maadili zitaweka adhabu, moja ya masharti au adhabu za Kanuni za Maadili zilizosainiwa jana kwa mujibu wa Kanuni ya 1.5 (a) ni kutoshiriki uchaguzi.
Hii ni mantiki ya kawaida katika tafsiri ya kisheria ya “syllogism” kwa sababu ya premises ambazo nimezieleza hapo juu.
Kwa maoni yangu ya jumla, Chama kimeacha haki yake na hakina uwezo wa kuidai kwa msingi wa “Waiver of Right” ; Aidha, kwa msingi wa tafsiri ya kisheria ya kifungu cha 162 kama nilivyoeleza hapo awali na utaratibu wa kuchapisha Kanuni za kisheria kwa Mpiga Chapa wa Serikali kwa ajili ya kuchapwa kwenye Gazeti la Serikali, sioni Chadema ikiwa na nafasi ya kipekee kupewa nafasi ya kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi wa Mwaka 2025. Kwa sababu haki yao waliipoteza jana tarehe 12.04.2025.
Soma Pia: Mnyika: Sitakuwepo kuwakilisha Chama kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi 2025 kwenye Ofisi za Tume ya Uchaguzi
Kwa wasilisho langu; Chadema imepoteza haki yake yenyewe na haiwezi kuidai hapo baadae.
I humbly berg to differ na maoni ya Rais wa TLS Boniface Mwabukusi na Wakili Kilatu.