Je, CHADEMA wakubali au wasikubali Mdahalo wa Uenyekiti wa chama? Wenzenu CCM huwa hawakubali Midahalo

Umerudia rudia sana hii kauli;
Wenzenu CCM, wenzenu CCM!
Kwani Chadema CCM ni wenzao?
Ni kama ukutane na kundi la malaika uwaulize eti wenzenu mashetani wanafanya hivi au hawafanyi vile!
Pasco waombe radhi Chadema kwa kuwaambia CCM ni wenzao! Wangekuwa wenzao wangewaulia ndugu na wanachama wao?
 
Tuwashauri, ili chama kipate umaarufu zaidi; hapa wakicheza vizuri watakifanya kiwe kwenye madia time zaidi. Hili lilipangwa kisomi kwa kugeuza tatizo kuwa fursa. ccm wengi wao wanajikuta wanatamka Cdm kila baada ya lisaa hasa humu Jf
 
Ni kama ukutane na kundi la malaika uwaulize eti wenzenu mashetani wanafanya hivi au hawafanyi vile!
Pasco waombe radhi Chadema kwa kuwaambia CCM ni wenzao! Wangekuwa wenzao wangewaulia ndugu na wanachama wao?
Mbona Mbowe alisema ccm ni wenzake?
 
Paskali wewe ni kaka yangu lakini ulichoandika hakina maana. Uhurumiwe tu. Pambaneni na chama chenu, CDM hamtaiweza
 
CCM wanavyoogopa mdahalo sio ajabu wakawatuma Mapolisi waje wawakilishe kwenye mdahalo, I mean Virungu maji ya pilipili mabomu ya machozi ndio watafanya mdahalo kwa niaba ya Chama kilichochokwa kuliko vyote hapa kwenye Jamhuri ya Ndizi.
 
Maadam Heche kaingia kugombea u makamu, mnaonaje kama utangulie mdahalo wa u makamu kati ya Heche na Wenje, ndipo uje mdahalo wa uenyekiti kati ya Mbowe na Lissum?.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ