Je, CHADEMA wakubali au wasikubali Mdahalo wa Uenyekiti wa chama? Wenzenu CCM huwa hawakubali Midahalo

Je, CHADEMA wakubali au wasikubali Mdahalo wa Uenyekiti wa chama? Wenzenu CCM huwa hawakubali Midahalo

Umerudia rudia sana hii kauli;
Wenzenu CCM, wenzenu CCM!
Kwani Chadema CCM ni wenzao?
Ni kama ukutane na kundi la malaika uwaulize eti wenzenu mashetani wanafanya hivi au hawafanyi vile!
Pasco waombe radhi Chadema kwa kuwaambia CCM ni wenzao! Wangekuwa wenzao wangewaulia ndugu na wanachama wao?
 
Tuwashauri, ili chama kipate umaarufu zaidi; hapa wakicheza vizuri watakifanya kiwe kwenye madia time zaidi. Hili lilipangwa kisomi kwa kugeuza tatizo kuwa fursa. ccm wengi wao wanajikuta wanatamka Cdm kila baada ya lisaa hasa humu Jf
 
Ni kama ukutane na kundi la malaika uwaulize eti wenzenu mashetani wanafanya hivi au hawafanyi vile!
Pasco waombe radhi Chadema kwa kuwaambia CCM ni wenzao! Wangekuwa wenzao wangewaulia ndugu na wanachama wao?
Mbona Mbowe alisema ccm ni wenzake?
 
Wanadodi

Nimesikia nia ya kuandaa mdahalo wa wagombea uenyekiti Chadema.

Huu ni uzi wa swali la ushauri wa bure kwa Chadema, Je wakubali au wasikubali mdahalo wa wagombea Uenyekiti wa Chadema?. Wenzenu CCM huwa hawakubali midahalo!.

Kwa sisi tuliosoma zamani, tulikuwa tunafundishwa midahalo kwenye school debates, nimebahatika kusoma sekondari shule moja na Tundu Lissu mimi nikiwa nimemtangulia niko A level, yeye O level ila alikuwa mzuri kwenye school debates akitugalagaza hadi sisi kaka zake wa A level, hivyo ukimuweka Tundu Lissu kwenye mdahalo na watu vilaza vilaza, ujue hiyo ni suicide mission kwa huyo kilaza!.

Ili mdajalo uwe mzuri, lazima wadahiliwa wawe ni watu wanaolingana lingana kwa sifa kwa kuwa na watu ambao ni like variables.

Huwezi kuwadahilisha wadahiliwa wawili wenye sifa tofauti

Huwezi kufanya mdahalo huku mdahiliwa mmoja ni akili kubwa, na akili chemka, mwingine ni akili ndogo, na kilaza kilaza, automatically akili kubwa itamgalagaza akili ndogo!. Je mtakubali?

Huwezi kufanya mdahalo kati ya mtu mmoja ni msataarabu, gentleman, mtu mwenye shukrani , anazungumza kwa lugha ya kiungwa na kistaarabu na kuzungumza vitu vya kweli, ukamuweka na mtu roporopo, mpayukaji anyeyezungumza kwa lugha kali, asiye na breki ya ulimi, anaweza kupayuka uongo na uzushi wowote na kuwaaminisha watu uongo huo ni ukweli!, ataishia kumdhalilisha tuu bure huyo mstaarabu wenu!, je mtakubali?

Huwezi kumshindanisha mtu mpambanaji wa kweli, aliyekipigania Chadema kwa machozi, jasho na damu, ikiwemo kumiminiwa pyu pyu 38, 16 zikampata! ukamlinganisha na mtu aliyekabidhiwa chama kama sadaka kwenye kisahani cha chai na Ba Mkwe hivyo kujiona kama chama ni mali yake binafsi, huu ukiwa ni mwaka wake wa 20 kwenye uenyekiti na bado anataka kuendelea tena!, je mtakubali?.

Hivyo hili ni swali la ushauri wa bure kwa Chadema, je mtakubali au msikubali mdahalo wa wagombea Uenyekiti wa Chadema?. Wenzenu CCM huwa hawakubali kabisa midahalo!.

Kwenye uchaguzi mkuu wa 2010, TBC chini ya Tido Mhando ilianzisha kipindi cha Mchakato Majimboni, kilichofanya midahalo ya wazi ya wagombea ubunge, kikiendeshwa na Shabani Kissu, kila jimbo ambalo kipindi kile kilipita, CCM ilipigwa chini!, Elections 2010 - Mchakato Majimboni: JJ. Myika, Ubungo Yako, Njia Nyeupe hivyo baada ya uchaguzi ndio ikabidi Tido ndio vile tena!. Hivyo CCM hawakubali mdahalo wowote wa uchaguzi.

Tuwashauri vizuri Chadema, je wakubali au wasikubali mdahalo wowote wa wagombea Uenyekiti wa chadema?.

Hoja hii nimeileta haswa kwa kuzingatia wengi wa mashabiki, wafuasi, wanachama na viongozi wa Chadema, wana akili kama za yule mnyama nyumbu, wakiambiwa chaguo la chama ni kuendeleza usultani na mgombea wao ni Sultan Mbowe, wao wanasubiri tuu tarehe 20 January, kura zote kwa Sultani Mbowe, hivyo kukifanyika mdahalo kumhusisha Kamanda Shujaa Lissu na Sultan Mbowe, Lissu akamgaragaza Sultani wao kwenye mdahalo, kuna hatari akili za mnyama nyumbu zikawahama, akili za kibinadamu zikawarudia, watamtosa Sultani Mbowe na kumchagua kamanda Lissu, ambaye atawaingiza ikulu 2015!, manyumbu wao hawana haja na ikulu, furaha yao ni sultani wao tuu kwenye kiti cha usultani hata kama watakuwa wapinzani milele!.

Mimi nimewafanyia a comparative ya assets & liabilities za kuiingiza Chadema ikulu, Japo Lowassa Alikuwa a Liability CCM, Akawa Asset Chadema. Lissu is a Very Bad Liability, but is The Only Asset Chadema Has Kuwangiza Ikulu!. Je... ? hivyo kama Chadema wanataka kuingia ikulu, mtu wa kuwaingiza ni Lissu, wala hahitaji mdahalo na yeyote!, lakini kama lengo ni kuendelea kubunya tuu ruzuku, waendelee na Sultani wao.

Haya mambo ya vyama vya kubunya tuu ruzuku, nilishauri Ruzuku kwa vyama vya Siasa: Mnaonaje tumshauri Rais Magufuli aifutilie mbali ruzuku hii? Ni ufisadi, nikashauri Kuelekea 2025 - Pascal Mayalla: Vyama vya siasa visipewe ruzuku, viongozi wake wajitolee

View: https://youtu.be/kpOuytUa4O4?si=0CEA3qzDha1b5_HQ
Amini usiamini, ruzuku kwenye vyama vya siasa ikifutwa, Sultani asinge endelea kung'ang'ania madaraka mwaka wa 20 sasa!.

Namalizia kwa lile swali la msingi la uzi huu, Je tuwashauri Chadema wakubali au wasikubali mdahalo wa wagombea Uenyekiti wa Chadema?.

Paskali.

Paskali wewe ni kaka yangu lakini ulichoandika hakina maana. Uhurumiwe tu. Pambaneni na chama chenu, CDM hamtaiweza
 
CCM wanavyoogopa mdahalo sio ajabu wakawatuma Mapolisi waje wawakilishe kwenye mdahalo, I mean Virungu maji ya pilipili mabomu ya machozi ndio watafanya mdahalo kwa niaba ya Chama kilichochokwa kuliko vyote hapa kwenye Jamhuri ya Ndizi.
 
Maadam Heche kaingia kugombea u makamu, mnaonaje kama utangulie mdahalo wa u makamu kati ya Heche na Wenje, ndipo uje mdahalo wa uenyekiti kati ya Mbowe na Lissum?.
P
 
Back
Top Bottom