Kwa nini unafarijika kuwa mwongo? Wewe hakika utakuwa umebeba roho ya shetani.
Nina uhakika hata ungepewa mwaka mzima ulete ushahidi kuwa Lisu aliwahi kusema hayo, hutaleta.
Kwa wasiofahamu, huyu mleta mada mwongo, ameamua kubadili majibu ya Lisu alipoulizwa kuhusiana na CHADEMA kumteua Lowasa (RIP) kuwa mgombea kupitia CHADEMA.
Lisu katika kufafanua alisema kuwa kabla ya kumteua Lowasa walii-contract kampuni ya nje kufanya tathmini juu ya mambo muhimu kadhaa. Baadhi yakiwa ni mambo ambayo wananchi wanayaona ni muhimu sana kwao. Utafiti huo ulionesha kuwa agenda ya ufisadi, katika umuhimu kwa wananchi, lilikuwa ya 9. Kwa hiyo siyo Lisu aliyesema kuwa ufisadi ni ajenda namba 9, bali ni wananchi. Na hiyo ni kwa kadiri ya utafiti wa hiyo kampuni.
Pia kwa watu wenye influence ilionekana Lowasa ndiye mwanasiasa pekee aliyekuwa maarufu kuliko wengine wote, licha ya CHADEMA kumweka kwenye orodha ya mafisadi. Na Lisu alikiri kuwa jina la Lowasa aliliingiza kwenye orodha hiyo ya mafisadi kutokana na taarifa ya Bunge ambapo Lowasa alitajwa kushindwa kuwasimamia watu wa chini yake waliotajwa kwenye sakata la Richmond, na taarifa hiyo ya Bunge haikusema kuwa Lowasa alihusika moja kwa moja. Uwajibikaji wake ulikuwa wa kisiasa. Taarifa ya kamati ya Bunge iliwataja waliohusika moja kwa moja na ambao kamati ilisema wagikishwe mahakamani, lakini Serikali haikufanya hivyo.