Je, chama kikongwe kitatumia dodoki gani ili kisafishike kitakasike?

Sio mimi bali ni gazeti lililoandika habari zake na kumpa title hiyo
Na kwa ufahamu wangu tafsiri yake ni mauaji mfuatano.. Zingatia neno SERIAL
 
kinyesi hata upulizie pafyumu vipi kimegoma
 
Nchi zingine wakijua polisi mnyanyasaji humfuata mtaani na kumkomesha kama kenya polisi watesi wengi walipigwa sana walipojichanganya mitaani
 
Unyanyasaji wa Polisiccm umewachafua ccm kwa kiwango cha kutisha
 
Zanzibar pemba na sehemu zingine watasoma visomo kulujuani Alibadiri kali kwa wale Polisiccm wote walioshiriki vitendo haramu vya kishetani dhidi ya chadema
 
Kuna Samia Squad
 
Lina kitubio. Je chama cha mauaji kinaweza kutubu na kikatubika? Jibu ni hapana!
SANA. NDIYO.
Kitubio ni kwa waTanzania wenyewe. Ndio mapadre kwa niaba ya Mungu.
Kufanya hivyo maana yake ni kusafisha, sio na dodoki la kawaida; bali 'scrubber' la chuma.
Kuondoa uchafu, kutupa mbali viongozi wabovu kama huyu aliyepo sasa na kukirudisha chama katika misingi yake ya kuwa chama cha wananchi; wakulima, wafanya kazi, wafanya biashara na wengine wote.
Uongozi wa chama ni lazima uwe ni kwa 'merit'; kufuatana na uwezo na sifa za mtu, siyo vigezo vya "Huyu ni mwenzetu" kama ilivyo sasa.

CCM ikirudi kwenye misingi hiyo, hata vyama vya upinzani vitajirekebisha viweze kuleta ushindani. Vile vyama vinavyo ishi kwa kutegemea kunyonya uchafu toka kwa CCM chafu, kama CUF na wenzao vitapotea.
 
Labda..

Tunarudia, LABDAπŸ™...
 
CCM ikirudi kwenye misingi hiyo...! πŸ₯ΊπŸ₯Ί never on earth!
 
Zanzibar pemba na sehemu zingine watasoma visomo kulujuani Alibadiri kali kwa wale Polisiccm wote walioshiriki vitendo haramu vya kishetani dhidi ya chadema
πŸ’ͺ🏿πŸ’ͺ🏿πŸ’ͺπŸΏβœŒπŸΏπŸ“ŒπŸ”¨
 
Mkuu 'Castr', heshima mkuu.
Sikumbuki kuwahi kukusoma humu JF, hadi leo. Ninaweza nikawa siyo sahihi, kwa vile sijasoma hoja iliyonivuta kama hiyo hapo juu iliyonifanya nimtambue aliyeiweka hapa.

Ni kweli, chama cha siasa kwa kawaida ni budi kiendeshwe na 'ideology', nadhani hii ni 'fact' isiyohitaji upinzani.
Lakini ninacho pishana na wewe, ni msisitizo wa maneno yaliyo fuatia, uliyotumia kama utetezi wa chama cha Mapinduzi.

Mkuu, CCM ya leo, unajuwa 'ideology' yake? Unasema 'ideology' hazifi,..., kwa hiyo CCM ya leo ni chama cha wakulima na wafanya kazi; kinacho amini katika 'ideology' ya ujamaa? Unaamini hivyo, kweli?

Hao wafuasi 12 milioni nchi nzima unaowazungumzia, unao uhakika leo hii wanajua vyema'chama chao kinasimamia nini? Unao uhakika hawa watu wamo ndani ya CCM kwa sababu ya 'ideology' yake inayo wavutia? Utafiti huu uliufanya lini, au nani alifanya na matokeo yake tushirikishe nasi tupate kuyachambua.
Hii CCM imekuwepo kwa miaka mingi kwa JINA; na kwa kweli huko nyuma kilikuwa ndiyo chama pekee hapa nchini. Wananchi wengi kwa sababu mbali mbali iliwabidi wawe wa chama hiki. Wengi wao hawajapata kubadili uanachama wao, wamebakia huko huko, si kwa sababu wanavutiwa na 'ideology' hewa ndani ya chama hicho. Kwa hiyo ni makosa kufikiri kuwa hawa wanachama 12 milioni ni wanachama wakereketwa wa chama hicho'
Unajuwa ni wanachama wangapi wapya ndani ya chama hicho; wote wameingia huko kwa sabau za 'ideology'? Maslahi ya kupata uongozi je; kufaidika binafsi kutokana na kuwa mwanachama wa chama kilichopo madarakani?

Mkuu Castr, nisikuchoshe. Ngoja nimalize kwa kukuomba uvumilivu; itokee kwa namna yoyote ile kuwa CCM ipoteze dola. Iondolewe madara

Naomba uniwie radhi kama humo ndani yamo makosa ya kiuandishi, kwa sababu nilikwenda mbio tu kuyaweka haya niliyo yawasilisha. Lakini ni matumaini yangu makubwa kwamba nitaeleweka vizuri tu, pamoja na makosa hayo.kani. Baada ya hilo kutokea, njoo hapa tena tuwajadili hao wanachama 12 milioni walioko huko ndani ya CCM kwa sababu ya 'ideology' ya chama hicho.
 
CCM ikirudi kwenye misingi hiyo...! πŸ₯ΊπŸ₯Ί never on earth!
You have to learn, never to say never again!
Naamini kwa dhati kabisa, inawezekana. lakini pengine unanielewa vibaya. Sipendekezi irudi ilivyokuwa kwenye miaka ile ya Mwalimu Nyerere, ya Ujamaa. The world has moved on, hata Mwalimu Nerere mwenyewe angerudi leo na kuchukua hatama hawezi kuirudisha CCM ile ile ya miaka hiyo. But the principless of human respect, independence, etc, rare commodities today in that party, remain the same.
 
Mumuache anagawa tuzo na goli la mama πŸ€£πŸ˜‚ my country bhana ss milion 20 kwa kalamu ili hali zahanati hazipai sana πŸ€£πŸ˜‚πŸ˜‚
 
But the principals of human✌🏿 respect, independence, ets remain the sameπŸ“ŒπŸ”¨βœŒπŸΏ
 
Dodoki la CHUMA TENA KIGUMU KAMA TALUMA LA RELI πŸ€£πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜‚
 
CCM wameisha poteza maana nzima ya kuwa kiongozi. Hivi unakuwaje kiongozi unaye tengeneza matatizo kwa unao waongoza. Yaani mtu unataka uwe raisi au vmbunge kwaajiri ya kuiba ,kuuwa, kutesa, ,kufilisi , na kuuza rasilimali za umma kwa wageni halafu . Wewe unafurahia kuishi kwenye nyumba ya kifahari, na kutembelea gari zuri? Yaani unajuwa kabisa vitu ulivyo navyo hujavifanyia kazi yoyote umevipora kwa watu walio kuamini uwangoze halafu imani hiyo unaitumia kuwatesa. Huo sio tu ni unyama bali pia ni upungufu wa akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…