Je, chama kikongwe kitatumia dodoki gani ili kisafishike kitakasike?

Je, chama kikongwe kitatumia dodoki gani ili kisafishike kitakasike?

Mkuu 'Castr', heshima mkuu.
Sikumbuki kuwahi kukusoma humu JF, hadi leo. Ninaweza nikawa siyo sahihi, kwa vile sijasoma hoja iliyonivuta kama hiyo hapo juu iliyonifanya nimtambue aliyeiweka hapa.

Ni kweli, chama cha siasa kwa kawaida ni budi kiendeshwe na 'ideology', nadhani hii ni 'fact' isiyohitaji upinzani.
Lakini ninacho pishana na wewe, ni msisitizo wa maneno yaliyo fuatia, uliyotumia kama utetezi wa chama cha Mapinduzi.

Mkuu, CCM ya leo, unajuwa 'ideology' yake? Unasema 'ideology' hazifi,..., kwa hiyo CCM ya leo ni chama cha wakulima na wafanya kazi; kinacho amini katika 'ideology' ya ujamaa? Unaamini hivyo, kweli?

Hao wafuasi 12 milioni nchi nzima unaowazungumzia, unao uhakika leo hii wanajua vyema'chama chao kinasimamia nini? Unao uhakika hawa watu wamo ndani ya CCM kwa sababu ya 'ideology' yake inayo wavutia? Utafiti huu uliufanya lini, au nani alifanya na matokeo yake tushirikishe nasi tupate kuyachambua.
Hii CCM imekuwepo kwa miaka mingi kwa JINA; na kwa kweli huko nyuma kilikuwa ndiyo chama pekee hapa nchini. Wananchi wengi kwa sababu mbali mbali iliwabidi wawe wa chama hiki. Wengi wao hawajapata kubadili uanachama wao, wamebakia huko huko, si kwa sababu wanavutiwa na 'ideology' hewa ndani ya chama hicho. Kwa hiyo ni makosa kufikiri kuwa hawa wanachama 12 milioni ni wanachama wakereketwa wa chama hicho'
Unajuwa ni wanachama wangapi wapya ndani ya chama hicho; wote wameingia huko kwa sabau za 'ideology'? Maslahi ya kupata uongozi je; kufaidika binafsi kutokana na kuwa mwanachama wa chama kilichopo madarakani?

Mkuu Castr, nisikuchoshe. Ngoja nimalize kwa kukuomba uvumilivu; itokee kwa namna yoyote ile kuwa CCM ipoteze dola. Iondolewe madara

Naomba uniwie radhi kama humo ndani yamo makosa ya kiuandishi, kwa sababu nilikwenda mbio tu kuyaweka haya niliyo yawasilisha. Lakini ni matumaini yangu makubwa kwamba nitaeleweka vizuri tu, pamoja na makosa hayo.kani. Baada ya hilo kutokea, njoo hapa tena tuwajadili hao wanachama 12 milioni walioko huko ndani ya CCM kwa sababu ya 'ideology' ya chama hicho.
Chief utakua sahihi ukisema haujawahi kuona hii username kwahiyo isikusumbue sana kujiuliza ikiwa ni mara ya kwanza kuiona.

Umeraise observation sahihi kabisa ikiwa wanachama 12M wote wamevutwa kwenye chama kwa kupitia 'ideology' ya chama tangu kinaasisiwa. Lakini hapo hapo umenifunga kujibu chochote kwakua umeniuliza ikiwa nimefanya utafiti.

Ni kweli pia sijafanya utafiti.

Na kwakua sijafanya utafiti kila nitakachojibu utaniuliza tena ikiwa nimefanya utafiti. Tutakua tunafanya 'merry go round' na hatutafikia muafaka.

Ambacho kimewahi kufanyiwa utafiti na nikakisoma kilifanyiwa utafiti na Lecturer wangu wa Politics wa MNMA. Ambapo utafiti ulilenga kutafiti kwanini CCM inaweza kushinda kwenye chaguzi nyingi zaidi.

Utafiti uliona kwamba ni kwakua wapiga kura wengi ni wazee kuliko vijana, wakifuatiwa na watu wa makamo kisha vijana ni kundi la mwisho.

Kwa namna CHADEMA imejiendesha kwa miaka mingi kwa kuhitaji watu kuandamana, watu kugoma n.k ilikua inawalenga vijana. Hata hoja nyingi za CHADEMA ziliwalenga vijana na zikawavuta vijana.

Isipokua tukija kwenye boksi la kura, kijana atasema "Sipotezi muda wangu kupiga kura" ili kucounter hii kitu CCM imejikita kuanza kurecruit wanachama mpaka kuanzia ngazi ya msingi. Sijaona response ya chadema kwenye recruitment ya wanachama wapya.

Hata hivyo itakua very interesting kufanya utafiti wa ulichoraise kwa mwenye fund. Ideology ya CCM bado ni ileile, kwenye kadi yake imeandikwa.

Ni kweli siyo chama cha wafanyakazi na wakulima tena kwakua sasa kinapokea kila mtu. Mpaka jobless tupo, ila pia tukumbuke nyakati za chama kinaundwa na mpaka nyakati za sasa ni ngumu kuweka mipaka ya 'wafanyakazi na wakulima pekee'

Ujamaa umekua blurry, lakini practically kuna maeneo hii ideology ya ujamaa bado inafanywa. Haswa eneo la Afya. Serikali imekua ikihudumia wagonjwa na kila ambaye hana uwezo na kua kwenye kundi specific anapatiwa sehemu fulani ya matibabu bure bila malipo.

Serikali ina bima ya afya ya bei ndogo kabisa ya shilingi elfu 30 ambayo itahudumia wanafamilia 6.

Marekani, kiranja karika kupinga ujamaa mpaka akajikuta kwenye cold war na Russia, waligoma Obama alivyotaka kuanzisha Obamacare kwakua waliamini mtu hatakiwi kutibiwa kwa gharama za chini au ambazo hazipo kabisa. Wakiamini italeta uvivu.

Uliandika kitu kizuri, sijaona typo. Lakini sina utafiti utakaoback up majibu yangu kwa 12M members hivyo kwa hapo sijajibu chochote.
 
Je, mchafu anachafuka tena? Hapana!
Je, mchafu anachafuliwa tena? Jibu pia ni hapana.

Kutoka jina jema kabisa la chama cha wanaolima na wanaofanya kazi, kuendea majina mengine kama
Chama cha walafi
Chama cha chukua chako mapema
Chama cha majambazi mpaka chama cha mauaji/wauaji... Kuna kutakasika tena hapo!?

Achana na ile slogan ya Wagalatia kwamba ijapokuwa dhambi zako ni nyekundu kama damu yeye (aliye juu) atazisafisha ziwe nyeupe kama theluji... Hili ni la kiroho zaidi, ni la kiiimani zaidi na ni la kininafsi zaidi.. Lina kitubio. Je chama cha mauaji kinaweza kutubu na kikatubika? Jibu ni hapana!
Uchafu ninini?

Uchafu ni kuweka kitu kisichostahili mahali husika. Kuna uchafu wa kimwili/kimazingira na kuna uchafu wa kiroho/ wa kiimani.. Haya ni makundi mawili makubwa ya uchafu.. Lakini vilevile kuna aina anuwai za uchafu
Uchafu unaweza kuwa ugonjwa.. Ugonjwa unaweza kutibika ama usitibike... Je uchafu wa chama pendwa unatiba!? Unatibika? Jibu pia ni hapana!

Kuna uchafu unaosafishika na kuna uchafu usiosafishika. Hata kwa kutumia kemikali kali kabisa.. Je uchafu wa chama tajwa unasafishika? Jibu ni lilile HAPANA.

Cheza na vyote lakini usicheze na hivi vitu viwili
Ardhi
Uumbaji

Hivi ni tunu za kimbingu alizotunukiwa mwanadamu... Fanya vyote lakini usiinajisi ardhi kwa kuimwagia damu isiyo na hatia.. Huu uchafu hausafishiki... Hii dhambi haina msamaha wa kimwili wala wa kiroho.

Usicheze na uumbaji kwakuwa hauna mbadala wala vipuri.. Kama kuna kitu kinapaswa
Kulindwa kwa nguvu zote basi ni uumbaji
Kuogopwa sana basi ni uumbaji
Kuheshimiwa sana basi ni uumbaji

Jina baya la CHAMA CHA MAUAJI limetokana na kutokuheshimu UUMBAJI wala KUULINDA wala KUUOGOPA!
Uumbaji haudhihakiwi kwa namna yoyote ile!

Chama kimefika ukomo wa dhuluma, ghiliba, mateso, wizi na kubwa kuliko yote. Mauaji... Hili doa halifutiki...!... Na kadiri kinavyoua ndivyo ladiri kinavyozidi kuharibu na kujichimbia kaburi kubwa.

Baadhi ya 'serial killers' walianza kwa kuua mashahidi ili wapone na kesi za mauaji zinazowakabili.. Lakini kila walivyoteketeza roho moja waliacha nyayo za ushahidi na kujikuta wanazidi kuua ili kupoteza ushahidi mpya!

Chama kimechafuka, kimenajisika na kinanuka damu za watu wasio na hatia. Hakuna dodoki wala kemikali iwayo yote inaweza kukisafisha, kukitakasa na kurudi kwenye asili yake!

Chama Cha Majangili
 
Duh 🙄 !
😳 !
 
Marekani, kiranja karika kupinga ujamaa mpaka akajikuta kwenye cold war na Russia, waligoma Obama alivyotaka kuanzisha Obamacare kwakua waliamini mtu hatakiwi kutibiwa kwa gharama za chini au ambazo hazipo kabisa. Wakiamini italeta uvivu.
Siyo sahihi. ObamaCare hadi leo hii ipo inaendelea.

Sitaandika juu ya hayo mengine uliyo eleza kwa kirefu, ila tu pengine kusisitiza tu kuwa," CCM kuwa chama cha wakulima na wafanya kaz"i wakati huo, haikuwa na maana kwamba waTanzania wengine ambao hawakuwa katika makundi hayo hawakutakiwa kuwa wananchama wa CCM. Maana yake ilikuwa kwamba wananchi wote walitambulishwa kwa makundi hayo mawili.
Na ni muhimu pia kueleza kuwa hakuna mtu yeyote anayetegemea kwamba CCM ilivyokuwa wakati ule ingeendelea kuwa vilevile miongo yote; wakati dunia imekwisha sogea mbele. Ila kinachotegemewa ni kwamba, 'basic principles' za hicho chama zisingeweza kuwa zimesahaulika na kutupiliwa mbali kama ilivyo sasa.

Niseme pia kwa ufup tui, juu ya CHADEMA kutofanya 'recruitment' kama unavyo dai. Siwatetei juu ya hilo, lakini kimsingi sikubaliani na sababu unayoiegemea kwa wao kushindwa kufanya hivyo.
 
Nchi zingine wakijua polisi mnyanyasaji humfuata mtaani na kumkomesha kama kenya polisi watesi wengi walipigwa sana walipojichanganya mitaani
Lisu akitoka jela atawafungulia kesi Polisiccm wote walioshiriki vitendo haramu kuwaonea kuwapiga kuwabambikia kesi chadema na pia kule Zanzibar wanawasomea Alibadiri Polisiccm wote waliompiga makamu katibu mkuu chadema upande wa Zanzibar
 
Back
Top Bottom