Je, Chama kipya cha Umoja Party kinaratibu upandaji bei wa Mafuta?

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Salaam Wakuu,

Chama kipya cha Siasa kinachoitwa Umoja Party, inasemekana ni chama kinachofuata, Uongozi wa Hayati Magufuli. Inasemekana Vigogo wengi wa CCM wapo nyuma ya hiki chama.

Wafuasi wengi wa Umoja Party wanadai Rais Samia hafanyi kazi kama Magufuli, na Watu Magufuli aliowaamin kama Polepole, Mkumbo, Bashiru, wameondolewa ili kambi ya Samia itafune Nchi.

Kwakuwa Waanzilishi wa Umoja Party wapo CCM, wanaweza kuhujumu Kazi za Rais Samia ili kumuondolea umaarufu aloujenga kwa kipindi kifupi?

Nini kifanyike ili Watanzania waache kuhujumiana? Kwenye siasa hujuma kama hizi wanaoumia ni wananchi
 
Waliambia Kwa Nia njema na uzalendo uliotukuka,wakiwamaliza waliowaita wapinzani,kiuhalisia ni wenye mawazo ya kujenga na kulitakua taifa yaliyo mema,kuwa wangeanza kutafuna wao Kwa wao na Sasa yanaelekea kutimia.japo Kwa wakati ule wengine walidharau na kuishia kukenua meno TU,Sasa waache wayaone wenyewe ikiwa ni pamoja Naya umoja party😜
 
Kulifuta Bunge na kufunguwa Ukurasa Mpyaa wa Uchaguzi HURU na wenye HAKI

Hapo Mataga watakuwa rasmi WAMEFUTIKA
 
Tanzania ina watu wengi wenye akili sana..wengi tu. Sio lazima hao iliowataja wawepo kuongoza...
 
Hakina lolote
 
Tunaamini katika nguvu ya umoja, fikira chanya na maendeleo yanayonekana kwa macho, siyo ya kwenye makaratasi na mipango miiingi kama ya January makamba na isiyo na tija,!
 

Nchi muhimu yoyote lazima iwe na vyama mbadala vinavyotoa sera mbadala.

Hao watu ni wakina nani, hujuma gani wanazifanya? Tuambie.

Kupigania maslahi, kazi, ajira, biashara, usalama wa Raia ni hujuma kwa CCM.
 

 
V
CCM vs ccm pambaneni na hali zenu sisi wananchi hayatuhusu
 
Tunaamini katika nguvu ya umoja, fikira chanya na maendeleo yanayonekana kwa macho, siyo ya kwenye makaratasi na mipango miiingi kama ya January makamba na isiyo na tija,!
Chuki binafsi kwa January hazitamaliza matatizo yako
 
Reactions: Tui
A word
 
Mnahamisha magoli.

Sababu imebadilika toka ile tuliyoizoea ya Vita vya Ukraine , Magufuli mpaka hii ya Umoja Party.

Inavyoonekana mambo yamekua magumu huko mpaka inakosekana sababu ya kudumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…