Je, chanjo ya COVID-19 hairuhusiwi kuingizwa hapa nchini na hospitali binafsi au famasia?

Je, chanjo ya COVID-19 hairuhusiwi kuingizwa hapa nchini na hospitali binafsi au famasia?

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,391
Reaction score
3,849
Naomba kujua kama hospitali au pharmacy binafsi inaweza ikaruhusiwa kuingiza chanjo ya corona au Covid19 au ni swala lisilo hitaji kibali.

Je, kuna uhitaji wa kibali maalum ili kuingiza chanjo hiyo hapa nchini, maana ni dawa kama dawa zingine au chanjo kama chanjo zingine.

Ni sheria ipi inapiga marufuku uingizwaji wa chanjo kama ipo tusaidie kuijua na vifungu vyake.
 
Mambo yahusuyo afya ya wenye taifa ambao ni Watanzania wizara ya afya ndio husimama kuhakikisha kinachoingizwa ni sahihi kwa wakati sahihi na kwa watu sahihi. Hao wengine sekta binafsi husubiria maelekezo.

Nina swali kama ulipata corona ikakupiga kweli kweli lakini mwili ukapambana na ukapona kuna haja ya chanjo?
 
Haziruhusiwi kuingia hapa nchini kwa sababu Tanzania inamtegemea Mungu katika kupambana na Corona(Kwa mujibu wa Magufuli).Sheria inayozipiga marufuku ni Magufuli.Yaani Magufuli ndiye sheria yenyewe.Kinachoiongoza Tanzania siyo sheria bali ni Magufuli.

Magufuli kwa utashi wake alisema kuwa chanjo zinaeneza Corona kwa hiyo ukiziingiza hapa nchini imekula kwako!Unakumbuka alisema kuwa kuna watu walienda kuchanjwa nje wakaleta Corona ya ajabuajabu?
 
Jiwe kama jiwe yani, akiamua wanaume wote wavae misuli kuanzia leo inakua katiba utasikia wanavyounga mkono juhudi hizo
 
Back
Top Bottom