Je, China ina mkakati wa kutoa mikopo isiyolipika ili itaifishe rasilimali za wadeni wake!?

Je, China ina mkakati wa kutoa mikopo isiyolipika ili itaifishe rasilimali za wadeni wake!?

City Of Lies

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2011
Posts
4,925
Reaction score
6,137
za-660x371.jpg

Taasisi ya Kimataifa ya Fedha (IMF) imepata wasiwasi kuwa huenda China ina mkakati wa kutoa mikopo isiyolipika ili wataifishe rasilimali za wadeni wawanao wadai.
_______________________________________
Serikali ya Zambia ipo kwenye mazungumzo na China ili kuangalia uwezekano wa kuwapa Shirika la Umeme la nchi hiyo (ZEWASCO) hii ni baada ya kushindwa kulipa deni kubwa wanalodaiwa na Serikali hiyo.
_______________________________________
China imeonekana kuwa nchi rafiki kwa Mataifa ya bara la Afrika lakini inatabiriwa kuwa siku moja itayazika Mataifa hayo katika dimbwi la madeni makubwa.

Rasilimali za nchi zitakazoshindwa kulipa madeni zitataifishwa na uhuru wa kujiamulia mambo wa nchi utakuwa mashakani.

Millardayo.com
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Viongozi wa kiafrika wanapenda sana mikopo ya uchina kwa sababu haiji na vigezo vya utawala bora na haki za raia. Yaani viongozi wakiafrika wakisikia kuwa hautowabana kwenye ugali wao hata kama masharti ni magumu kiasi gani lazima wakuone ni msaada kwao.
 
No free lunch!Lakini ukweli ni huu,ikiwa nchi za Kiafrika zitashindwa kuinvest kwenye Applied Science ambayo siku hizi inaitwa technology,hatutaenda popote!!!Lazima tu invest kwenye research na uvumbuzi,ni muhimu iyo ikawa sera,then Africa itaweza kusogea,wacha tuonekane primitive lakinu tuvumbue vyetu....!!!!
 
Kweli mkuu 👏.
 
Ndiyo maana jiwe aliwapiga chini wachina kaenda zake japan na korea kusini. Mchina hafai
 
Serikali ya awamu ya nne nusu waingie mkenge. Bagamoyo na Bandar ya Dar watanzania wamshukuru waziri Nundu kuna mikataba kama ingesainiwa bandari ya Dar mngeisikia imezungushiwa uzio wa kichina. Mombosa mambo yameiva ni swala la muda yatatokea ya Zambia
 
Viongozi wa kiafrika wanapenda sana mikopo ya uchina kwa sababu haiji na vigezo vya utawala bora na haki za raia. Yaani viongozi wakiafrika wakisikia kuwa hautowabana kwenye ugali wao hata kama masharti ni magumu kiasi gani lazima wakuone ni msaada kwao.
No wonder wanalalamikia masharti magumu ya nchi za ulaya ila kuitawala kwao dunia Muda mrefu kunawafanya wa behave kama wazazi. Ila wengi wa wachambuzi na vyombo vya magaribi vimeonya kuna wasi wasi nchi zikachemka
 
Hivi tunakopeshwa na bastola kichwani au kwa raha zetu?

Hata benki ukishindwa lipaa deni wanakamata Mali zako. La msingi ni kukopa kwa tija
 
Hivi tunakopeshwa na bastola kichwani au kwa raha zetu?

Hata benki ukishindwa lipaa deni wanakamata Mali zako. La msingi ni kukopa kwa tija
Hiv utaratibu ukoje?
Nilidhani ukikopa unaweka dhamana kitu, sasa hapa kwenye hii mikopo ya nchi na nchi kuna dhamana inawekwaga?
 
"Wachina ni maLafiki wa kweri na ni ndugu zetu tangu zamani.., masharti yao ya mikopo ni mazuLi..." hiyo ni kauli ya Jiwe juzi kati wakati anazindua ujenzi wa chuo cha siasa na propaganda cha ccm huko kibaha, kinachojengwa na wachina..

Kuna siku tutatakiwa kuwa na viza na paspoti kuingia Dar
 
Back
Top Bottom