Je, Clatous Chama kuelekea Far Rabat kwa kishingo?

Li ngunda ngali

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2023
Posts
707
Reaction score
2,572
Yupo wapi mwamba wa Lusaka? Nani amemshuhudia akishiriki yahusuyo Klabu yake tokea arejee juzi?

Inasemekana, hata kwenye zoezi la kupimwa afya, hakuwepo! Vilevile, inadaiwa kaigomea safari ya Turkey.

Duru ndani ya Klabu yake zinatabanaisha, jamaa kapata offer ya haja kutoka kwa swahiba wake coach Kishingo pale atakapo hudumu na timu mpya huko Morocco. Na amemhakikishia namba ya kudumu.

Nahofia, hali ya hewa huenda ikabadirika ghafla pale Msimbazi na kuwa yenye mawimbi mengi!

Muda ni Mwalimu.
 
Shughulikia tatizo la kuchanganya R na L
 
Kishingo hayupo Far Rabat
ni vizuri zaidi kufanya uchunguzi kabla ujaleta uzi wako hapa
 
Chama sio mungu wa Simba Sc, Simba Sc ni timu kubwa walikuwepo wengi, wapo wengi, na watapita wengi...

Chama aondoke au abaki, bado Simba ni Simba tu, kuna mechi zake alikuwa anapatia, na nyingine alizingua...

Hao waarabu kama wana mahela waje hata sasa tufanye biashara..
 
Mmetoka kwa Baleke sasa umeona muongelee na Chama pia, mtachoka tu! Lakini wewe hata Kishingo hujui yuko wapi, utaaminikaje?
 
Acha unafiki, kama chama sio Mungu wa simba kwanini ile game amefanyiwa sub kipindi cha kwanza mlijaa povu hadi mkataka kumfukuza kocha?
 
Mi naona ni bora angeondoka ,kwa sababu kwanza haendani na mifumo ya kocha ,pili ashakua kirusi ndani ya krabu
 
Wao mbumbumbu wanasemaga hakuna simba bila chama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…