John Wickzer Mulholland
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 6,656
- 14,403
Kuna kitu ambacho siyo cha kawaida kwenye kesi inayomkabili bwana Hamis Luwongo aliyehukumiwa jana na mahakama ya kuu ya kanda ya Dar es salaam kwa kosa la kumuua mkewe kisha kuuchoma moto mwili wa mkewe.
Katika kuhakikisha inatenda haki, mahakama iliomba mtuhumiwa afanyiwe vipimo vya akili.
Issue inaanzia hapo.
Bwana Luwongo alifanyiwa vipimo vya akili na Daktari bingwa wa magonjwa ya akili Dk. Sadiki Mandari, kutoka hospitali ya taifa ya afya ya akili Mirembe.
Cha kushangaza ni kwamba ripoti ya kwanza aliyo present mahakamani inasoma kuwa mtuhumiwa bwana Luwongo alikuwa na matatizo ya akili. Ikabidi mahakama imuite daktari aje atoe ushaidi huo mahakamani.
Cha kushangaza, Dk. Mandari alipokuja mahakamani aliwasilisha ripoti kinzani na ile ya kwanza kitendo ambacho kilimkasirisha Jaji Mwanga.
Je, ni sahihi Jaji Mwanga kuishia kukasirika, au Dr. Mandari awajinishwe 1). Kwa kuidanganya mahakama; 2). Kukiuka maadili ya kazi?
View attachment 3251217
View attachment 3251182View attachment 3251178
Hivi ndivyo madaktari wa Tanzania walivyo.Kwa ambao hawawajui huwa wanawaona kwa nje madaktari ni wasafi ila mimi nawajua madaktari kwa ndani ni wachafu.
Madaktari waliwahi kuiaminisha ngazi ya maamuzi uongo kuhusu mimi ili ngazi hiyo ya maamuzi iamue kama wanavyotaka wao,nikadhulumiwa haki yangu.
Lakini Mungu si Dk D..........n wala Mungu si Prof. P...........e , Mwenyezi-Mungu alinifungulia njia nyingine ya kutoboa maisha, Mwenyezi-Mungu alinipeleka mahali pengine penye vinono na pesa ndefu kuliko udaktari.
Au hiyo report iliyowasilishwa mahakamani awali ilichakachuliwa!
Imagine huyo ni daktari wa hadhi ya juu kabisa kiasi cha kuaminiwa katika ishu critical kama hiyo. Then anafanya madudu kama thithiemu. pumbavu kabisa huyo, naye awajibishwe pia
Kutokana na kuwepo kwa UTATA huu mkubwa sana katika Ripoti ya Kitaalamu ya Utabibu kuhusu Afya ya Mtuhumiwa, basi upo uwezekano mkubwa sana wa Mtu huyo kuachiwa huru endapo kama atakata Rufaa katika Mahakama ya Rufani. Jopo la Majaji wa Mahakama ya Rufani watakuwa na kazi nyepesi Sana katika kutoa Uamuzi wa Kesi hii.Ana kesi ya kujibu
Huyo Daktari na huyo Jaji tayari wametengeneza na kusafisha njia ya ushindi kwa huyo Mfungwa.
Ripoti hizo zote Mbili za Uchunguzi wa Afya ya Akili ya huyo mtuhumiwa ambazo zimewasilishwa Mahakamani, zote kabisa ni BATILI hadi wakati huu.
Jaji huyo wakati wa Kuendesha Kesi hiyo, alipaswa kutoa AMRI ili huyo Mtuhumiwa achunguzwe Afya yake ya Akili chini ya Jopo lingine la Madaktari wengine mara tu ulipotokea utata huo wa Ushahidi wa Ripoti ya Daktari, lakini siyo kutumia ripoti yoyote ile ya Tabibu ambayo tayari imewasilishwa mbele yake.
Hoja ya Msingi hapa ni:-
Kama Daktari anakana kuitambua Ripoti iliyowasilishwa awali hapo Mahakamani na kudai kwamba siyo Ripoti Halali, Je, kuna UHAKIKA gani kwamba hiyo Ripoti ambayo aliyowasilisha yeye mwenyewe kwa mara ya Pili kuwa ni Halali????????
Hao Mawakili wa Utetezi wa huyo Mfungwa wanapaswa wakate Rufaa katika Mahakama ya Rufani, uwezekano wa Rufaa hiyo kushinda ni mkubwa sana hususani kutokana na hiyo Hoja nzito ya kuwepo kwa Mkanganyiko/Utata mkubwa sana katika Ushahidi uliowasilishwa Mahakamani ambao umetumika katika kumtia hatiani Mshitakiwa huyo.
Huyo Mshitakiwa/ Mfungwa atatoka jela.
All in all, This Case is not proved beyond the reasonable doubt!