Je, daktari katika kesi ya mauaji alipokea rushwa au nayeye alikuwa na matatizo ya akili alipotoa ripoti mbili kinzani mahakamani?

Au hiyo report iliyowasilishwa mahakamani awali ilichakachuliwa!
Imagine huyo ni daktari wa hadhi ya juu kabisa kiasi cha kuaminiwa katika ishu critical kama hiyo. Then anafanya madudu kama thithiemu. pumbavu kabisa huyo, naye awajibishwe pia
Ana kesi ya kujibu
Kutokana na kuwepo kwa UTATA huu mkubwa sana katika Ripoti ya Kitaalamu ya Utabibu kuhusu Afya ya Mtuhumiwa, basi upo uwezekano mkubwa sana wa Mtu huyo kuachiwa huru endapo kama atakata Rufaa katika Mahakama ya Rufani. Jopo la Majaji wa Mahakama ya Rufani watakuwa na kazi nyepesi Sana katika kutoa Uamuzi wa Kesi hii.

Huyo Daktari na huyo Jaji tayari wametengeneza na kusafisha njia ya ushindi kwa huyo Mfungwa.

Ripoti hizo zote Mbili za Uchunguzi wa Afya ya Akili ya huyo mtuhumiwa ambazo zimewasilishwa Mahakamani, zote kabisa ni BATILI hadi wakati huu.
Jaji huyo wakati wa Kuendesha Kesi hiyo, alipaswa kutoa AMRI ili huyo Mtuhumiwa achunguzwe Afya yake ya Akili chini ya Jopo lingine la Madaktari wengine mara tu ulipotokea utata huo wa Ushahidi wa Ripoti ya Daktari, lakini siyo kutumia ripoti yoyote ile ya Tabibu ambayo tayari imewasilishwa mbele yake.
Hoja ya Msingi hapa ni:-
Kama Daktari anakana kuitambua Ripoti iliyowasilishwa awali hapo Mahakamani na kudai kwamba siyo Ripoti Halali, Je, kuna UHAKIKA gani kwamba hiyo Ripoti ambayo aliyowasilisha yeye mwenyewe kwa mara ya Pili kuwa ni Halali????????

Hao Mawakili wa Utetezi wa huyo Mfungwa wanapaswa wakate Rufaa katika Mahakama ya Rufani, uwezekano wa Rufaa hiyo kushinda ni mkubwa sana hususani kutokana na hiyo Hoja nzito ya kuwepo kwa Mkanganyiko/Utata mkubwa sana katika Ushahidi uliowasilishwa Mahakamani ambao umetumika katika kumtia hatiani Mshitakiwa huyo.
Huyo Mshitakiwa/ Mfungwa atatoka jela.

All in all, This Case is not proved beyond the reasonable doubt!
 
Rushwa ni adui wa haki
 
Na angeenda kutetea ripoti ya awali angeumbuka na angepigwa nyavu! Lazima ingeombwa mshtakiwa akapimwe kwa Dr mwingine na majibu yangekuja tofauti na ndipo mtiti ungeanzia!
 
Hata DNA za majivu hazijaonyesha kuwa ni za mke wake. Hii kesi ni hatari
 
Unazungumzia hawa hawa madaktari ambao kipindi cha korona wote walikua kama wamesomea umeme?

Tanzania hatuna wasomi bwana, sie tunajua kukariri tu.
 
Huyo muuaji ana kiburi, majivuno, hautii, kiufupi ni mshenzi, anapaswa anyongwe haraka sana
Hizi siyo sifa za kumnyonga mtu, Personal character za mtu sioni kama zinahusika kwenye kufanya maamuzi ya hukumu.

Maamuzi ya hukumu yako kwenye ushahidi wa tuhumza za mshitakiwa. ikiwa ushahidi hautahacha mashaka hata kidogo, hukumu inatolewa.

Lakini Huwezi kumuhukumu mtu kwa sababu ya kiburi, Maringo na majivuno yake.
 
Dr.Sadiki Mandali hata yeye anafahamu kwamba yeye siyo psychiatric specialist pekee nchi hii, hivyo sidhani kama kwa sensitivity ya kesi iliyopo anaweza kuchezea report kama inavyoelezwa.

Kama itakuwa ni kweli alitoa report tofauti MAT na Ofisi ya Mganga mkuu wanatakiwa kumuhoji kuthibitisha hilo na aeleze kwanini kuna huo mchanganyiko wa report.

Kisha ikithibitishwa katenda kosa ama kwa uzembe au kutokujua achukuliwe hatua stahiki, na mamlaka husika.

Sijui wa tampa onyo, au karipio kali, au kusimamisha leseni yake kwa muda, au kufutiwa kabisa, au kufukuzwa au vyote.

Na hili ni swala nyeti sana hata kwenye mahakama kufikia maamuzi ya hukumu, Sasa sijui walitumia report gani na nani alifanya hyo determination ya report ipi itumike.

Na kama mahakama ili hisi Dakitari aliwasiliana na ndugu wa mtuhumiwa, mahakama ilipaswa kuikataa report hiyo ambayo tayari imeshapoteza uhalali, kwa sababu ule myororo wa siri na kitaaluma(professionalism) haupo tena.

Mahakama ilipaswa imtumie dakitari mwingine mwenye taaluma hiyo, kwa level ya huyo au wajuu zaidi yake au hata kama ni kutoka nje ya nchi.

Huwezi kufikia kutoa hukumu kwa Report zenye mashaka, nadhani hapa wakili wa mtuhumiwa naweza kuikataa report na kukata rufaa, tukaanza upya.

Anyway tuwaachie wao wataalam, sisi tuendelee na soga zetu za JF.
 
Kutokana na mkanganyiko huu katika Ripoti ya Daktari, Kesi yote kabisa inaonekana kuwa ni BATILI. Na hata Hukumu/Uamuzi uliofikiwa pia ni Batili.

Wakili wa Utetezi hapa anapaswa aandae Rufaa na kuwasilisha Mahakama ya Rufani ili Hukumu hiyo itenguliwe na huyo Mshitakiwa/Mfungwa aachiwe huru.

Kuachiwa huru kwa huyo Mfungwa ndio utakuwa Uamuzi mzuri zaidi kwenye Kesi hii lakini siyo kuamua kuirejesha tena Kesi hiyo Mahakama Kuu ili ikasikilizwe upya.

Nafikiri huyo Jaji baada ya kuchukizwa na matendo ya huyo Daktari ameamua makusudi kutoa Uamuzi wa namna hiyo kwa kutumia Ushahidi wenye utata na wenye mapungufu makubwa sana ya kisheria akiwa na uhakika kwamba lazima Hukumu yake hiyo itatenguliwa kwenye rufaa na Mshitakiwa kuachiwa huru.
Mimi naamini kwamba Hukumu yenye utata mkubwa sana wa namna hii haikutolewa kwa bahati mbaya na huyo Jaji.
 
Hii inaitwa critical thinking
 
Labda ni maagizo kutoka juu, lakini kwa akili za kawaida sioni sababu ya mtu judge kutoa hukumu kwa ushahidi wa kuunga unga.

Kama haaamini taarifa ya Dakitari alipaswa, aombe mamlaka husika MAT ama wamlete bingwa zaidi ya huyo kuhakiki taarifa au yeye aikatae mojakwa moja, au aombe ushauri kwa wenzake nini kifanyike, naamini wangeomba mtu mwingine amfanyie mtuhumiwa evaluation au hata mtaalamu kutoka nje kama inawezekana.

Huyo Dakitari inawezekana ali temper na report yake mwenyewe, alikula pesa akatoa report halafu alipogundua msala umekaa hovyo akatengeneza report nyingine.

Haiwezekani ndugu wa mtuhumiwa awe na taarifa za siri na za kitaaluma, lazima aliwasilianan naye na lazima alipokea pesa.

Haya ,mambo nchi yetu hii mpaka mama yao aseme takukuru chunguzeni, bila hivyo imeisha hiyo.
 
Huruma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…