Je, Demokrasia ni Illusion?Je, Umma unaweza Kuamua mustakabali wa Taifa ama ni kulishana Upepo?

Je, Demokrasia ni Illusion?Je, Umma unaweza Kuamua mustakabali wa Taifa ama ni kulishana Upepo?

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,436
Reaction score
4,756
Mwaka Jana 2025 tarehe kama ya Leo nilikuwa katika viunga vya jiji la Dar es Salaam.Hali ilikuwa shwari na waliokuwa wakishiriki katika mchakato wa uchaguzi walikuwa wakiendelea na kampeni katika hali ya utulivu.Hakuna ambaye aliamini kwamba yaliyotukia tarehe 29Oktoba yangetukia pamoja na kauli kadhaa zilizokuwa zikitolewa.

Mwaka huu 2026 tarehe kama ya leo nimeona nilete mjadala huu mwepesi hapa jukwaani ili nipate maoni ya wanajukwaa na zaidi ili tuweze kuamua mustakabali wa nchi yetu kwa pamoja na kwa utashi.

Utangulizi:
Kama upo hai wakati huu, na kama Tarehe 29 Oktoba 25 Hukupoteza Uhai wako,uhai wa ndugu zako au hata mali zako basi unapaswa kumshukuru Mungu.Huenda ama wakati wako ulikuwa haujafika ama tu hatma ili kuepusha na kutaka kushiriki moja kwa moja katika matukio ya siku ile.Swali la kujiuliza ni JE ungetoka unafikiri hali ingekuwaje?Je labda kungekuwa na mabadiliko?Labda na wewe ungekuwa sehemu ya takwimu za waliokufa?Au labda ungekuwa we ndie unaendesha serikali kupitia ama vyombo vya ulinzi au vyombo vya kisiasa Je Unafikiri kama ungefanya UAMUZI tofauti na uliofanya siku ile Je hali ya nchi ingekuwaje?hali yako ingekuwaje?

Je Demokrasia ni Hadaa?
Ukisikiliza maoni na mitazamo ya watu hasa linapokuja swala la Demokrasia unajiuliza swali moja.Je hii ni Demokrasia ni Uhadaa wa kisiasa au ni uhalisia wa maisha na taratibu za kibinadamu?Je Tunapoitazama demokrasia tunaiona kama ndio njia bora na sahihi ya kuweza kuamua mustakabali wa Maisha na jamii au ni hadaa tu na kulishana upepo ila sio kweli kwamba mchakato wa kidemokrasia unaweza kuleta mabadiliko ya kweli?

Je Umma Unaweza kuamua Mustakabali wa Taifa?

Swali Jingine la kujiuliza ni kwamba Je Umma unaweza kufanya uamuzi wa mustakabali wa TAIFA?Kama unaweza Je Unawezaje?na kama hauwezi nini basi maana ya demokrasia?Je ulevi huu we demokrasia umewahadaa watu ya kwamba wana uwezo wa kuamua mustakabali wao bila kuzingatia kwamba uamuzi huo hauwezi kufanywa na umma?

Nimechokoza tu mjadala ili kwa wale ambao Wanapenda codes;

Basi iwekeni Tarehe 1 November kwenye kumbukumbu zenu kwani kuna tukio limeanza kuonesha dalili ya kutimia hiyo Tarehe.Wapo wanaojaribu kulizui ila Bahati Mbaya sio la kuzuilika bali ni la kulipokea na kulitumia kwa ajili ya Uponyaji wa TAIFA.
 
Back
Top Bottom