Je, dereva usipofunga mkanda, ikitokea ajali airbag haitafunguka?

Farolito

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Posts
12,001
Reaction score
27,175
Wakuu,

Naomba kufahamishwa

1. Je airbag inaweza isifunguke kama dereva hukufunga mkanda wakati ajali inatokea?

2. Je abiria wa mbele nae kama hakufunga mkanda pia airbag haitafunguka?

3. Na Je ni ajali ya kugongana uso kwa uso,na kugonga gari/kitu kizito kwa mbele tu,au hata gari ikigongwa nyuma au upande airbag itafunguka?

4. Je airbag ikifunguka itahitaji kununua mpya au itarudishiwa hiohio?


Asante

 
1&2 Kufunguka kwa airbag hakutegemei mkanda. Airbag itafunguka kama kawaida ila kama hujafunga mkanda ajali ndogo ambayo huenda hata usingechubuka inaweza ikakuondoa duniani au kukupa wounds za maana tu. Hivyo ni vizuri airbag ikatumika pamoja na mkanda.

Pia ukumbuke during ajali hiyo airbag na seat belt zitakusaidia ikiwa total momentum yako ni 300KgKm/Hr au less yani mfano mtu mwenye uzito wa kg 60 akipata ajali at 50km/h anaweza kuwa salama. Ila zaidi ya hapo ni majanga.

3. Sijui. Ila kuna gari zina mpaka 10 airbags depending on which side colision imetokea.

4. Nayo sijui
 
Asante kwa maelezo mazuri,kwanini mwenye uzito wa kg 60 akipata ajali at 50km anakuwa salama kuliko mwenye uzito zaidi?

Pia kwanini kama hukufunga mkanda airbag ikifungua unaweza kuumia zaidi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  1. Ufunge mkanda au usifunge, inapotokea ajali, airbag lazima ifunguke.
  2. Airbag itafunguka hata kama aliyekaa seat ya pembeni kwa dereva hakufunga mkanda.
  3. Ukipata ajali ukiwa kwenye speed ya kuanzia 25km/hr airbag hufunguka...
  4. Utahitaji kununua airbag nyingine, ile itakua haifai na huwezi kuirudishia ile ile...


Cc: mahondaw
 
Asante mkuu, nimepata mwongozo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa maelezo mazuri,kwanini mwenye uzito wa kg 60 akipata ajali at 50km anakuwa salama kuliko mwenye uzito zaidi?

Pia kwanini kama hukufunga mkanda airbag ikifungua unaweza kuumia zaidi?

Sent using Jamii Forums mobile app

Katika maelezo yangu nimegusia kuhusu momentum kwamba inapotokea ajali huyo dereva au abiria anatakiwa kuwa kwenye momentum Isiyozidi 300KgKm/h. Mometum ni product ya speed na Mass ya kitu. Sasakama mtu akiwa na uzito zaidi ya 60kg at 50km/h then momentum yake itakuwa ni above 300 na hivyo itakuwa hatari kwake.

Kuhusu suala la airbag na mkanda. Ukisoma legislation ya seat belt wanakuambia ni mandatory kuvaa seat belt all the time. Pia during ajali, Seat belt ndiyo inayoweza kukuprotect wewe ubaki where you are na pia seat belt inasaidia kudistribute energy ya impact into your body na kuprotect hiyo isikuletee madhara. Hizo kazi haziwezi kufanywa na airbag.
 
Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inatehemea na aina ya gari...mgari yetu haya mengi tunayoendesha model zo 2000 huko airbag itafunguka aidha uwe umefunga mkanda au hujafunga...

Lakini kuna baadhi ya model mkanda unahusianishwa na airbag module.....hivyo ni lazima ufunge mkanda ili ku activate airbag module...

Unaweza kugoogle kujua kama gari lako ni lzima ufunge mkanda ndiyo Airbag ifanye kazi au laa..

Magari hayafanani.
 
Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…