Je Diamond akifa Leo hii Kiba atabaki kwenye ubora au atapotea kama Ray kigosi

py thon

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2016
Posts
2,476
Reaction score
4,448
Ndugu zangu wana JF mie sie mpenzi sana wa hili jukwaa ila kwa siku ya Leo imenibidi niingie hivyo hivyo

Miaka 7 nyuma Tanzania ilipiga hatua kubwa sana kwenye tasnia ya filamu na tasnia hii ilibebwa sana na nguli Kanumba na hakika Kanumba alikuwa kwenye peak na kufikia hatua kucheza filamu na magwiji wa nollywood .

Kanumba alichochea sanaa "bongo movie" kupendwa sana hapa nchini na kama ilivyokuwa kawaida kuna watu walitembelea nyota ya Kanumba na pasi ya kupepesa macho Ray kigosi alitembelea nyota ya marehemu Kanumba na ikatengenezwa beef kama la Mond na kiba na bifu lile lilileta ushindani na kumbeba Ray

Lakini tokea Kanumba afariki bongo movie nayo imekufa na Ray pia amekufa kisanaa ,Ray hasikiki kabisa ,nani anafuatilia kazi za Ray saizi ????


Pasi na shaka Ray alikuwa anatembelea nyota ya Kanumba.


tuje kwenye muziki kuna hawa wasanii 2 maarufu Diamond na Kiba na wasanii hawa wana mashabiki wengi mpaka kupelekea mgawanyiko wa timu kuna wanaojiita timu kiba na wengine timu diamond na kiukweli ushindani huu umechochea maendeleo kwa wasanii hawa haswa Ally Kiba .

Na Beef ya Diamond na Kiba naifananisha na ile ya Kanumba na Ray japo Ray alikuwa anabebwa kupitia beef ile ,tuweni wakweli msema kweli ni mpenzi wa Mungu in JPM voice ,Ally kiba ame-step up baada ya Diamond kufanya vizuri na beef lao limembeba sana

What If Leo hii Diamond kafa kama ilivyokuwa Kanumba je Kiba atabaki kwenye ubora huu au atapotea naye kama Ray kigosi ?

Je Kiba anatembelea nyota ya Diamond ?
Diamond akiondoka Kiba atabak kileleni?
 
Kuna posts zinaandikwa wakati mtu yupo uani, zinakuaga na mtiririko mzuri, hoja zinapangwa vyema mno, tatizo hua ni mada inayozungumziwa
 
tambua kwamba Diamond kamkuta Kiba ni msanii mwenye jina na ameshajijenga.
Diamond anajua Kiba ni legendary, tatizo la Diamond ana tabia za kiswahili ndio maana anapenda vimaneno maneno vya kijinga, anapenda malumbano kisa anaona yeye maarufu, wenzake walishakua maarufu toka kitambo
 
Kiba kwisha kabisaaaaaaa...... Maana kwa sasa anajikongoja kwa sababu tu ya mondi [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Hivi unajua kama kiba alikuwepo hata kabla ya Diamond na alikuwa anafanya vizuri tu.
 
Mkuu uzi huu sio hila timu kiba bhana munaulizwa about future munjibu about the past eti alikuwepo kabla ya mondi yaan akili zenu zimejaa stress
 
Alikiba alifanya muziki vikamshinda. Na akakimbia Game. Tukabaki watz hatuna wakutupa raha tunayoitaka katka muziki. Kijana akapanda , akapanda, akapanda Ally akajifanya anarudi, mara anataka kiti chake ndo tukaanzia hapo. Ila nikirudi kwenye uzi ni kwamba Kiba anatembelea nyota ya Dangote. Koz alifanya akashindwa akakinbia. Angalia Dangote anavofanya vitu vyake kwa hesabu kali. Na yipo systematic sana. Unajua km kiba katoa nyimbo kama tatu ivi lkn mapokezi yake ndo ivo tena. Ngoja tusibir akifa mtu. Tutajua km tutakuwepo.
 
Kwa muziki anaoimba sasa hivi ni lazima awe Kigosi
 
Uko sahihi mkuu Kiba yupo long time kwenye gem huyo midomo ni mtaka sifa kwenye social media pia ni mshirikina sana anayejiona yuko juu pia ana tabia za kike ndo mana anapenda mabeef ya kijinga
 
Wewe umwewakumbusha vema trend ya Kiba. Na aliposema nataka kiti changu clouds wakaingilia na lengo waliamini wangeweza kumpoteza diamond na kumpandisha kiba, inasemekana clouds walikuwa hawaelewani na Mond kwa sababu alikataa kunyonywa. Basi baada ya kupigapiga vi promo vya hapa na pale ndio imebaki hivyo hali leo, japo ushindani wao upo theoretically tu na si practically
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…