Ndugu zangu wana JF mie sie mpenzi sana wa hili jukwaa ila kwa siku ya Leo imenibidi niingie hivyo hivyo
Miaka 7 nyuma Tanzania ilipiga hatua kubwa sana kwenye tasnia ya filamu na tasnia hii ilibebwa sana na nguli Kanumba na hakika Kanumba alikuwa kwenye peak na kufikia hatua kucheza filamu na magwiji wa nollywood .
Kanumba alichochea sanaa "bongo movie" kupendwa sana hapa nchini na kama ilivyokuwa kawaida kuna watu walitembelea nyota ya Kanumba na pasi ya kupepesa macho Ray kigosi alitembelea nyota ya marehemu Kanumba na ikatengenezwa beef kama la Mond na kiba na bifu lile lilileta ushindani na kumbeba Ray
Lakini tokea Kanumba afariki bongo movie nayo imekufa na Ray pia amekufa kisanaa ,Ray hasikiki kabisa ,nani anafuatilia kazi za Ray saizi ????
Pasi na shaka Ray alikuwa anatembelea nyota ya Kanumba.
tuje kwenye muziki kuna hawa wasanii 2 maarufu Diamond na Kiba na wasanii hawa wana mashabiki wengi mpaka kupelekea mgawanyiko wa timu kuna wanaojiita timu kiba na wengine timu diamond na kiukweli ushindani huu umechochea maendeleo kwa wasanii hawa haswa Ally Kiba .
Na Beef ya Diamond na Kiba naifananisha na ile ya Kanumba na Ray japo Ray alikuwa anabebwa kupitia beef ile ,tuweni wakweli msema kweli ni mpenzi wa Mungu in JPM voice ,Ally kiba ame-step up baada ya Diamond kufanya vizuri na beef lao limembeba sana
What If Leo hii Diamond kafa kama ilivyokuwa Kanumba je Kiba atabaki kwenye ubora huu au atapotea naye kama Ray kigosi ?
Je Kiba anatembelea nyota ya Diamond ?
Diamond akiondoka Kiba atabak kileleni?