Unaona sasa unavopwaya? Hivi kila mtu angekupa pesa huyo mzazi wako ungemzika mwenyewe? Utabeba jeneza kwahizo pesa?
Nimekueleza kule kwenye ile comment bado hutaki kujifunza, pesa si kila kitu.
Kuna mama mmoja namfahamu alikuwa ni bosi mkubwa Barrick Minning, yeye misiba ya ndugu zake kwanza alikuwa halali msibani na wala hata kuhudhuria tu ni shida, lakini akipigiwa simu ni wa kwanza kuomba namba E-money ili achange na kweli alikuwa mchangaji mzuri sana.
Ikaja mume wake akafa na ndugu zake pia kila walipopigiwa simu walikuwa wanauliza namba ya M-pesa ili wamrushie michango, nilikwenda kwenye msiba ule kwa heshima ya rafiki yangu yule mama alikuwa analia kwa mengi.
Tangu tukio lile yule mama pamoja na kwamba bado ana pesa lakini kwenye misiba ya ndugu sasa hivi analala.
Sidhani kwa mtu mwenye akili ttimamu ni jambo la kujivunia unafiwa na mzazi na hakuna rafiki wa kuwasha gari yake kusafiri na wewe kukupa joto.
Ukitaka kuujuwa unafki wa hao unaodhani ni marafiki zako subiri siku Mzee Malecela Mungu amchukuwe utawaona kimbelembele chao maana wanajuwa ni channel ya kukutana kwa karibu na Rais na viongozi wengine waandamizi na watatowa magari yao mpaka Mtera.
Mark my word, maandishi yetu hapa JF huwa hayafutiki utayakumbuka haya.