Je, Diaspora wetu wana mchango wowote kuisaidia Tanzania kisiasa? Wana any influence kwenye siasa za nchi yetu? Angalia Diaspora wa India

Mkuu Pascal Mayalla hongera kwa mjadala. Wewe ni msomi na nina hakika unaelewa vizuri unachoandika. Umehoji mchango wa Diaspora kwenye SIASA.

Na SIASA ni "concept" inayoendana na matendo yenye lengo kuu la kushindania kushika madaraka. Siasa inaendana na matendo ya ki-HARAKATI.

Siasa inaweza kufanywa kupitia ushiriki kwenye vyama vya siasa au kwa njia nyingine, kwa mfano kupiga kura, kuongeza ushawishi wa kukubalika kwa hoja ("awareness-raising") kupitia maandamano, migomo, nakadhalika. Mfano ni huo wa Diaspora wa kihindi wafanyao harakati kuunga mkono BJP.

Kwa hiyo kwa kifupi Mkuu Pascal unahoji mchango wa Diaspora kwenye HARAKATI. Naona hili inabidi liwe wazi maana wachangiaji wanaleta mambo ya "makontena", "fursa", "utalii", nakadhalika!!

"Video clips" ulizoweka kwa kiwango kikubwa zinazungumzia changamoto ya Uraia Pacha. Ni hiyo ya mwisho ya mahojiano na Diaspora Ali Salim Ali ndio inatoa picha kidogo ya changamoto za ushiriki wa Diaspora wa Tanzania kwenye harakati.

Na hiyo story ya Diaspora wahindi nayo inaonesha changamoto za harakati na ndio maana mwandishi kakiri toka mwanzo kabisa, "The event, called the World Hindu Congress, was controversial"

Sasa ukioanisha hoja kuu uliyoweka ya ushiriki wa Diaspora kwenye siasa (harakati) na "video clips" ulizoweka zilizosheheni hoja ya Uraia Pacha, je ulitaka watu wajadili:

"Mustakabali wa Ushiriki wa Diaspora Kwenye Harakati na Hoja ya Uraia Pacha"?
 
Kiukweli diaspora wetu katika siasa zetu, ukiondoa individual efforts za diasporans kama Mzee Mwanakijiji, lakini diaspora wetu hawana mchango wowote katika siasa zetu.
P
 
Wewe Pascal uamuzi wa kuacha Uandishi ulikuwa sahihi lakini sijui kwanini umerudi na usibakie kwenye siasa. Kwenye siasa hutakiwi kutumia akili . Kama hao watanzania ambo wako hapo ndani wananyimwa haki ya ya kujiamulia nani awaongoze itakuwaje unaulizia Diaspora?
 
Hatuna tume ya uchaguzi
 
Ndio
 
Kwenye mahojiano na BBC, Rais Samia amezungumzia uraia pacha, unakuja!.
Big Up sana kwa Samia.
P
 
Diaspora wa India ukiwagusa tu mbaazi azinunuliwi, wale wananguvu kwao wanapeleka ajira pia Kodi India inaingia ,wakinunua kolosho kubangua India watu India upata ajila, dadadeki wa kwetu wao kudai urais pacha Kila uchwao
 
Anayekwamisha diaspora ya waTanzania kuchangia maendeleo nyumbani ni sheria za nchi ya Tanzania


15 December 2022

Ugumu wa Diaspora wa Tanzania kufanya biashara Tanzania vs Kenya

Diaspora wa Tanzania aliyechukua uraia wa nchi nyingine ana wakati mgumu sana kufanya biashara Tanzania, tofauti na kama akienda nchi nyingine ya Afrika Mashariki kama Kenya au Rwanda nk.

Source : EBM Swahili
 
Nakuunga mkono, mimi na wife wangu kwanza tulihamia UK, kisha US, mimi nimeendelea kuwa Mtanzania, mwenzangu ni US subject, nilipopata ile ajali, nimetibiwa na support from her!.

Watanzania wengi wanaojilipua, wanajilipua kwasababu ya circumstances na sio kuukana Utanzania wao. Turuhusu dual citizenship!.

Tukiruhusu dual citizenship, diaspora wetu, watafanya mambo makubwa kama diaspora wa India, Nigeria, Ghana na Kenya.
Haya mambo ya diaspora tumeyaongea sana humu

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…