Elections 2010 Je, Dr. Willibrod Slaa atatufaa?

Its a very interesting article with some facts. Lakini pia ni habari ambayo haina uzito wowote katika king'ang'anyoro cha Urais cha sasa.

Inanikumbusha Kampeni za Uchaguzi uliopita wa Wamarekani, kilikuwa na aina mbili za Uandishi: Unaomuunga Mkono Obama na Kumponda Mc Cain na ule Unaomuunga Mkono Mc Cain na Kumponda Obama. Hili ndilo linalotokea sasa kati ya JK na WS huku magazeti ya Uhuru; IPP Media; New Habari na yale ya Serikali yakiwa positive zaidi kwa JK wakati yale ya Tanzania Daima; Mwananchi; Mwanahalisi; (Raia Mwema?) yakiwa positive zaidi kwa Slaa nk.

Afterall unaweza kuiangalia glass yenye maji hadi katika kati katika namna mbili: Half-Full au Half-Empty. All these are issues of Mind and Attitudes.

As a matter of Fact utendaji Serikalini huwa haundani sana na maisha binafsi, ndo maana Wamarekani pamoja na Ufirauni na Ufuska wa Bill Clinton bado walimchagua tena kuwa Rais kwa kuwa utendaji wake ulikuwa mzuri..

The future can be made by looking at the past. Katika uongozi, Dr. Slaa ameonyesha njia alipokuwa Mbunge katika kuyashughulikia masuala ya Nchi na amefanikiwa. Palipo na ukweli tuseme ukweli. Katika hili, natofautiana sana na Mwandishi. Pia ikumbukwe kuwa hakuna chama chochote ambacho hakina tofauti baina ya wanachama wake au hata viongozi.

Mwenye Macho haambiwi tazama na wala mwenye masikio haambiwi sikia.
 

Mkulima Mimi,

..tunachohoji hapa ni kwanini Jenerali Ulimwengu akaji-associate na makala za kihuni-huni na kidini-dini kama hizi?

..Raia Mwema siyo kama Jamii Forums ambako anaweza kutokea mkichaa aka-post upupu wakati moderators wako off duty.

..binafsi nilikuwa naliheshimu sana gazeti la Raia Mwema, but not after they published this article.

..labda Jenerali Ulimwengu,Johnson Mbwambo, na waandishi wengine tunao waheshimu wako likizo, na walioachiwa ofisi ndiyo wamefanya madudu haya.
 
jokaKuu,
Nadhani Mkulima mimi kishajibu,
Makala hii ni personal opinion ya mwandishi. Hicho ndicho kitu Mwanajamii alijaribu kuficha. Jenerali kama publisher na editor asingefanya haki kwa kumnyima huyu jamaa kutoa maoni yake. Kwa hiyo tuliza boli. Now that we know it is a personal opinion and not a news item.
 
Slaa ni mtoto wa nyerere hana jipya :huyu ni ccm , akipata madaraka tutarudi zile enzi za nyerere kukaa foleni ya sigara . Hivi karibuni aliutembelea mzimu wa nyerere kule dodoma . Huyu mtu ni hatari sana .

Nadhani wewe ni hatari kuliko yeyote nimewahi kumsikia! Kama Slaa ni mtoto wa Nyerere na Kikwete ni Mtoto wa nani? na Mkapa? hawa wageni wanalo jambo hapa jamvini, hamna uchambuzi ni hisia hisia tu, bure kabisa
 
Mimi sidhani kama habari kama hii inaleta impact yeyote kwa wapiga kura kwa sababu iko very personal haigusi moja kwa moja maisha ya watu kama vile masuala ya rushwa ufisadi uvunjifi wa katiba wizi wa mali ya umma nk.

Hizi ni propaganda za CCM baada ya kuona uwezekano wa kum corner Slaa kwa issue zenye impact kwa watu ni mdogo. Kwa hiyo wanatumia any available weapon ili waweze kumchafua ukiwemo udini, kumjengea chuki, kujenga makundi ndani ya Chadema, ukabila nk.

Swala la upadri wa Slaa ni jambo dogo sana kwa sababu hata wanaojaribu kulitumia wanajua hata kama watafanikiwa halitawasaidia kwa kiasi wanachofikilia. Naweza kusema kadri wanavyoeneza ukatoliki wake ndivyo wanavyomleta karibu na jamii ya wakatoliki na wakristo ambao si haba kwa Tanzania.

Mwisho naweza kusema sidhani kama makala hii inaweza kuchapishwa kwenye gazeti la Jenerali Ulimwengu bila yeye kujua, anaelewa nini kinaendelea na ameruhusu kwa maslahi yake zaidi. Pamoja na Jenerali kuhusika au kutohusika na makala hii waelewe kuwa kiongozi wa inchi hachaguliwi kwa misingi ya dini.

Kwa historia ya Tanzania hakuna dini yeyote inayoweza kumweka rais madarakani bila kushirikiana na dini nyingine, na vilevile tusisahau kuwa kwa nchi kama yetu ni vigumu sana kupata kiongozi asiye na dini lazima tu atatokea ndani ya dini fulani. Labda cha kujiuliza kwanini mambo ya dini ya mgombea yanajitokeza leo, hatukuyaona wakati wa Mkapa na Kikwete kwenye term ya kwanza.
 
Hakuna atakae mpa kura Padre Slaa, huyu bado ni mtandao wa kanisa katoliki ametumwa, anajaribu kuwafumba macho wananchi kwa kutumia jf, ameshindwa kumkinaisha mkewe ahame ccm, mkewe hadi leo ni ccm damu.

Kumkabidhi padre nchi ni ku-commit suicide, ametumwa na mtandao aweze kusign memorumdum nyingine, watz hawatodanganyika kamwe!!
 
Acha niwe nimedanganyika kwa kumpa Slaa kura yangu, hata mje kwa gear gani 2010 HATUDANGANYIKI
 
Dada zako walisema hivyo hivyo. Ila siku hizi WANA WATOTO.
 

Ni kweli kabisa Slaa ana mkono wa kanisa nyuma yake ukitaka kujua hilo soma gazeti la Tanzania Daima la jana jumatano.Maaskofu wa mkoa wa Kilimanjaro wametoa waraka wa kumuunga mkono bwana Slaa.habari hiyo iko ukurasa wa tatu.
 
Nasikia 2Pac na Michael Jackson wanataka kumuunga mkono MZIRAY, Aisee!!!!

Padri una bahati kweli. Waja leo na waanza kutukana watu leo, mhhhhh!!!!!

Wee ndiyo vile Vibabu vya JF vinaingia upya JF kama mtoto wa Chekechea.

Ila ukiangalia ka uso, KAMEKOMAAA!! Hihiiiiiii

Ukitema mate yanaduna, hruuu hruuuu, unatoa unga....... Welcome Kibabu.

Ni kweli kabisa Slaa ana mkono wa kanisa nyuma yake ukitaka kujua hilo soma gazeti la Tanzania Daima la jana jumatano.Maaskofu wa mkoa wa Kilimanjaro wametoa waraka wa kumuunga mkono bwana Slaa.habari hiyo iko ukurasa wa tatu.
 
Ni kweli kabisa Slaa ana mkono wa kanisa nyuma yake ukitaka kujua hilo soma gazeti la Tanzania Daima la jana jumatano.Maaskofu wa mkoa wa Kilimanjaro wametoa waraka wa kumuunga mkono bwana Slaa.habari hiyo iko ukurasa wa tatu.
Mtajazana sana mwaka huu

Padri

Junior Member

Join Date Thu Aug 2010
Posts 1
Thanks : 1
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power
 

Tatizo lenu mafisadi wa dini mnajifanya kusahau (kuufumbia macho?) Uislamu wa Kikwete.Msilogwe kuwagawa wapiga kura kwa misingi ya dini kwani mtakaothirika ni nyie (takwimu kuhusu viwango vya elimu kati ya wakristo na wasio wakristo zinajieleza bayana).Katika kutapatapa kwenu mnaweza kujikaanga kwa mafuta yenu wenyewe.

Tumemvumilia Kikwete pamoja na udini wake lakini kwa vile mmeshalamba asali sasa mnataka kuchonga mzinga.Hamtaki kusikia Mkristo akiingia tena Ikulu.Mshindwe na mlegee.

Slaa ahukumiwe kwa uwezo wake wa kutetea maslahi ya Watanzania na sio imani yake ya kidini.Na mkileta hizo personal issues (family,etc),mgombea wenu ana skandali kadhaa ambazo naamini nanyi mnazifahamu.

All in all,hamtofanikiwa.
 

watu kwa makusudi yenu wenyewe au kwa kutumiwa mnapanda mbegu ya chuki dhidi ya wakatoliki, mnajua mnachafua dr. Slaa na chadema hamjui kuwa mnaandaa chuki dhidi ya wakatoliki kwamba wameamua kusimamisha mgombea. Nadhani hamjui ukubwa na uwezo wa kanisa hilo kama likiamua kufanya kweli kwa kumsimamisha mgombea, kwa jinsi mnavyolishutumu waziwazi nadhani msingesema slaa atashindwa maana nadhani kanisa katoliki ndilo linaongoza kuwa na watu wengi! Kwahiyo wingi wao ni ushindi tayari! Kwa kulishutumu kanisa katoliki sababu ya muumini wake dr slaa kuamua kugombea urais mnaanza kuzua maswali wakatoliki wanaanza kuhoji hivi mkatoliki hapaswi kugombea urais!?
Ila naanza kupata hisia kwamba inawezekana ccm miaka yote ilisapotiwa na kanisa katoliki mwaka huu inavyoonesha kanisa limegoma kwahiyo ccm inahisi moja kwa moja kanisa lipo nyuma ya mgombea wa chadema aliyewahi kuwa padre huo ndio wasiwasi wao mkubwa! Kwani wanaamini kanisa halijawahi kuwa neutral kabisa kwenye uchaguzi mda wote lilikuwa sambamba nao sasa kwanini leo kanisa halitaki kushirikiana nao tena!
Wadanganyika amkeni siasa sio kama ushabiki wa mpira wa simba na yanga hata mkifungwa mnatafuta sababu kuwa mlihujumiwa. Ushabiki huu wa chuki tena kwa makusudi unaweza usiishie hapa kwani kwa kusemasema jambo ambalo halipo mnawasaidia watu kuanza kuona uwezekano wa kufanya hilo huko mbeleni! Kama waliotuhumu hili wataliacha lipite na serikali ikafumbia macho basi mbeleni makanisa na misikiti vitasimamisha wagombea maana haramu imehalalishwa, mnawafunza wale ambao hawana mawazo kuanza kufikiria uwezekano wa kufanya hivyo! Kila mtu na imani yake lakini mambo ya ushabiki usio na maana hautatupeleka popote! Wanafiki endeleeni wanamapinduzi songeni mda utafika kila kitu kitakaa sawa......!!
 
Huyu dr slaa hafai hata bure.....dr slaa ni bora raisi sio rais bora na waswahili wanasema rais huwa ghali
 
Haiwezekni kigezo kikubwa kuwa ni dini tukiendeleza ubaguzi huu tutaangamia kama taifa watu hawaujui ukatoliki lakini ndo wanaeleza uongozi wa katoliki watu hawa wamefilisika sera badala ya kuongelea masuala kama ufisadi,umaskini,wizi tunajadili watu kama slaa na matukio kama alikuwa padre n.k let us be successful people and not average
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…