Elections 2010 Je, Dr. Willibrod Slaa atatufaa?

Elections 2010 Je, Dr. Willibrod Slaa atatufaa?

Unaweza usichambe kabisa ukabaki na gundu vile vile, ndicho ninachokataa.

Kumwambia Dr. Slaa asijibu hakutamsaidia maana maji kashayavulia nguo, hana budi kuyaoga, ama sivyo ataonekana mtu wa ku half step, na ahadi yake ya kujibu maswala yoyote atakuwa kaivunja, kitu ambacho si kizuri hususan mapema hivi kwa mgombea urais.

Nimeuliza mengi zaidi ya lugha na sijapata majibu, soma post.

Haifagiliwi groupthink hapa, wembe ule ule unaochana uzembe wa CCM utatumika kwa upinzani.Mwendo wa zero tolerance ndio mwendo pekee utakaolinyanyua taifa letu, mimi sina chama wala ushabiki, natafuta excellence kutoka kote.

no group thinking and haitakaa itokee... fuatilia mada utaona where i stand, lakini lazima uambiwe ukweli, kuchamba kwingi kutoka na m@vi

excellence in vigezo vingi na si english au lugha, and that's where we differ

narudia tena... kuchamba kwingi kutoka na ------

That is you bro

Acidic
 
Dr. Slaa kura yangu unayo tayari kwa sababu unaweza zaidi ya waliopo!
 
Hilo la Dkt. Slaa kutojua Kiingereza umelitoa wapi? Au kwa vile kaandika "the onus of proove' wewe kwako ndio imekuwa hajui Kiingereza?

Certainly no Kibunango, not even Makamba.

But still anakwambia "Onus of proove" akimaanisha "onus of proof", minor thing some say, but not very presidential.

And he is trying to project a presidential image here. We have to be critical because one of our problems is that we are not critical enough.

On the other hand, being balanced as always, I take his coming here as a real positive in that he can deal with his online constituents directly. Unlike other candidates.
 
Nataraji si hulka wala mazowea ya Dr. Slaa kuandika bila ya paragraph na kanuni nyengine sahihi za uandishi.

manake kwa Rais mtarajiwa kuandika kwa namna kama hii inatisha.

:confused2:
 
Dr unaandika bila hata ya paragraph watu watashindwa kusoma.

Halafu "the onus of proove' ndiyo kitu gani mkuu? Kama Kiingereza mambo fulani tuandike Kiswahili tu tutaelewana, hii mikogo ya Kiingereza cha kuunga unga inakuaibisha tu.

Kiswahili cha first person na third person kinachanganywa humo humo wakati mtu (Dr.) anajiongelea mwenyewe !

Na inakuwaje CHADEMA mkawaachia CCM kuchukua majimbo 10 bila kupingwa, mengine wagombea hawarudishi fomu, mengine wanarudisha fomu lakini wagombea dhaifu kama kina Regia Mtema, hivi mkipeleka wabunge dhaifu kama hawa mnatuambia nini kuhusu uimara wa chama?

Zaidi ya hapo, je ukweli kwamba hamna wagombea madhubuti unachangia CHADEMA kuchukua mapandikizi ya watu walioshindwa kupata nafasi kugombea ubunge kwa tiketi za CCM ?

Para inajumuisha sentensi zaidi ya moja na inabeba sehemu ya ujumbe au ujumbe. Para inapanuliwa mfano kwa kutoa mifano au ku-list kama alivyo fanya Dr. Hivyo Dr. ana para moja tu. Pia ukiangalia ameweka periods sehemu ambayo msomaji upumzika kwa muda wa kutosha kabla ya kuendelea. Kwa kawaida kama unasoma para na unakutana na neno ambalo haulifahamu basi unatumia context au unakimbilia kwenye dictionary!
 
Certainly no Kibunango, not even Makamba.

Hahahaa...Kibs where you at?

But still anakwambia "Onus of proove" akimaanisha "onus of proof", minor thing some say, but not very presidential.

I think you are "misunderestimating" him...

And he is trying to project a presidential image here. We have to be critical because one of our problems is that we are not critical enough.

Fair enough...

On the other hand, being balanced as always, I take his coming here as a real positive in that he can deal with his online constituents directly. Unlike other candidates.

True...true
 
Nataraji si hulka wala mazowea ya Dr. Slaa kuandika bila ya paragraph na kanuni nyengine sahihi za uandishi.

manake kwa Rais mtarajiwa kuandika kwa namna kama hii inatisha.

:confused2:

Hivyo ndivyo ambavyo huandika. Nenda kwenye profile yake halafu bofya pale panaposema 'find all posts' uone mabandiko yake ya huko nyuma
 
Groupthink ni pamoja na kukubali kufikiri kwamba kuna watu wako above criticism, kwa mkumbo wa JF. Habari za kuchamba - ashakum si matusi- nilishakujibu hapo juu, huja address counter yangu.

excellence in vigezo vingi na si english au lugha, and that's where we differ
1. Nimeongea zaidi ya maswala ya lugha, na nilishakuambia hili katika post ya juu, nikakushauri usome hiyo post uone nilichoongea zaidi ya lugha, sasa naona hujasoma, na huna kipya unarudia rudia. Rudi kusoma post.

2. Lugha nayo ina excellency, na lugha inaweza kuonyesha mambo mengine.Kwa mfano umakini. Dr. Slaa hajajionyesha kwamba ni makini katika kuandika, na hii si katika kiingereza tu, nimeonyesha hata alivyokanganya kiswahili.Kwa hiyo ukisema Kiingereza au Kiswahili kachanganya mambo, hili linaweza kuleta swali katika umakini wake.

Mchagua sana nazi hupata koroma, anayeogopa kuchagua kabisa kwa kuhofia kupata koroma hapati hata koroma, hapati nazi kabisa

Acha watu wachambue na kuchagua.!

That is you bro
Acidic
I am cut from a different cloth, what? You don't like it ?
 
Hivyo ndivyo ambavyo huandika. Nenda kwenye profile yake halafu bofya pale panaposema 'find all posts' uone mabandiko yake ya huko nyuma

Not a good look, let alone a presidential look.

About "Onus of proove", there is no misunderstanding that, you can't misunderstand something that is wrong, you can only misunderstand something that is right. Dr. kachemsha na atakuwa muungwana kama akija hapa na kukubali hilo tuliache tuongelee mengine.

By the way maswali yangu sijajibiwa, contrary to ahadi yake.

I hope he will not pull a Regia Mtema on us, and value the input enough to work on it.
 
Hivyo ndivyo ambavyo huandika. Nenda kwenye profile yake halafu bofya pale panaposema 'find all posts' uone mabandiko yake ya huko nyuma

Duh! kwa bahat mbaya ni kweli japo kuwa kwenye posts nyengine angalau kuna matumizi ya herufi kubwa baada ya full stop.

Uandishi wake wa leo unaweza kukataa kuwa ni mtu aliyemaliza chuo kikuu achilia mbali mtu anaegombea nafasi ya uraisi.
 
https://www.jamiiforums.com/members/dr-w-slaa.html
Nadhani ni mazoea tu....

icon1.gif
Re: Dr. Slaa Akamatwe, ahojiwe na ikiwezekana achukuliwe hatua
Invisible,
Japo ni muda mrefu sasa tangu ulipouliza swali lako kama "Pendekezo (la kukamatwa kwa Dr. Slaa na kuhojiwa) hili limetekelezwa, kwa ajili ya kuweka kumbukumbu sahihi naomba kutangaza kuwa Dr. Slaa hajakamatwa wala hajahojiwa hadi leo japo angelitamani sana kukamatwa na kuhojiwa ili baadhi ya majibu ya maswali mengi ya Ufisadi yaweze kupatikana. Hata hivyo, napenda kuarifu jamvi hili kuwa :-
Katika Civil Case no 140 ya mwaka 2008 iliyofunguliwa na Yusuf Manji (Plaintiff) dhidi ya Dr.Willibrod Slaa (Defendant) katika mahakama Kuu Kanda ya Dar-Es-Salaam na kusikilizwa na Jaji Shaidi, Dr. Slaa alishitakiwa na Bwana Yusuf Manji(Plaintiff) kwa kumchafulia jina (Defamation). Bwana Yusuf Manji alitetetewa na Wakili Msomi Muganyizi na Dr. Slaa(Defendant) alitetewa na Wakili Msomi, Bwana Tundu Lissu. Kesi ilihusu kimsingi Tamko la Dr. Slaa lilinukuliwa katika magazeti kadhaa kuwa " Bwana Yusuf Manji hawezi kuwa "Nguzo ya Uchumi wa Tanzania" kwa kuwa anatuhuma nyingi za "ufisadi" ( japo hakuwepo kwenye list of Shame) na kuwa hawezi kuwa "organizer wa Economic Forum na facilitator katika Economic Forum iliyokuwa inaandaliwa na Gazeti mmoja la Uingereza, The Economist mwezi Oktoba/November, 2007. Kkauli/Tamko hilo la Dr. Slaa lilinukuliwa na magazeti ya "Kulikoni"na "This Day". Hata hivyo baada ya Tamko hilo la Dr Slaa, Organizers wa Forum hiyo kwa "protest" hiyo walimwondoa Bwana Yusuf Manji kuwa Facilitator na Organizer wa Forum hiyo. Forum iliendelea. Baada ya hatua hiyo ya kuondolewa Bwana Manji akaona amechafuliwa jina lake na ya Biashara yake, na pia kwa hatua hiyo ya kuchafuliwa amepoteza Biashara yake. Katika hatua ya kuanza kusikilizwa kesi hiyo, Wakili Msomi Tundu Lissu akaweka PO (Preliminary Objection) na kesi hiyo ikafia katika hatua ya PO. Katika rulling yake Judge Shaidi, alitoa uamuzi kwa maneno yafuatayo: " Under the circumstances of this Case I hold that the plaint as drafted does not fully disclose cause of action against the defendant, I therefore reject it undr Order Vll of the Civil Procedure Code, Imetolewa 14/012010. ( Mimi nimeipata Nakala mwezi June). Hivyo nadhani kwa kumbukumbu ya Jamvi ni vizuri, kuwa siyo tu pendekezo halikutekelezwa, lakini jitihada "linalokaribiana" na hilo kwa njia ya Mahakama nalo pia limegonga ukuta, japo mhusika alichukua njia ya Kesi ya Madai. Ninachoweza kusema tu ni kuwa Watanzania i) Wawe Majasiri katika kutetea nchi yetu, hasa Watanzania Wasomi, na wako wengi sana katika Jamvi hili. Kulalamika tu hakutoshi, tuchukue hatua stahiki, ikiwa ni pamoja na kupiga kelele. Kumbe inasaidia sana. ii) Kupiga kelele kwetu kusiwe kwa misingi ya Ushabiki, wala itikadi, bali kweli itokane na ukweli, chuki ya kweli dhidi ya ufisadi, uwizi wa mali na Rasilimali za Taifa letu na au ubadhirifu wa mali ya umma ambao wengi katika Jamvi tunaonyesha wazi kuwa tunauchukia. Haitoshi kuonyesha kuwa tunauchukia bila hatua madhubuti nje ya Jamvi. iii) Hata mahakama zetu, pale ambapo hoja za msingi zinajengwa, na kwa mambo yanayohusu jamii kwa ujumla wake inasimama upande wa haki hasa ( High Court) kama ilivyoonyesha katika maamuzi yake mbalimbali, mathalan Mgombea Binafsi.
Nadhani taarifa hii kwa wana Jamvi inaweza kusaidia kuwajengea ukakamavu zaidi, ujasiri zaidi, uzalendo zaidi ( mimi naamini "Zaidi" hii inamaslahi makubwa kwa Taifa letu kuliko "Zaidi ya JK" ambayo sijui kama hata Yeye Mwenyewe anaweza kueleza ni Zaidi ya nini. Thanks​

Para inajumuisha sentensi zaidi ya moja na inabeba sehemu ya ujumbe au ujumbe. Para inapanuliwa mfano kwa kutoa mifano au ku-list kama alivyo fanya Dr. Hivyo Dr. ana para moja tu. Pia ukiangalia ameweka periods sehemu ambayo msomaji upumzika kwa muda wa kutosha kabla ya kuendelea. Kwa kawaida kama unasoma para na unakutana na neno ambalo haulifahamu basi unatumia context au unakimbilia kwenye dictionary!

Usitake nianze kuchambua vitu blow by blow, the mixing of the first and third person (in Swahili) no capitalization on starting sentences, etc.

Usitake kumtetea katika hili, utamuaibisha zaidi.
 
Duh! kwa bahat mbaya ni kweli japo kuwa kwenye posts nyengine angalau kuna matumizi ya herufi kubwa baada ya full stop.

Uandishi wake wa leo unaweza kukataa kuwa ni mtu aliyemaliza chuo kikuu achilia mbali mtu anaegombea nafasi ya uraisi.

Unajua labda wakati anasoma hakukuwa na Microsoft Office applications kwa hiyo mambo ya single na double spacing yatakuwa magumu kidogo....
 
Hapa jamvini tunaandika kwa minajili ya kuuhabarisha umma, sasa ktk hali kama hii inachukiza sana akina Tamika binti Dilunga na trupu lake kuanza kubitch kingereza au sijui punctuation, inakera sana na kubore sometimes. Sisemi kwamba watu waandike hovyohovyo, lakini lets be real, hatupo shuleni hapa, it does n't mean everything goes lakini kuna some comfrot level kwamba ujumbe unafika ..thats most important. Tunapoondoka kwenye hoja na kuanza kuangalia punctuation tuna-sink kwene level za akina Malaria Sugu na akina Tamika.

Ni maoni tu.
 
Dr unaandika bila hata ya paragraph watu watashindwa kusoma.

Halafu "the onus of proove' ndiyo kitu gani mkuu? Kama Kiingereza mambo fulani tuandike Kiswahili tu tutaelewana, hii mikogo ya Kiingereza cha kuunga unga inakuaibisha tu.

Kiswahili cha first person na third person kinachanganywa humo humo wakati mtu (Dr.) anajiongelea mwenyewe !

Na inakuwaje CHADEMA mkawaachia CCM kuchukua majimbo 10 bila kupingwa, mengine wagombea hawarudishi fomu, mengine wanarudisha fomu lakini wagombea dhaifu kama kina Regia Mtema, hivi mkipeleka wabunge dhaifu kama hawa mnatuambia nini kuhusu uimara wa chama?

Zaidi ya hapo, je ukweli kwamba hamna wagombea madhubuti unachangia CHADEMA kuchukua mapandikizi ya watu walioshindwa kupata nafasi kugombea ubunge kwa tiketi za CCM ?

Nafarijika kwamba walau Dr. Slaa anajibu hoja zenu, lakini kama hoja zenu zinahamia kwenye lugha yake na majimbo mengine kuachiwa CCM kunachosha sana. Waulizeni na wagombea wengine nao wajibu maswali yenu. Ila kitu ambacho kinanishangaza ni jinsi mtoa mada anavyojaribu kuelezea kitu ambacho hama ufahamu nacho na anajaribu kupotosha watu.
 
Hapa jamvini tunaandika kwa minajili ya kuuhabarisha umma, sasa ktk hali kama hii inachukiza sana akina Tamika binti Dilunga na trupu lake kuanza kubitch kingereza au sijui punctuation, inakera sana na kubore sometimes. Sisemi kwamba watu waandike hovyohovyo, lakini lets be real, hatupo shuleni hapa, it does n't mean everything goes lakini kuna some comfrot level kwamba ujumbe unafika ..thats most important. Tunapoondoka kwenye hoja na kuanza kuangalia punctuation tuna-sink kwene level za akina Malaria Sugu na akina Tamika.

Ni maoni tu.

Kiingereza na punctuation ni muhimu, kinaweza kutuonyesha mtu anavyofikiri na umakini wake.

Nimeuliza mengi zaidi ya Kiingereza, na sijajibiwa.

Hapa kama mtu unakuja kama "Brazameni" unatuletea picha za clubs, huwezi kunisikia nakushikia bango kuhusu punctuation na Kiingereza sijui, hujajipresent hivyo.

Ukija kama Dr. W. Slaa, mgombea urais, lazima tupandishe bar.

We unataka rais ambaye hajui kuandika ? Pengine Dr. Slaa atashinda urais na kwenda Ikulu huku akikumbuka maneno yetu na kubadili hili.

Hapa tunatoa constructive criticism, isije mbele kutokea Dr. Slaa anataka kuandika kitu formal ikawa aibu.
 
HAPANA.

Kuandika 'vizuri' hakuna mafungamano na fikra au umakini. Kuna maprofesa wanachemka hata wanapoandikia kwenye fields zao itakuwa huyu mwanasiasa Slaa? Na hii sio article ya specialization kwenye gazeti au kitabu, ni post tu ya kwenye forum tu..Sisemi kwamba aandike hovyohovyo kwa kusudi la, ila lazima tuangalie bigger picture hapa, ambayo ni kuangalia hoja iliyopo mezani.

Walau tumshukuru Slaa kwa kuja humu kuonesha anachangamana na wanamijadala na walau anajua kutumia kompyuta na internet. Wengine huko hata kuumba hati ni 'wito'.
 
Nafarijika kwamba walau Dr. Slaa anajibu hoja zenu, lakini kama hoja zenu zinahamia kwenye lugha yake na majimbo mengine kuachiwa CCM kunachosha sana. Waulizeni na wagombea wengine nao wajibu maswali yenu. Ila kitu ambacho kinanishangaza ni jinsi mtoa mada anavyojaribu kuelezea kitu ambacho hama ufahamu nacho na anajaribu kupotosha watu.

Husaidii chochote kwa kutotoa detail, sanasana unaweza kuwafanya watu wakuone mpambe unayetetea bila data.

Kuna maswali yameulizwa hayajajibiwa, kama una majibu unaweza kujibu.

Dr. Slaa mwenyewe kakaribisha maswali yote tu, ingawa naona anagwaya kujibu.

Ameandika

Nawashukuru wana jamvi wote, na wanajamvi mko huru kudodosa lolote kwa vile kiongozi hana private life,

hivyo Dr Slaa anaweza kuulizwa lolote na ufafanuzi unaotakiwa utatolewa
 
Back
Top Bottom