Elections 2010 Je, Dr. Willibrod Slaa atatufaa?

Elections 2010 Je, Dr. Willibrod Slaa atatufaa?

1. Hana mbinu wala mikakati ya kushinda
2. Anaonekana ana kaugonjwa ka ulevi na anataka kuwaambukiza watanzania wote ugonjwa huo
3. Hajui uchumi unakwendaje (labla kwa vile ni mtheolojia)
4. Hauziki
5. Anaishi kihuni (hana ndoa)
6. Jema pekee alilofanya (ingawa hajafanikiwa na hatafanikiwa) ni kuwataja wevi pale mwembe yanga
7. Mnafiki. Analialia eti posho za wabunge ni kuwa huku anazipokea
8. Hodari wa kulalamika lalamika
9. Anataka kuzalisha jamii yta wavuta sigara (huende na bangi pia) pamoja na walevi
10. Hakubaliki

Kwa hali hiyo, SITAMCHAGUA
Duuh hii kali sana.bwana Slaa ni kama samaki mdogo ndani ya bahari.sera yake ni EPA tu.kazi ya Professor Lipumba kaaiba na kuifanya yake.
 
Hatuna haja na mtu anayetaka watz wote tuwe walevi. Kama anataka pombe iwe divai kanisani kwake apeleke special request serikalini awe exempted kwenye kodi!

Tatizo letu wanachadema tukiguswa pabaya tunaanza kudiscuss watu badala ya hoja!

Dokta Slaa ameonyesha weledi wa hali ya juu kudisplay sifa hizi kwa muda mfupi sana

Hoja ya antibayotiki ingekuwa valid kama asingezingatia kutoa maelezo zaidi kwenye sababu/point namba 1, 7, 8.

Nawaogopa sana wale wanaowaweka ant Slaa kuwa ni wasaliti. Binafsi I am not either Pro Slaa nor Pro Kikwete. Hawawote hawawezi. Nitacast my vote atakaposimama mgombea binafsi. Vyama vyote vya siasa, and especially vya upinzani ni hopeless.

Duuh hii kali sana.bwana Slaa ni kama samaki mdogo ndani ya bahari.sera yake ni EPA tu.kazi ya Professor Lipumba kaaiba na kuifanya yake.

Pumba
 
Nataraji si hulka wala mazowea ya Dr. Slaa kuandika bila ya paragraph na kanuni nyengine sahihi za uandishi.

manake kwa Rais mtarajiwa kuandika kwa namna kama hii inatisha.

:confused2:

nani ambaye yuko kwenye campaign anaweza kuja kukujibu hapa, dr slaa anajitahidi sana ukizingatia anatumia mkono mmoja kwenye keyboard.
hana mda wa kukaa na kuanza kuedit kitu cha JF yupo very busy sasa hivi
fikirieni kidogo majuku aliyokuwa nayo na mkono wake mmoja
 
Du kweli ujinga wetu faida yao,we padri umeona epa tuu yote slaa aliyofanya hujayaona ?tunasubiri tuone mgonjwa wenu akifika moshi atatumie ambulance gani maana zote za pale zimenunuliwa na ndes pesa(ndesamburo-chadema)sasa kama hafanyi kampeni bila ambulance ngoja tuone moshi
 
1. Hana mbinu wala mikakati ya kushinda
2. Anaonekana ana kaugonjwa ka ulevi na anataka kuwaambukiza watanzania wote ugonjwa huo
3. Hajui uchumi unakwendaje (labla kwa vile ni mtheolojia)
4. Hauziki
5. Anaishi kihuni (hana ndoa)
6. Jema pekee alilofanya (ingawa hajafanikiwa na hatafanikiwa) ni kuwataja wevi pale mwembe yanga
7. Mnafiki. Analialia eti posho za wabunge ni kuwa huku anazipokea
8. Hodari wa kulalamika lalamika
9. Anataka kuzalisha jamii yta wavuta sigara (huende na bangi pia) pamoja na walevi
10. Hakubaliki

Kwa hali hiyo, SITAMCHAGUA

Another chick with no head crossing the road!
 
nani ambaye yuko kwenye campaign anaweza kuja kukujibu hapa, dr slaa anajitahidi sana ukizingatia anatumia mkono mmoja kwenye keyboard.
hana mda wa kukaa na kuanza kuedit kitu cha JF yupo very busy sasa hivi
fikirieni kidogo majuku aliyokuwa nayo na mkono wake mmoja

tunamshukuru kwa juhudi zake za kufika hapa kuja kujibu maswala ya wananchi na pia kutoa fursa zaidi ya kuendelea kuulizwa masuala hayo.

Tungemshukuru zaidi kama angetumia dakika chache zaidi kutuletea ujumbe ambao ni rahisi kusomeka na kueleweka.

Naamini kuandika herufi kubwa na ndogo kwenye sentensi kwa kutumia mkono mmoja (nilidhani amekwisha poa though) ni kazi ngumu kidogo hasa ukiwa busy na masuala mengine muhimu, lakini kubofya enter/return sidhani kama ingelimchukulia muda wa ziada au kumuwia vigumu kufanya kwa kutumia mkono mmoja.

kikawaida Dk Slaa huwa hatumii paragraph, japo kuwa kanuni nyengine za kiuandishi huwa anazitumia, tungelimuomba atusaidie wasomaji kwa kutuwekea paragraph ili ujumbe wake aliouandika katika wakati huo finyu alionao, ueleweke kirahisi.
 
Du kweli jamaa hatufai.pia Dr.amekiri mwenyewe kuwa mgombea mwenza ni darasa la saba(elimu ya kujua kusoma na kuandika).Je huyu atamudu kuwa Makamu wa RAIS?!
 
Wengi wamekuwa wanajiuliza kuwa Dk. Wilbroad Slaa ni nani? Na anataka au anaweza kuifanyia nini Tanzania. Wanajiuliza kama ni nani na ni nini kinachomsukuma Dk. SLAA kutaka apewe mamlaka ya kuiongoza Tanzania.

Dk. SLAA ni Mtanzania, muumini na Daktari wa Falsafa katika masuala ya dini yake ya Ukristo dhehebu la Katoliki. Alikuwa Kasisi au bado ni Kasisi kwa maana ya Sakramenti isiyofutika, lakini aliasi wakati akiwa Katibu wa Baraza la Maaskofu, nafasi kubwa sana katika kanisa hilo lenye waumini wengi.

Haifahamiki kama alikorofisha nini, ingawa kuna madai kwamba alifanya ufisadi kwenye fedha za kanisa. Inafahamika kwamba alipoondoka kwenye uongozi wa kanisa alioa kama ishara ya kusema sasa ukasisi basi, lakini kanisa lilikataa kubariki ndoa yake kwa maana ile ile kwamba sakramenti hizo hazitolewi mara mbili kwa mtu mmoja.

Asingeweza kupata Sakramenti ya Ndoa baada ya kupata Sakramenti ya Ukasisi. Hakujali akaendelea na shughuli zake na sasa anatarajia kuwa Kasisi wa kwanza kuwa Rais wa Tanzania kama kura zitatosha ifikapo Octoba 31, mwaka huu.

Katika kitabu anachokitumia Dk. SLAA kwa sala, ambacho ni Biblia, yapo maelezo katika Timotheo sura ya tatu mstari wa kwanza hadi wa tano (Tim.3:1-5) kwamba: "Ni neno la kuaminiwa mtu akitaka kazi ya uaskofu; atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha, si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole, si mtu wa kujadiliana wala asiwe mwenye kupenda fedha; mwenye kusimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu, yaani mtu asiyejua kuisimimia nyumba yake mwenyewe, atalisimamiaje kanisa la Mungu".

Mchanganuo wa aya hiyo hapo juu unatoa picha tofauti za namna ya kumwelewa Dk. SLAA kama mtu anayetafuta nafasi ya kuwa Rais wa Tanzania. Kwa upande mmoja, hata kama zipo sababu nyingine zilizomwondoa katika nafasi ya Ukatibu wa Baraza la Maaskofu, kuhusishwa kwake na ufisadi wa fedha za misaada kulimwondolea sifa ya kuwa kiongozi kanisa la Mungu, Analaumika.

Naamini hajajitoa kwenye Ukristo bado ni Mkatoliki na zipo taarifa ambazo zimeshaandikwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kwamba kanisa linamuunga mkono katika harakati zake za kutaka uongozi wa juu wa nchi.

Kanisa limeshakanusha kwamba halimuungi mkono kwa sababu Tanzania haina dini na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamekuwa wakisisitiza kwamba Chama chao kisihusishwe na dini kwa maelezo kwamba uongozi wake ni wa watu wa dini zote na hata pengine wale wasio na dini.

Pamoja na ukweli kwamba viongozi waanzilishi wa CHADEMA ni wakristo, kanisa halingeweza kuonyesha kwamba linamuunga mkono, lakini ni vyema ikakubalika kwamba kwa miaka yote kanisa limekuwa likiamini kwamba dini ya mfalme wako ndio dini yako.

Hata kama Dk. SLAA aliukataa Ukasisi na akaonekana muovu mbele ya macho ya uongozi wa kanisa, lakini kwa sasa anaonekana ni mali kwa kuwa jiwe lililokataliwa na wajenzi wote, sasa limekuwa jiwe la msingi wa nyumba. Ukorofi wa Dk. SLAA kwa kanisa wa kuivuruga Sakramenti ya Ukasisi utavumiliwa na haitashangaza kama hata ndoa yake ikabarikiwa na kanisa endapo atafanikiwa kuupata Urais.

Ushahidi wa hali kama hiyo upo. PASTEUR BIZIMUNGU, hakuwa na ndoa na SERAFIN hadi alipoteuliwa kuwa Rais wa Rwanda wakati RPF inaingia madarakani mwaka 1994. Kanisa ndilo lililomtaka afunge ndoa kabla ya kuapishwa kuwa Rais. Kanisa linachotaka ni Dk. SLAA kuwa Rais wa Tanzania. Waraka wa kanisa uliotolewa na Baraza la Maaskofu tarehe 2 Julai, 2010, ulikuwa ni ishara tosha ya kuwajulisha Wakristo kwa ujumla kwamba wana mtu wao na bila shaka ni Dk. SLAA.

Kasisi/Padre anayejiondoa kwenye huduma zake za Kipadre huchukuliwa na kanisa kama mwana mpotevu (Prodigal Son) au kondoo aliyepotea, ambaye wakati wowote anaweza kurudi kundini. Kwa kuwa kazi mojawapo ya kanisa ni kuwatafuta na kuwarudisha kundini kondoo waliopotea, kanisa halijakata tamaa kuhusu uwezekano wa Dk. SLAA kurudia wito wake wa upadre.

Kwa kuzingatia dhamira yake kama mpakwa mafuta (the anointed) si jambo la ajabu ikiwa Dk. SLAA atarudi kwenye utume wake kama padre na kuiacha nchi "solemba". Hata asiporudia upadre wake, upo uwezekano wa mchungaji huyo, akisukumwa na sauti ya wito wake wa upadre kuiongoza nchi kwa maslahi ya kanisa ambalo limemlea na kuchora moyoni mwake alama ya upadre isiyofutika (indelible mark) kama Kanisa Katoliki linavyoamini.

Wapo baadhi ya Watanzania watakaokumbuka kwamba mara baada ya uhuru wa Zimbabwe kupatikana mwaka 1980, Waziri Mkuu ROBERT MUGABE hakukubaliana na pendekezo la Rais CANAAN BANANA kwamba nchi hiyo iwe ya kikristo. Hakuna uhakika kama hilo haliwezi kutokea Tanzania ikiwa Dk. SLAA atafanikiwa kuwa Rais.

Taarifa ambazo ni vigumu kuzithibitisha na ambazo si vyema kuzipuuza zinaonyesha kwamba baadhi ya maaskofu wamekuwa wakikutana na uongozi wa Chadema kujadili hoja ya uongozi wa kitaifa na suala la uras mwaka 2015. Maoni ni kwamba hata kama urais hautapatikana mwaka 2010, angalau washinde na kuhakikisha kwamba Chadema kinakuwa chama kikuu cha upinzani bungeni ili kutoa nafasi ya kujiandaa kwa urais mwaka 2015.

Taarifa hizo zinaonyesha kwamba ili kufanikisha dhana ya CHADEMA kuwa chama kikuu cha upinzani Bungeni ni vyema MBOWE arudi jimboni kugombea na DK. SLAA agombee Urais hata kama hatafanikiwa, lakini atakuwa kivutio kikubwa cha kuwashawishi wananchi kuchagua Wabunge wengi wa chama hicho.

Mikakati ya kanisa imekuwa haimshirikishi ZITTO KABWE kwa sababu yeye anahofiwa kwamba ama yupo karibu na CCM au anatumia elimu yake kujijenga ili agombee Urais mwaka 2015.

Dk. SLAA alisita sana kuchukua fomu za chama chake kukubali kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na yamkini watu walio wengi walikuwa wanamuuliza ni kwa nini anafanya hivyo, lakini wajuzi wa mambo walitambua kwamba Dk. SLAA alikuwa anasita kwa sababu nyingi ikiwa ni pamoja na kuamini kwamba alishafikishwa mahali pabaya ambapo pande zote mbili na kila upande ukiwa na dhamira yake ulikuwa unataka kumtumia. MBOWE alitaka kumtumia kukijenga Chama na Kanisa kujiimarisha.

Kwa upande mwingine, Dk. SLAA alipokuwa anajiunga na CHADEMA baada ya kuenguliwa CCM alifanya hivyo kwa kuamini kwamba angejijengea wasifu mpya, lakini hakujua kwamba anaingia kwenye Chama cha kifamilia kinachoendeshwa kwa gwanda la kikabila na kuongozwa na MBOWE ambaye naye anatajwa kuwa si msafi sana.

DK. SLAA amekuwa msitari wa mbele kupiga vita ufisadi hususan ndani ya serikali. Katika vita hivyo, Dk. SLAA amekuwa akisema kwamba serikali ya CCM haiwezi kupiga vita rushwa kwa sababau yenyewe imekuwa ikiendesha ufisadi tangu ilipoingia madarakani enzi za TANU. Kwa hoja hii, Dk. SLAA anaonyesha kwamba sio mkweli labda lengo lake ni kuichafua CCM ili ashinde katika uchaguzi huu.
Lakini hata kama hiyo ndiyo dhamira yake, atakuwa anafanya makosa makubwa akijaribu kupuuza juhudi za serikali ya awamu ya nne chini ya Rais KIKWETE katika kupambana na rushwa na ufisadi. Ni mapema mno Dk. SLAA kusahau juhudi za Muasisi wa Taifa hili Mwalimu JULIUS KAMBARAGE NYERERE na Waziri Mkuu MORINGE SOKOINE katika mapambano yao dhidi ya rushwa na wahujumu uchumi.

Kuna wasiwasi kwamba Dk. SLAA amegombea Urais kupitia kwenye chama ambacho hana madaraka na uwezo wa kukemea maovu ya ndani. Hana maelezo ya wazi kwamba ni kwa nini alikubaliana na ukaidi wa MBOWE alipon'gan'gania kwamba ni yeye pekee asimame kama mgombea wa Uenyekiti wa chama hicho na kumlazimisha ZITTO KABWE aondoe jina lake.

Matumizi ya ovyo ya fedha za CHADEMA ni ugonjwa ambao Dk. SLAA ameshindwa kuupatia dawa ingawa anafahamu kwamba ndio uliosababisha kuleta hali ya kutoelewana kati ya MBOWE na aliyekuwa mbunge wa Tarime CHACHA WANGWE ( sasa marehemu).

Ameshindwa kuyavunja makundi mawili ndani ya CHADEMA; kundi moja likiongozwa na Naibu Katibu Mkuu ZITTO KABWE na kundi lingine likiongozwa na Mwenyekiti FREEMAN MBOWE. Makundi yote haya mawili yanaelezewa kwamba kila moja linataka Urais mwaka 2015. Moja ya athari inayotokana na mivutano ya makundi haya ni kushindikana mara tatu kuteua Wabunge wa viti maalum. Hali hiyo ilitokea baada ya wagombea wanaomuunga mkono FREEMAN MBOWE kushindwa isipokuwa mmoja tu ambaye ni mtoto wa PHILEMON NDESAMBURO aliyekuwa Mbunge wa Moshi mjini.

Wote wanaoomunga mkono ZITTO walishinda na hali hiyo ilikuwa inaonekana kuwa tishio kwa Mwenyekiti Mbowe, ambaye alitamka kwamba mkutano huo ni batili. Haifahamiki kama wabunge wa viti maalumu wa CHADEMA watateuliwa lini, lakini swali la msingi na lisilo na jibu ni kwamba kwa nini DK. SLAA amekaa kimya kwenye kadhia hii. DK. SLAA anawashawishi Watanzania waanze kuamini kwamba hata wakimpa mdaraka ya kuiongoza dola ya Tanzania, atakuwa na tabia ya kuuzia masuala ya kitaifa kwa sababu hajiamini. Watanzania wanatakiwa kufikiri sana kabla ya kufanya maamuzi.

Source: Gazeti la Raia mwema Agosti 25 – Agosti 31, 2010
Mgombea mwenza ana wasifa gani? nasikia ni std 7, ya shule gani? Dr Slaa akiwa Rais akawa hayupo nchini, Huyo ndiye atakayekaimu nafasi ya Rais.mmmmm sijui ZINDUKA.
 
Naomba kuhukumiwa kwa kusema ukweli.

Dr. Slaa ni Mpinzani Mzuri sana, Dr. Slaa ni Auditor Mzuri... lakini on his own sio Kiongozi mzuri... Zitto kuna wakati alitoa sifa moja kubwa na JK ambayo Dr. Slaa hanayo... nayo ni tolerance... kuwa na subira... ukiongoza nchi na kukurupuka... my friend....

Lingine muhimu sana kwa Dr. Slaa na Wapinzani wengi ni madikteta... na hapa ndipo wanatofautiana sana na JK... JK needs people to be free to air-out their views...

Well simfagilii JK, bale naweka tu mambo kama ninavyoyaona.

Otherwise nakuunga mkono na sera zako (za CHADEMA) kuondoa ofisi ya mkuu wa mkoa... ila wakati unaeleza usiongelee watu sana, maana du Rais mtarajiwa, mafisadi, mafisadii, je wakiisha.... please ongelea taasisi zaidi.
 
1. Hana mbinu wala mikakati ya kushinda
2. Anaonekana ana kaugonjwa ka ulevi na anataka kuwaambukiza watanzania wote ugonjwa huo
3. Hajui uchumi unakwendaje (labla kwa vile ni mtheolojia)
4. Hauziki
5. Anaishi kihuni (hana ndoa)
6. Jema pekee alilofanya (ingawa hajafanikiwa na hatafanikiwa) ni kuwataja wevi pale mwembe yanga
7. Mnafiki. Analialia eti posho za wabunge ni kuwa huku anazipokea
8. Hodari wa kulalamika lalamika
9. Anataka kuzalisha jamii yta wavuta sigara (huende na bangi pia) pamoja na walevi
10. Hakubaliki

Kwa hali hiyo, SITAMCHAGUA

Kamwambie aliyekutuma kuwa Wadanganyika wote siyo wajinga!!!!!
 
1. Uvumilivu gani wa Kikwete wakati amewaadhibu wale wote waliokuwa kwenye kambio dhidi yake wakati wa mchakato wa kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM mwaka 2005?

2.Kama udikteta unaozungumzia wa Dk.Slaa ni ule wa kutaka Zitto aondoe jina lake wakati akitakka uenyekiti wa kiTaifa, nadhani unachanganya kati ya udikteta na uwezo wa kufanya maamuzi magumu hata kama ni kmatwakwa ya wengi, kwa huu ni uongozi!

Naomba kuhukumiwa kwa kusema ukweli.

Dr. Slaa ni Mpinzani Mzuri sana, Dr. Slaa ni Auditor Mzuri... lakini on his own sio Kiongozi mzuri... Zitto kuna wakati alitoa sifa moja kubwa na JK ambayo Dr. Slaa hanayo... nayo ni tolerance... kuwa na subira... ukiongoza nchi na kukurupuka... my friend....

Lingine muhimu sana kwa Dr. Slaa na Wapinzani wengi ni madikteta... na hapa ndipo wanatofautiana sana na JK... JK needs people to be free to air-out their views...

Well simfagilii JK, bale naweka tu mambo kama ninavyoyaona.

Otherwise nakuunga mkono na sera zako (za CHADEMA) kuondoa ofisi ya mkuu wa mkoa... ila wakati unaeleza usiongelee watu sana, maana du Rais mtarajiwa, mafisadi, mafisadii, je wakiisha.... please ongelea taasisi zaidi.
 
tunamshukuru kwa juhudi zake za kufika hapa kuja kujibu maswala ya wananchi na pia kutoa fursa zaidi ya kuendelea kuulizwa masuala hayo.

Tungemshukuru zaidi kama angetumia dakika chache zaidi kutuletea ujumbe ambao ni rahisi kusomeka na kueleweka.

Naamini kuandika herufi kubwa na ndogo kwenye sentensi kwa kutumia mkono mmoja (nilidhani amekwisha poa though) ni kazi ngumu kidogo hasa ukiwa busy na masuala mengine muhimu, lakini kubofya enter/return sidhani kama ingelimchukulia muda wa ziada au kumuwia vigumu kufanya kwa kutumia mkono mmoja.

kikawaida Dk Slaa huwa hatumii paragraph, japo kuwa kanuni nyengine za kiuandishi huwa anazitumia, tungelimuomba atusaidie wasomaji kwa kutuwekea paragraph ili ujumbe wake aliouandika katika wakati huo finyu alionao, ueleweke kirahisi.

ungetaka isiwe na makosa ingebidi slaa aipeleke kwa mtu wa kuiedit, kwanza imenishangaza sana slaa kupata mda wa kusoma hii na kujibu, sasa wewe unataka iwe edited
marais huwa wanaongea na watu wengine ndio wanaandika na kedit, unadhani kikwete anaandika habari.......

slaa endelea hivyo hivyo wanaotaka kuelewa wataelewa wasiotaka wamuulize kiongozi mwingine wasubirie majibu miaka mitano hijayo
 
Naomba kuhukumiwa kwa kusema ukweli.

Dr. Slaa ni Mpinzani Mzuri sana, Dr. Slaa ni Auditor Mzuri... lakini on his own sio Kiongozi mzuri... Zitto kuna wakati alitoa sifa moja kubwa na JK ambayo Dr. Slaa hanayo... nayo ni tolerance... kuwa na subira... ukiongoza nchi na kukurupuka... my friend....

Lingine muhimu sana kwa Dr. Slaa na Wapinzani wengi ni madikteta... na hapa ndipo wanatofautiana sana na JK... JK needs people to be free to air-out their views...

Well simfagilii JK, bale naweka tu mambo kama ninavyoyaona.

Otherwise nakuunga mkono na sera zako (za CHADEMA) kuondoa ofisi ya mkuu wa mkoa... ila wakati unaeleza usiongelee watu sana, maana du Rais mtarajiwa, mafisadi, mafisadii, je wakiisha.... please ongelea taasisi zaidi.

Kama JK ameweza kuwa rais na waTZ tunalizika naye, then nakuhakikishia kuwa mTZ yeyeto mwenye akili timamu anawe kuongoza nchi. yetu. Ninikueleza hivyo kwa kujua kuwa JK siyo kiongozi period!!!
 
Nataraji si hulka wala mazowea ya Dr. Slaa kuandika bila ya paragraph na kanuni nyengine sahihi za uandishi.

manake kwa Rais mtarajiwa kuandika kwa namna kama hii inatisha.

:confused2:
katumia mobile. pia ana haraka zake na hana muda wa kutosha kujibu hoja. pia uelewe kuwa kawaheshimu sana wanajamvi hadi kufikia hatua ya kujibu hoja. kwa hilo inabidi umpe tano
 
Huyu dr slaa hafai hata bure.....dr slaa ni bora raisi sio rais bora na waswahili wanasema rais huwa ghali

Yesterday 11:41 PM #35 Malembeka Shija

Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
Join DateWed Aug 2010
Posts16
Thanks : 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power0

Kibaraka mwingine huyu hapa!!
 
Unaweza usichambe kabisa ukabaki na gundu vile vile, ndicho ninachokataa.

Kumwambia Dr. Slaa asijibu hakutamsaidia maana maji kashayavulia nguo, hana budi kuyaoga, ama sivyo ataonekana mtu wa ku half step, na ahadi yake ya kujibu maswala yoyote atakuwa kaivunja, kitu ambacho si kizuri hususan mapema hivi kwa mgombea urais.

Nimeuliza mengi zaidi ya lugha na sijapata majibu, soma post.

Haifagiliwi groupthink hapa, wembe ule ule unaochana uzembe wa CCM utatumika kwa upinzani.Mwendo wa zero tolerance ndio mwendo pekee utakaolinyanyua taifa letu, mimi sina chama wala ushabiki, natafuta excellence kutoka kote.

Kimyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom