Je, Elimu ya Juu ni 'DEAD HORSE' kwa Vijana wa Tanzania

Je, Elimu ya Juu ni 'DEAD HORSE' kwa Vijana wa Tanzania

its MalekoGJ

New Member
Joined
Aug 27, 2020
Posts
3
Reaction score
5
Je, Elimu ya Juu ni 'DEAD HORSE' kwa Vijana wa Tanzania
Katika ulimwengu wa sasa, ambapo vijana wengi wa Kitanzania wanahangaika kupata ajira licha ya kuwa na shahada za vyuo vikuu, pendekezo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa la kuwahimiza wahitimu kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi kupitia VETA linaibua maswali mengi.

Je, hatua hii ni suluhisho la muda mfupi au ni dalili ya tatizo kubwa zaidi katika mfumo wetu wa elimu na ajira?

Nadharia ya 'DEAD HORSE' na Elimu ya Juu

Nadharia ya 'Dead Horse' Hutumikq kuelezea hali ambapo mtu/watu au taasisi wanaendelea kuwekeza katika mikakati isiyofanya kazi, badala ya kutafuta mbinu mbadala.

Katika muktadha huu, tunaweza kujiuliza: Je, mfumo wetu wa elimu ya juu umekuwa 'Dead Horse' ambao tunaendelea kuubebesha mizigo ya matumaini ya ajira kwa vijana wetu?

Je, Shahada Bado Ina Thamani?

Ikiwa shahada hazitoi ujuzi unaohitajika kwenye soko la ajira, tunapaswa kujiuliza kuhusu thamani yake.
Je, tunawapa vijana wetu matumaini ya uongo kwamba elimu ya juu ni tiketi ya uhakika ya mafanikio? Au tunahitaji kurekebisha mfumo wetu wa elimu ili kuhakikisha kuwa wahitimu wanakuwa na ujuzi unaohitajika?

Mafunzo ya Ufundi Suluhisho au Kukwepa Tatizo?

Kuwahimiza wahitimu wa vyuo vikuu kujiunga na mafunzo ya ufundi kunaweza kuonekana kama suluhisho la haraka. Lakini je, hii ni njia ya kukwepa kushughulikia matatizo ya kimuundo katika soko la ajira na mfumo wa elimu?

Je, tunahitaji kuangalia upya sera zetu za ajira na elimu ili kuhakikisha kuwa zinakidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye?

Ujumbe kwa VijanaTumaini au Kukata Tamaa?

Pendekezo hilo alilolitoa Waziri Mkuu limepeleka ujumbe gani kwa vijana wetu? Je, linawapa matumaini mapya au linawakatisha tamaa kuhusu thamani ya elimu ya juu? Tunapaswa kuwa makini tusije tukawafanya vijana wetu wahisi kwamba jitihada zao za kupata shahada hazina maana.

Badala ya kutafuta suluhisho la haraka, tunahitaji mjadala wa kina kuhusu mustakabali wa elimu na ajira nchini Tanzania. Tunapaswa kuangalia jinsi ya kuboresha mfumo wetu wa elimu ili kuhakikisha kuwa unatoa ujuzi unaohitajika, na pia kuunda mazingira ya kiuchumi yanayowezesha ajira kwa wahitimu wetu.

Toa Maoni Yako

Je, unakubaliana na pendekezo la Waziri Mkuu? Unadhani ni suluhisho sahihi au tunahitaji kuchukua hatua nyingine? Toa maoni yako hapa chini na tushiriki katika mjadala huu muhimu.
 
Haya mambo yameelezwa siku nyingi, na watu wengi.

Hayajaanza leo.

Nyerere aliandika mpaka vitabu kuelezea umuhimu wa elimu ya ufundi.

Aung Sang Suu Kyi kashaeleza jambo hili Myanmar.

Elimu ya juu na elimu ya ufundi ni vitu viwili vinavyo complement each other, vyote vinahitajiana.

Msome Aung Sang Suu Kyi alivyoelezea suala hili.

"Daw Aung San Suu Kyi urged youth to “open their eyes and ears for more opportunities” and to develop the capacity to handle many other jobs.” The State Counsellor promoted vocational education, telling the public in Kalay that university education and vocational training are equally important, and that her government is doing its best to reduce unemployment."
 
Maisha yapo katika hesabu

Kwakuwa wao ndo decision makers (wafanya maamuzi) nategemea atoe suluhisho ambalo litakuwa realistic na sio Kama aanavyofanya sasa hivi.

Binafsi nachojua hata vijana wakisoma VETA bado tatizo la Ajira haliwezi kuwa solved

Kwakuwa sisi hatupo na wala hatujajiandaa kuikomboa nchi

ccm ni chama kilichoshindwa kuisaidia nchi

Ahsante
 
Je, Elimu ya Juu ni 'DEAD HORSE' kwa Vijana wa Tanzania
Katika ulimwengu wa sasa, ambapo vijana wengi wa Kitanzania wanahangaika kupata ajira licha ya kuwa na shahada za vyuo vikuu, pendekezo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa la kuwahimiza wahitimu kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi kupitia VETA linaibua maswali mengi.
Ni kwa watoto wa walala hoi, chawa wana uhakika wa ajira
 
Hymaya mambo yameelezwa siku nyingi, na watu wengi.

Hayajaanza leo.

Nyerere akiandika mpaka vitabu kuelezea umuhinu wa elimu ya ufundi.

Aung Sang Suu Kyi kashaeleza jambo hiki Myanmar.

Elimu ya juu na elimu ya ufundi ni vitu viwiki vinavyo complement each other, vyote vinahitajiana.

Msome Aung Sang Suu Kyi alivyoelezea suala hili.

"Daw Aung San Suu Kyi urged youth to “open their eyes and ears for more opportunities” and to develop the capacity to handle many other jobs.” The State Counsellor promoted vocational education, telling the public in Kalay that university education and vocational training are equally important, and that her government is doing its best to reduce unemployment."

Haya mambo nimeyasoma darasa la 03 zaidi ya miaka 40 iliyopita

Sera za ujamaa
Elimu ya kujitegemea

Ila Taifa la watu wajinga wanasubiri mpaka itokee eruption ndo waongee

Nyerere kashindwa
Mkapa
Kikwete
Magufuli
Na sasa Mama

Watu waliokosa weledi na mikakati imara wanajiropekea
 
Hata hiyo elimu ya Ufundi wanayoisema serikali imeshindwa kuiendeleza.
 
Maisha yapo katika hesabu

Kwakuwa wao ndo decision makers (wafanya maamuzi) nategemea atoe suluhisho ambalo litakuwa realistic na sio Kama aanavyofanya sasa hivi.

Binafsi nachojua hata vijana wakisoma VETA bado tatizo la Ajira haliwezi kuwa solved

Kwakuwa sisi hatupo na wala hatujajiandaa kuikomboa nchi

ccm ni chama kilichoshindwa kuisaidia nchi

Ahsante
Tunaongozwa na watu washamba sana.
 
Haya mambo yameelezwa siku nyingi, na watu wengi.

Hayajaanza leo.

Nyerere aliandika mpaka vitabu kuelezea umuhimu wa elimu ya ufundi.

Aung Sang Suu Kyi kashaeleza jambo hili Myanmar.

Elimu ya juu na elimu ya ufundi ni vitu viwili vinavyo complement each other, vyote vinahitajiana.

Msome Aung Sang Suu Kyi alivyoelezea suala hili.

"Daw Aung San Suu Kyi urged youth to “open their eyes and ears for more opportunities” and to develop the capacity to handle many other jobs.” The State Counsellor promoted vocational education, telling the public in Kalay that university education and vocational training are equally important, and that her government is doing its best to reduce unemployment."
Huku bariadi sasa hivi kuna vijana wadomi wanajifunza tiba za jadi kuna mwamko mkubwa

Hii tuiiteje mkuu ?VETA au
 
Mfano wa mzazi bora

FB_IMG_17418755995588632.jpg
 
Technical Schools Ziwe Active Sanaa na Pia ziongezwe!
 
Bora elimu ya VETA Ni elimu ya nadharia na vitendo pia ni ya muda mfupi

Una degree huna kazi kutwa kutuma cv nakutembea kutafuta kazi na kazi zenyewe hakuna kuna faida gani?

Nashauri serikali iongezee nguvu kwenye vyuo vya ufundi ikiwezekana vyuo vyote vikuu nchini viwe vya VETA.
 
Dunia inaenda Kasi sana lakini bahati mbaya viongozi wetu bado wanaishi kwenye ulimwengu wa miaka ya 80s.

Kila kiongozi point yake ni "vijana mjiajiri" huku yeye ana zaidi ya miaka 40+ kwenye ajira.

Tunakoelekea kama hakutakuwa na mabadiliko,elimu ya chuo kikuu haitakuwa na thamani tena.
 
Back
Top Bottom