Mcqueenen
JF-Expert Member
- Nov 2, 2019
- 6,843
- 11,702
Mwaka 1859 mwanabaiolojia Charles Darwin alichapisha kitabu chake kuhusu chanzo cha viumbe wote duniani chenye jina “On the origin of species” Kilichoelezea theory yake ya evolution. Darwin alisema kwamba hivi viumbe vyote tunavyoviona leo (Aina Zaidi ya million 8.6) vikizagaa kwenye uso wa dunia havikuwa hivyo milele tangu mwanzo, lakini vilitokana na mabadiliko ya muda mrefu yanayoitwa evolution.
Evolution ni mchakato ambao aina mbalimbali za viumbe husitawi kutoka maumbo ya awali (viumbe vya awali) wakati wa historia ya dunia.
Darwin alielezea kwa ndani jinsi viumbe vinabadilika kulingana na sababu mbalimbali na akaelezea mechanism inayosababisha viumbe kubadilika na kutengeneza viumbe wapya (specie formation)
Mechanism kuu ni mbili ambayo ni Natural selection/Uteuzi wa asili na Variation/Tofauti katika viumbe.
i. Variation: Viumbe havifanani, kutokana na randomness/unasibu wa uzazi (Watoto hawafanani 100% na wazazi) na pia kuna mutation (Mabadiliko katika gene za viumbe) husababisha viumbe wa aina moja wasifanane. Mfano unaweza kufuga kuku wekundu tu bandani lakini baada ya vizazi kadhaa unaweza kuona kuku wanazaliwa wenye rangi tofauti.
ii. Natural selection/Uteuzi wa asili : Mazingira husababisha viumbe wenye sifa nzuri kuishi na wale wenye sifa mbaya hupotea. Hivyo katika mfano hapo juu, ikitokea waganga wanapenda kuku wekundu basi wale kuku wekundu watapotea lakini wale wengine wenye rangi tofauti wataishi….Hivyo baada ya muda mrefu itaweza kutokea kuku wa aina tofauti na wale wa mwanzo na kuleta aina nyingine ya kuku...Hii process ikiendelea kwa muda mrefu inaweza kutokea aina ya viumbe kama kuku lakini wametofautiana sana na kuku mpaka wanashindwa kuzaliana na kuku wa kawaida (Hivyo kiumbe kipya kinakuwa kimepatikana)
Lakini leo ni May Mwaka 2022 AD (Takriban miaka 163 baadae) Bado watu wanabishana kama hii concept ya Evolution ya Darwin ni ukweli (Fact) au ni nadharia tu (Theory).
Kwenye huu uzi nataka nielezee kama hii evolution ni fact au ni theory tu, na nitajaribu kujibu baadhi ya maswali yanayowasha vichwa vya watu wengi kuhusu evolution, hivyo twende Pamoja.
Ikumbukwe kipindi Darwin anachapisha kitabu chake Nyanja mbalimbali za kisayansi kama Genetics, embryology, Anatomy zilikuwa hazijatanuka na kuwa kama leo. Hata fossils zilikuwa hazijagunduliwa kwa wingi kama leo, Hivyo Darwin alipingwa na watu wengi sana kwakuwa kipindi hicho watu wengi waliamini Dunia iliumbwa kwa mara moja miaka isiyozidi 6000 nyuma. Kwakuwa leo Nyanja hizo zimetanuka na tunajua mengi Zaidi basi tuyapitie hayo mengi kwa kifupi.
i. Anatomy;
Viumbe wengi wanafanana maumbile kuashiria kuwa wana chimbuko moja. Mfano Mifupa ya mikono na miguu ya paka inafanana na mifupa ya binadamu nk. Nk.Viumbe vingi kwenye kundi moja hufanana sana maumbo, Hivyo viumbe vingi huonesha kuwa vilitokana na wazazi walewale/Chimbuko moja.
ii. Genetics.;
Mendel (Mwaka 1865) aligundua kuwa viumbe vinarithishana sifa kwa njia ya kuzaa kupitia vinasaba (DNA). Kwa kutumia sayansi ya kisasa kuziangalia hizi DNA wanasayansi wamegundua kuwa Hivi vinasaba vya viumbe mbalimbali vinafanana. Viumbe wa kundi moja (mfano mamalia) huwa na vinasaba vinavyofanana sana kuliko wale wa makundi tofauti. Hivyo huonesha viumbe vina chimbuko moja.
iii. Fossils
Mabaki ya viumbe wa zamani yamekuwa yakipatikana chini ya dunia. Mabaki mengi yameonesha kuwa hapo kale kulikuwa na viumbe ambavyo leo havipo tena duniani na mabaki hayo pia yameonesha kwa kiwango kikubwa jinsi viumbe vya leo vina chimbuko moja. Mfano ugunduzi wa Alesi pale Kenya umeonesha kuwa Alesi alikuwa ni kiumbe mwenye sifa za binadamu na nyani, hivyo alikuwa ni babu yetu sisi binadamu na nyani.
iv. Embryology
Hapa tunaangalia viumbe vikiwa ndani ya tumbo/Yai kabla havijazaliwa..Viumbe vingi katika ngazi za mwanzoni huwa vinafanana, mfano mimba ya mwezi mmoja ya binadamu, kile kijusi kinafanana na kijusi cha nyani,mbwa,papa,Ng’ombe nk. Ni katika ngazi za mbele za ukuaji ndipo vijusi huanza kutofautiana Hivyo inaonesha kuwa viumbe vyote vina chimbuko moja.
NB: Evolution imaonesha kuwa viumbe vyote duniani vina chimbuko moja, Yule kiumbe wa kwanza alitokanaje hilo ni swali na mada nyingine ambayo ni ya siku nyingine.
While Evolution haisapoti lakini pia haipingi uwepo wa Mungu (Unaweza kuamini kuwa Mungu aliumba kiumbe wa Kwanza ambaye aliendelea kuevolve na kuleta viumbe wote duniani)