Je, Evolution ni Ukweli au Nadharia tu?

Je, Evolution ni Ukweli au Nadharia tu?

Aisee! Na wewe umekaririshwa? Nitajie dating method yoyote unayoijua ambayo inaweza pima kitu kilichokaa milions of years!
Umeanza standard lies of evolutionists. Hakuna evidence ya hizo milions of Years!
You seem to reject facts even if you see them just because it contradicts your previous knowledge. Fossils and rocks have been dated go google you'll see the methods.

What is important is to shape knowledge agree with fact because facts are facts they do not change simply because you know something else.
 
Futile assumption. You are trying to put language barrier that is not there! Where do you get this?
I use my sense too remember. In order to reconcile some facts with knowledge this makes sense. So no one lied but someone was out of vocabulary
 
Wewe umechanganyikiwa. Hujui mbele wala nyuma ni wapi.
Both evolution na creation za religious ni uongo mkubwa.

Kisayansi haiwezekani uumbaji wa watu wawili waje wazae races na rangi tofaut tofauti bila ya kuwa na muingiliano wa mbegu ya utofauti ili kuja kuleta kiumbe cha race/rangi ya tofauti na hawa waliopo.

Sijui kwanni ktk sayansi na dini watu huogopa kuhoji haya maswali.

Eti mtu wa mwanzo alikuwa nyani and then why not now hao nyani hawabadiriki?

Kama huyo eva na adam walikuwa wazungu je hawa races zingine za waafrika/indians, chinese, walitokea vipi? Hakuna muujiza wa mtu kuzaliwa na race tofaut na ya mzazi wake pasipokuwa na muunganiko wa races mbili tofaut ili kuleta huo uchotara.

Upuuzi mwingine ni kuforce tuamni races za watu weupe zilitokea baada ya watu weusi kwenda maeneo ya baridi na kupelekea ngozi zao kubadirika na kuwa weupe, je wale watumwa wa kiafrika waliochukuliwa mateka miaka400 iliyopita kwanini hawajabadirika mpka leo wapo vile vile weusi?

Sayansi na Dini hizi zote ni takataka na propaganda zilizotungwa na wahuni ili kufichwa ukweli wa asili ya maisha ya dunia na kweli hii huwezi ipata kwa kusoma hizo takataka za vitabu vya dini ama vitabu vya kisayansi vilivyobase kwenye nadharia za wahuni wa Propaganda za Evolution..
 
Hakuna maelezo namna gani unicellular animal ambao allegedly ndio our ancestors waligeuka kuwa multicellular. Na ilikuwaje tukawa male and female. Na kati ya figo, moyo na mapafu kipi kilitangulia ku evolve? Kama ni moyo huyo kiumbe aliishije bila mapafu? Kama mapafu aliishije bila moyo?

Halafu linkuja suala la missing missing links. Kama evolution ilikuwa inafanyika taratibu kuna wanyama wangekufa kabla ya kuwa evolved. Yaani tuseme reptilia wana evolve kuwea birds then kw namna ilivyo slow kuna reptilia wangekufa kabl hawajawa ndege so repti-bird.

Sitaki kwenda kwenye deep scientific problems za evolution kwa sababu wengi hawataelewa na itakuwa ni waste of time.

No one have ever observed evolution. It happened in the mind of evolutionists like Darwin and is still happening in some minds today!
Okay nimeona kuna maswali ma5 hapo. nayo ni
1. Emergence of multicellular organisms
2. Emergence of sex
3. Irreducible complexity of a biological system
4. Missing links in evolution
5. Observation of evolution
Nitajibu yote:::
Tuanze na la kwanza

1. Unicellular organisms waligeukaje kuwa multicellular??
Cell ziliungana ili kuadapt mazingira kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo..Kwaajili ya kukwepa kuliwa na parasites, kwajili ya kuongeza utaalam wa utendaji au kuruhusu utambuzi mkubwa zaidi wa stimulus za mazingira. Multicellularity iliibuka kutokana na mwingiliano kati ya cells mbalimbali katika kikundi, kitu kilichopelekea shinikizo la specialization.

Cell zinatafuta resources kwa kutumia chemotaxis, cell zikiungana huwa zinaongeza efficiency ya chemotaxis hence inaonesha kwanini unicellular zilikuja kuwa multicellular.
ingawa zipo tradeoffs za kuwa katika kikundi, kama vile kugawana rasilimali zinazopatikana lakini yapo kuna manufaa: Mfano katika kikundi, seli zinaweza kugawanya kazi kati yao ili kuwa na ufanisi zaidi, na inaweza kuunda mbinu za kisasa za kujilinda kila mmoja dhidi ya madhara.
Sasa nini kilisababisha seli za kwanza kujiunga kuwa kundi na kuwa multicellular?

Njia moja ya kujibu swali hili ni kufuatilia tabia ya ukungu wa moulds. Viumbe hivi vipo kama seli moja (Unicellular) lakini hujiunga na kuunda makoloni(multicellular) wakati rasilimali katika mazingira yao zinapopungua. Watafiti wameona kuwa makoloni ya ukungu wa molds (slime moulds) yanaweza kuzungukia (Navigation) mazingira yao bora zaidi kuliko seli moja ikiwa peke yake. Sifa hii inapendekeza kwamba manufaa ya kusonga pamoja kama kikundi yanaweza kuwa sababu inayoendesha seli moja kuunda vikundi na kuwa multicellular.

2. Emergence of sex
Sex ilianza kama isogamy baadae ndio zikaspecify na kuwa male na female kwa baadhi ya viumbe along evolution.

Tunajua sex zilikuja takriban miaka bilion 2 iliyopita. Ikiwa ni kama njia ya kushare DNA information na kuongeza variation kwa offsprings. Hizi variation ndiyo nzuri maana zinaongeza chance ya specie kusurvive..Mfano Kama binadamu wote tungefanana basi ikitokea ugonjwa kama corona ukaua mmoja basi unaweza kuua population ya binadamu wote,,lakini kwakuwa tunatofautiana ndiyo ile imeongeza chance ya kusurvive kwakuwa Corona itaua baadhi na baadhi haitawadhuru.

Viumbe wa kwanza kuwa sexual (wafanya ngono) walikuwa isogamous - (ambayo ni sawa na kuwa mashoga, isipokuwa kila kiumbe kipo mahali fulani katikati ya mwanamume na mwanamke.)

Mpaka leo Viumbe wengi, ikiwa ni pamoja na fungi, algae and single-celled pond-swimmers bado wanareproduce kwa isogamy. Kwa kufanya hivyo, wanatupa dalili kwa nini? na ni jinsi gani jinsia zilivyotokea.

Ili kuelewa maisha kabla ya ujio wa wanaume na wanawake, unahitaji ujue role ya kila mmoja: Wanaume hutoa seli ndogo ya ngono (manii au poleni) kuliko wenzao wa kike ambao hutoa yai kubwa.

Lakini kwa hawa viumbe Isogamous, kwa upande mwingine, bado wanafanya ngono lakini badala ya kuchanganya manii na mayai wao wanachanganya seli za ngono zenye takriban ukubwa sawa - zinazojulikana kama gametes.

Viumbe vingine hupanua chaguzi zao za ngono kwa kuwa na jinsia nyingi—Uyoga huwa na jinsia hadi 30,000 na uyoga unaweza kuoana na uyoga wowote isipokuwa ule wenye jinsia sawa.

Hata hivyo baada ya Isogamy, cell zikaanza kuspecialize na hivyo idadi ya jinsia ikabidi zipungue.

Jinsia mbili ni nzuri maana hizi gametes zinagawana majukumu, shahawa haibebi mitochondria ila yai ndiyo linabeba mitochondria, hivyo vikiungana mitochondria zote zinatoka kwa mama..Hii ni nzuri maana kwenye isogamy, baba na mama wote wana mitochondria sawa hivyo inaweza kusababisha hizi mitochondria kuzaana kwa wingi kwa watoto na kuongeza expence kwenye cell.
 
Na kati ya figo, moyo na mapafu kipi kilitangulia ku evolve? Kama ni moyo huyo kiumbe aliishije bila mapafu? Kama mapafu aliishije bila moyo?

Halafu linkuja suala la missing missing links. Kama evolution ilikuwa inafanyika taratibu kuna wanyama wangekufa kabla ya kuwa evolved. Yaani tuseme reptilia wana evolve kuwea birds then kw namna ilivyo slow kuna reptilia wangekufa kabl hawajawa ndege so repti-bird.

Sitaki kwenda kwenye deep scientific problems za evolution kwa sababu wengi hawataelewa na itakuwa ni waste of time.

No one have ever observed evolution. It happened in the mind of evolutionists like Darwin and is still happening in some minds today!
Okay nimeona kuna maswali ma5 hapo. nayo ni
1. Emergence of multicellular organisms
2. Emergence of sex
3. Irreducible complexity of a biological system
4. Missing links in evolution
5. Observation of evolution
Nitajibu yote:::
Tuendelee la 3

3. Irreducible complex argument inasema viumbe vingi ni irreducibly complex, Maana yake ni kwamba mfano ukitoa moyo kwa binadamu, mwili wote unakufa,kwahiyo haiwezekani vikaevolve step by step. However unatakiwa ujue kuwa sio miaka yote viungo vilikuwa complex hivi..Mfano Dar tunaweza kusema ni jamii iliyokomaa Na irreducibly complex, mfano ukitoa System za usafirishaji (Barabara,bandari,airport) mji unakufa maana watu watakosa mpaka vyakula..Ukitoa huduma za afya pia mji utakufa kwa milipuko ya magonjwa etc,Ukitoa Polisi tu mji unakufa na watu wataukimbia maana uhalifu utakithiri..Lakini haimaanishi Dar ilianza ikiwa na polisi,bandari,airport na mabarabara yote....Vijiji vingi vinaanza vikiwa simple tu baadaye vinaanza kuwa complex and matured..Hivohivo hata kwenye evolution, Hizi organs kama moyo,mapafu na figo zilianza primitive na kuadvance into complexity.
Argument yako ya irreducible complex inaanguka maana kila organ inaweza kuwa reduced into a primitive form.
Cell ilianza kwa kuwa na mdomo,tumbo,figo na moyo lakini zikiwa very primitive.
Kwenye cell kuna cellwall ambayo inafanya kazi kama ngozi, mdomo wa kuingiza vyakula,oxygen na nutrients mbalimbali (Endocytosis) na kutoa uchafu kwenye cell (exocytosis) pia oxygen huingia ndani ya cell na Co2 hutoka nje ya cell kupitia cellwall (Hivo pia cellwall ni kama mapafu)..Kwahyo cellwall tayari inafanya kazi ya ngozi,mdomo,mapafu na anus. Ndani ya cell kuna cytoplasm ambayo inafanya kazi ya kusafirisha nutrients na chakula ndani ya cell (Kama moyo na damu unavyosafirisha) lakini pia cell inachambua na kukusanya uchafu ili utoke kwa exocytosis (Kama figo),
Kwahyo evolution inapoendelea na multicellular organisms zilipokuja,,, cell ziligawana majukumu, Baadhi zikaanza kujikita kwenye intake of molecules, zingine distribution (Kama blood vessels) na zingine kucontrol kila kitu (Brain)
Kupitia ushahidi wa comparative genome na fossil records tumeona kuwa kuna viumbe vilikuwa na organ kama moyo lakini bado haujawa advance kama huu tulio nao..mfano wa kiumbe huyo ni yule aliyekuwa kama mnyoo majini aliyemzaa samaki (anaitwa pikaia) Hawa pikaia walikuwa na sifa za chordates na ndiyo walikuwa babu zao na samaki ambao ni babu zao na mijusi ambao ni babu zao na panya ambao ni babu zao na nyani.
Mfano hata leo tuna viumbe kama minyoo ambavyo havina moyo ulioadvance kama wetu lakini vinapump damu mwilini kwa organ ambayo ni kama moyo ulio primitive (Aortcic arch)..Hivyo, hata Huu moyo wa binadamu ulianza kama specialization ya baadhi ya cell kutengeneza kama cappilaries/blood vessels na kuanza kupump damu mwilini ,,baadae ukaendelea ukawa kama msuli wenye chamber tofauti tofauti kwaajili ya kuongeza efficiency.
Kipindi moyo ulikuwa primitive, hata tumbo,mapafu na figo vilikuwa primitive pia...Kama vile kijiji kikiwa primitive ambapo maji ni visima na umeme ni vibatari,, hiki kijiji hata vitu vingine vitakuwa primitive (mfano elimu, miundombinu, afya nk.) Lakini kikianza kukua na kuwa mji...Vitu vyote vitaadvance mpaka huwezi kuuliza Hizi barabara za lami zilijengwa lini kama hakukuwa na umeme kijijini??
 
Halafu linkuja suala la missing missing links. Kama evolution ilikuwa inafanyika taratibu kuna wanyama wangekufa kabla ya kuwa evolved. Yaani tuseme reptilia wana evolve kuwea birds then kw namna ilivyo slow kuna reptilia wangekufa kabl hawajawa ndege so repti-bird.

No one have ever observed evolution. It happened in the mind of evolutionists like Darwin and is still happening in some minds today!
4. Missing links in evolution.
Movie ya evolution ni kubwa kiasi kwamba kila mwaka paleontologists wanazidi kugundua mafuvu na fossils kibao zinazosaidia kutengeneza picha kamili ya puzzle ili kuielewa movie nzima ya evolution.
Missing link zipo nyingi lakini sio kigezo cha kuikataa theory nzima kwasababu link zilizogunduliwa tayari ni nyingi sana na zinaendelea kugunduliwa.
(Yani ni sawa na uokote fuvu la binadamu likiwa pamoja na mbavu zake na mifupa ya mikono na miguu, halafu mtu akuambie huyu alikuwa binadamu wewe ukatae kwakuwa bado hatujapata mifupa ya hips na vidole)

Kuhusu swali lako la transition mfano repti-birds, Kwanza unatakiwa ujue kuwa Hawa ndege ni Dinasours.
Kipindi dinasours wapo duniani, walikumbwa na majanga mengi ikiwemo kupigwa na kimondo na climate change iliyosababisha ukosefu wa vyakula duniani na kusababisha Dinasours wengi kupotea kwenye uso wa dunia..Baadhi ya dinasours waliosurvive mpaka leo ni wale waliokuwa wadogo kiumbo (Hawakuitaji chakula kingi) na wakawa na mabawa yaliyowasaidia kutafuta chakula kwa urahisi ambao leo Tunawaita ndege.

Kwahiyo technically speaking, Hawa ndege ni reptiles.

5. Observing evolution.
Evolution imekuwa observed mara nyingi sana.
Mfano proffesor Richard Lenski aliamua aangalie evolution ya E.coli Bacteria kwa kuwaangalia jinsi wanavyomultiply kwenye solution yenye glucose across vizazi 59,000.

Baada ya vizazi 59000 amegundua kuwa hawa bacteria wa sasa wana ukubwa mara mbili zaidi ya wale wa kwanza na pia wana uwezo mkubwa zaidi wa kutumia glucose kuliko babu zao.

Tena alienda mbali na kuwa anawatofautisha hawa bacteria mpaka akatengeneza specie mpya ya bacteria ambayo ilijitokeza kwenye kizazi cha 20,000 ambapo bacteria hawa wana uwezo wa kudigest citric acid (Kama ile ya kwenye limao)

Ukichukua babu zao bacteria unakuta hawawezi kuidigest citric acid lakini kupitia random mutation, hawa bacteria wamekuwa na huo uwezo. Na hata DNA sequence ya hao bacteria ilitofautiana.

Mifano ya hivi ipo mingi mno na mingine ni ile unatembea nayo wewe mwilini, Mfano misuli ya sikioni, mimi hapa nina uwezo wa kutingisha masikio, kitu ambacho hakinisaidii vyovyote lakini ndugu zetu mamalia kama mbwa,paka wanatumia misuli hiyo kugeuza masikio kufuata source ya sauti.
 
Attachments

  • Dinasours.jpg
    Dinasours.jpg
    8.1 KB · Views: 12
  • wx.jpg
    wx.jpg
    8 KB · Views: 11
  • index.jpg
    index.jpg
    12.2 KB · Views: 12
4. Missing links in evolution.
Movie ya evolution ni kubwa kiasi kwamba kila mwaka paleontologists wanazidi kugundua mafuvu na fossils kibao zinazosaidia kutengeneza picha kamili ya puzzle ili kuielewa movie nzima ya evolution.
Where are those fossils? Kila matamahuluku yaliyogunduliwa ni mnyama kamili wa aina fulani. Yaani wakikuta ndege basi ni ndege. Na hiyo siyo evolution!

Missing link zipo nyingi lakini sio kigezo cha kuikataa theory nzima kwasababu link zilizogunduliwa tayari ni nyingi sana na zinaendelea kugunduliwa.
Please leta data za hizo missing links. Maana ndio nitakuwa nasikia kwako, na nitashukuru kuzipata. Toka kwa reliable source!

(Yani ni sawa na uokote fuvu la binadamu likiwa pamoja na mbavu zake na mifupa ya mikono na miguu, halafu mtu akuambie huyu alikuwa binadamu wewe ukatae kwakuwa bado hatujapata mifupa ya hips na vidole)
Hapa umepiga stori. Nasubiri data sasa!

Kuhusu swali lako la transition mfano repti-birds, Kwanza unatakiwa ujue kuwa Hawa ndege ni Dinasours.
Kipindi dinasours wapo duniani, walikumbwa na majanga mengi ikiwemo kupigwa na kimondo na climate change iliyosababisha ukosefu wa vyakula duniani na kusababisha Dinasours wengi kupotea kwenye uso wa dunia..Baadhi ya dinasours waliosurvive mpaka leo ni wale waliokuwa wadogo kiumbo (Hawakuitaji chakula kingi) na wakawa na mabawa yaliyowasaidia kutafuta chakula kwa urahisi ambao leo Tunawaita ndege.
Hii na hadithi ya binti chura zina tofauti gani? Hakuna aliyeshuhudia haya yakitokea, hakuna ushahidi. Yaani ni paukwa pakawa.
Kama unadhani sio hekaya basi leta ushahidi wa data!

Kwahiyo technically speaking, Hawa ndege ni reptiles.
Sio technically sema magically! Kama tu ile hadithi ya aliyombusu chura akawa binti mfalme enzi za mama na mwana!

5. Observing evolution.
Evolution imekuwa observed mara nyingi sana.
Mfano proffesor Richard Lenski aliamua aangalie evolution ya E.coli Bacteria kwa kuwaangalia jinsi wanavyomultiply kwenye solution yenye glucose across vizazi 59,000.

Baada ya vizazi 59000 amegundua kuwa hawa bacteria wa sasa wana ukubwa mara mbili zaidi ya wale wa kwanza na pia wana uwezo mkubwa zaidi wa kutumia glucose kuliko babu zao.

Tena alienda mbali na kuwa anawatofautisha hawa bacteria mpaka akatengeneza specie mpya ya bacteria ambayo ilijitokeza kwenye kizazi cha 20,000 ambapo bacteria hawa wana uwezo wa kudigest citric acid (Kama ile ya kwenye limao)

Ukichukua babu zao bacteria unakuta hawawezi kuidigest citric acid lakini kupitia random mutation, hawa bacteria wamekuwa na huo uwezo. Na hata DNA sequence ya hao bacteria ilitofautiana.
How is this evolution? Hawa bacteria wali evolve na kuwa nini? Maana bacteria wakiwa bacteria bado sio evolution.
Hii ni adaptation na iko inbuilt kwa kila kiumbe. Adaptation is not evolution. It is still the same kind of animal!
 
3. Irreducible complex argument inasema viumbe vingi ni irreducibly complex, Maana yake ni kwamba mfano ukitoa moyo kwa binadamu, mwili wote unakufa,kwahiyo haiwezekani vikaevolve step by step. However unatakiwa ujue kuwa sio miaka yote viungo vilikuwa complex hivi..
Vilikuwaje? Unaweza kueleza huyo "binadamu wa viungo simple" alikuwaje? Hivyo viungo rahisi vilikuwaje? Na utuletee data za chanzo chako cha hii habari.

Mfano Dar tunaweza kusema ni jamii iliyokomaa Na irreducibly complex, mfano ukitoa System za usafirishaji (Barabara,bandari,airport) mji unakufa maana watu watakosa mpaka vyakula..Ukitoa huduma za afya pia mji utakufa kwa milipuko ya magonjwa etc,Ukitoa Polisi tu mji unakufa na watu wataukimbia maana uhalifu utakithiri..Lakini haimaanishi Dar ilianza ikiwa na polisi,bandari,airport na mabarabara yote....Vijiji vingi vinaanza vikiwa simple tu baadaye vinaanza kuwa complex and matured..Hivohivo hata kwenye evolution, Hizi organs kama moyo,mapafu na figo zilianza primitive na kuadvance into complexity.
Huu mfano wako dhaifu sana, so nitauacha tu!
Moyo primitive ulikuwaje? Kati ya ventricle na auricle kipi kili evolve kwanza? Je moyo primitive ulikuwa na veins?
Mapafu primitive yalikuwaje? Kati ya mapafu na moyo kipi kilitangulia? Kama ni moyo, ulihitaji oksijeni? Uliipataje? Kama ni mapafu, yalihitaji damu? Ilifikaje kwenye mapafu?

Ukiisha kujibu, naomba chanzo/data

Argument yako ya irreducible complex inaanguka maana kila organ inaweza kuwa reduced into a primitive form.
Kwa aina ya argumentation from thin air kila argument inaanguka. Ila kitaalamu hamna kit kama primitive organ. Hazipo! Hazijawahi kuwepo!
Kama unakataa tupe mifano iliyokuwa observed!

Cell ilianza kwa kuwa na mdomo,tumbo,figo na moyo lakini zikiwa very primitive.
Hizo primitive organs zikoje? Halafu hizi stori chanzo chake ni wapi? Ni nani aliye observe hizi mambo za primitive organs? Maana hakuna any scientific record ya organ yoyote kuwa primitive.

Kuna tofauti gani kati ya maelezo yako na hadithi za Alfu lela ulela?

Kwenye cell kuna cellwall ambayo inafanya kazi kama ngozi, mdomo wa kuingiza vyakula,oxygen na nutrients mbalimbali (Endocytosis) na kutoa uchafu kwenye cell (exocytosis) pia oxygen huingia ndani ya cell na Co2 hutoka nje ya cell kupitia cellwall (Hivo pia cellwall ni kama mapafu)..Kwahyo cellwall tayari inafanya kazi ya ngozi,mdomo,mapafu na anus. Ndani ya cell kuna cytoplasm ambayo inafanya kazi ya kusafirisha nutrients na chakula ndani ya cell (Kama moyo na damu unavyosafirisha) lakini pia cell inachambua na kukusanya uchafu ili utoke kwa exocytosis (Kama figo),
Kwahyo evolution inapoendelea na multicellular organisms zilipokuja,,, cell ziligawana majukumu, Baadhi zikaanza kujikita kwenye intake of molecules, zingine distribution (Kama blood vessels) na zingine kucontrol kila kitu (Brain)
Kupitia ushahidi wa comparative genome na fossil records tumeona kuwa kuna viumbe vilikuwa na organ kama moyo lakini bado haujawa advance kama huu tulio nao..mfano wa kiumbe huyo ni yule aliyekuwa kama mnyoo majini aliyemzaa samaki (anaitwa pikaia) Hawa pikaia walikuwa na sifa za chordates na ndiyo walikuwa babu zao na samaki ambao ni babu zao na mijusi ambao ni babu zao na panya ambao ni babu zao na nyani.
Mfano hata leo tuna viumbe kama minyoo ambavyo havina moyo ulioadvance kama wetu lakini vinapump damu mwilini kwa organ ambayo ni kama moyo ulio primitive (Aortcic arch)..Hivyo, hata Huu moyo wa binadamu ulianza kama specialization ya baadhi ya cell kutengeneza kama cappilaries/blood vessels na kuanza kupump damu mwilini ,,baadae ukaendelea ukawa kama msuli wenye chamber tofauti tofauti kwaajili ya kuongeza efficiency.
Kipindi moyo ulikuwa primitive, hata tumbo,mapafu na figo vilikuwa primitive pia...Kama vile kijiji kikiwa primitive ambapo maji ni visima na umeme ni vibatari,, hiki kijiji hata vitu vingine vitakuwa primitive (mfano elimu, miundombinu, afya nk.) Lakini kikianza kukua na kuwa mji...Vitu vyote vitaadvance mpaka huwezi kuuliza Hizi barabara za lami zilijengwa lini kama hakukuwa na umeme kijijini??
Aisee, hii ni sayansi nayo? Inatokea wapi? Maana naona umepiga stori sana kuliko data na uhalisia. Umeongea abstracts kibao. Sijaona data ku support stori zako zote hizi.

Mpaka utakapoleta data, zitabakia kuwa hekaya, ngano na visasili!
 
Je unaturuhusu tutumie kanuni hizihizi katika hadithi ulizotuletea wewe mwanzo? Je wewe unao ushahidi wa watu na viumbe kuanza vikiwa vizima vizima. Umeona wapi likitokea.

Mbona kwa upande wetu sisi kila siku tunawaona watu wakianza kama seli samaki[wanaogelea bahari ya amniotic fluid], mijusi kisha ndio wanakuwa watu wasio na uwezo wa kuzaa baadaye kadri muda unavyoenda wanabalehe etc etc

Wewe una ushahidi gani kwamba wanatokeaga mijitu mizima mizima
 
Kwanza unakubali kuwa evolution ni soga, hekaya na visasili? Ni kama hadithi ya binti chura?

Anzia hapo kwanza, usitafute pa kujifichia. Kama sio hadithi basi leta data na ushahidi!
 
Kwanza unakubali kuwa evolution ni soga, hekaya na visasili? Ni kama hadithi ya binti chura?

Anzia hapo kwanza, usitafute pa kujifichia. Kama sio hadithi basi leta data na ushahidi!
Hapana aijakubali.

Braza hujauona huo ushahidi wangu wa kwamba nimeona seli ndogo zikibadilika kuwa samaki [kijusi kinaogelea bahari ya amniotic fluid inayokilisha na kukilinda kabla hakijatengeneza mifumo imara] kisha kanakuwa kamtu etc etc

Na wewe naomba ushahidi mmoja wa kitu tata kutokea hivyohivyo kikiwa kitata ndio tuendelee.
 
Sasa hiyo ni evolution?
Yaani kukua kwa samaki ndio evolution?
Kwa hiyo samaki ana evolve kutoka nini kwenda nini?

Hatua za ukuaji wea viumbe hai sio evolution ndio maana hata terminologies za kisayansi sio evolution bali ni growth, metamorphosis et al.

Ukitaka kutuhakikishia kuwa evolution ni kweli utuambie aliyeshuhudia ancestor wetu alikuwa unicellular ni nani au wapi kumewahi tokea unicellular organism ikabadilika kuwa multicellular organism.

Na wakati ukiandaa hilo jibu tusaidie pia genetical information za ku upgrade uni to multi ziliongezeka tokea wapi?
 
kutokea hivyohivyo kikiwa kitata ndio tuendelee.
Hujatoa ushahidi ambao ni acceptable kwa standard yoyote kuwa evolution happened na hutaki kukubali kuwa ni hekaya.

Ukiweza kutoa ushahidi wa kuwa evolution iliwahi kutokea popote then utakuwa na moral authority ya kuhoji supernatural Creation na majibu yapo.

Kwanza tumalize hili la dhahania dhaifu ya mageuko.
 
Sasa hiyo ni evolution?
Yaani kukua kwa samaki ndio evolution?
Kwa hiyo samaki ana evolve kutoka nini kwenda nini?

Hatua za ukuaji wea viumbe hai sio evolution ndio maana hata terminologies za kisayansi sio evolution bali ni growth, metamorphosis et al.

Ukitaka kutuhakikishia kuwa evolution ni kweli utuambie aliyeshuhudia ancestor wetu alikuwa unicellular ni nani au wapi kumewahi tokea unicellular organism ikabadilika kuwa multicellular organism.

Na wakati ukiandaa hilo jibu tusaidie pia genetical information za ku upgrade uni to multi ziliongezeka tokea wapi?
Ona sasa kumbe inaonesha wewe hutaki ushahidi wa evolution.

Bali unataka evolution ifanyike upya ili na wewe ushuhudie upige na picha!

Kila siku tunaona unicellular zygote inabadilika kuwa multicellular embryo bado unataka ushahidi gani.

Kuna swali uliuliza kuwa nini kilianza kati ya mapafu na moyo ukapewa majibu kwamba wakati vinakua havikuwa specialized saaana kama vinavyoonekana baadaye. Nakuongezea na hii: wakati vinajidevelop vilikuwa katika mazingira wezeshi zinasaidiwa chakula na hewa na kila kitu mojakwa moja kutika katika mazingira. Kwa miaka mamilioni huko ilikuwa ni bahari ya molekyuli 'primordial soup'

Kwa sasa ndiyo amniotic sac na placenta na mmama mzima anayemzunguka mtoto ndiyo anayemsaidia kabla hajatimia kujitegemea. Napumzika mazee.
 
Ona sasa kumbe inaonesha wewe hutaki ushahidi wa evolution.

Bali unataka evolution ifanyike upya ili na wewe ushuhudie upige na picha!

Kila siku tunaona unicellular zygote inabadilika kuwa multicellular embryo bado unataka ushahidi gani.
Basi hii sentensi ya mwisho inaonesha hujui unachokisema. Rudi darasani tena aisee. Zygote wa multicellular ni unicellular oganism ambaye anakuwa multicellular? Can you explain the magic? All multicellular animals produce after their kind that's multicellular orgs!

Kujaribu kulazimisha growth stages ziwe proof ya evolution ni ucheshi. Kama ungeonyesha somehow zygote wa unicellular animal changed to multicellular then angalau ungekuwa umejenga kesi yako. Ila multicellular org kuzaa multicellular org sio evolution at all

Kuna swali uliuliza kuwa nini kilianza kati ya mapafu na moyo ukapewa majibu kwamba wakati vinakua havikuwa specialized saaana kama vinavyoonekana baadaye.
Hii chai! Ndio maana hujaleta data zaidi ya stori zaidi. Umesema kulikuwa na viungo primitive na hujaeleza taarifa umetoa wapi na hivyo viungo primitive vinafananaje ma vinafanyaje kazi. Na pia kipi kilitangulia ku evolve na kilifanyaje kazi bila kingine.

Umeyakimbia maswali ya moto haya. Unajua huna majibu na kuwa hadithi hizi mwenye akili timamu na moyo wa kuelewa hawezi kubali kufanganywa.

Hekaya za watu wazima...

Nakuongezea na hii: wakati vinajidevelop vilikuwa katika mazingira wezeshi zinasaidiwa chakula na hewa na kila kitu mojakwa moja kutika katika mazingira. Kwa miaka mamilioni huko ilikuwa ni bahari ya molekyuli 'primordial soup'
Naona magical wand ya mamilioni ya miaka hatimaye umeileta.

Boys and girls, loong ago and faaar away there was a chemical soup. Out of that came everyone. Claps to our great great great grandpa... Chem Soup!

That's magical folks! That's "science"!

Ah hizi stori tu kama za mama Debora Mwenda ws mama na mwana!

Kwa sasa ndiyo amniotic sac na placenta na mmama mzima anayemzunguka mtoto ndiyo anayemsaidia kabla hajatimia kujitegemea.
Mama anazaa mwanadamu, bacteria anatoa bakteria na kuku anatotoa kuku. Hakuna evolution hapo!
Napumzika mazee.
Rest In Peace bro. May God open your eyes. Blessings!
 
Mwaka 1859 mwanabaiolojia Charles Darwin alichapisha kitabu chake kuhusu chanzo cha viumbe wote duniani chenye jina “On the origin of species” Kilichoelezea theory yake ya evolution. Darwin alisema kwamba hivi viumbe vyote tunavyoviona leo (Aina Zaidi ya million 8.6) vikizagaa kwenye uso wa dunia havikuwa hivyo milele tangu mwanzo, lakini vilitokana na mabadiliko ya muda mrefu yanayoitwa evolution.
Evolution ni mchakato ambao aina mbalimbali za viumbe husitawi kutoka maumbo ya awali (viumbe vya awali) wakati wa historia ya dunia.
Darwin alielezea kwa ndani jinsi viumbe vinabadilika kulingana na sababu mbalimbali na akaelezea mechanism inayosababisha viumbe kubadilika na kutengeneza viumbe wapya (specie formation)
Mechanism kuu ni mbili ambayo ni Natural selection/Uteuzi wa asili na Variation/Tofauti katika viumbe.
i. Variation: Viumbe havifanani, kutokana na randomness/unasibu wa uzazi (Watoto hawafanani 100% na wazazi) na pia kuna mutation (Mabadiliko katika gene za viumbe) husababisha viumbe wa aina moja wasifanane. Mfano unaweza kufuga kuku wekundu tu bandani lakini baada ya vizazi kadhaa unaweza kuona kuku wanazaliwa wenye rangi tofauti.
ii. Natural selection/Uteuzi wa asili : Mazingira husababisha viumbe wenye sifa nzuri kuishi na wale wenye sifa mbaya hupotea. Hivyo katika mfano hapo juu, ikitokea waganga wanapenda kuku wekundu basi wale kuku wekundu watapotea lakini wale wengine wenye rangi tofauti wataishi….Hivyo baada ya muda mrefu itaweza kutokea kuku wa aina tofauti na wale wa mwanzo na kuleta aina nyingine ya kuku...Hii process ikiendelea kwa muda mrefu inaweza kutokea aina ya viumbe kama kuku lakini wametofautiana sana na kuku mpaka wanashindwa kuzaliana na kuku wa kawaida (Hivyo kiumbe kipya kinakuwa kimepatikana)

Lakini leo ni May Mwaka 2022 AD (Takriban miaka 163 baadae) Bado watu wanabishana kama hii concept ya Evolution ya Darwin ni ukweli (Fact) au ni nadharia tu (Theory).
Kwenye huu uzi nataka nielezee kama hii evolution ni fact au ni theory tu, na nitajaribu kujibu baadhi ya maswali yanayowasha vichwa vya watu wengi kuhusu evolution, hivyo twende Pamoja.
Ikumbukwe kipindi Darwin anachapisha kitabu chake Nyanja mbalimbali za kisayansi kama Genetics, embryology, Anatomy zilikuwa hazijatanuka na kuwa kama leo. Hata fossils zilikuwa hazijagunduliwa kwa wingi kama leo, Hivyo Darwin alipingwa na watu wengi sana kwakuwa kipindi hicho watu wengi waliamini Dunia iliumbwa kwa mara moja miaka isiyozidi 6000 nyuma. Kwakuwa leo Nyanja hizo zimetanuka na tunajua mengi Zaidi basi tuyapitie hayo mengi kwa kifupi.
i. Anatomy;
Viumbe wengi wanafanana maumbile kuashiria kuwa wana chimbuko moja. Mfano Mifupa ya mikono na miguu ya paka inafanana na mifupa ya binadamu nk. Nk.Viumbe vingi kwenye kundi moja hufanana sana maumbo, Hivyo viumbe vingi huonesha kuwa vilitokana na wazazi walewale/Chimbuko moja.
ii. Genetics.;
Mendel (Mwaka 1865) aligundua kuwa viumbe vinarithishana sifa kwa njia ya kuzaa kupitia vinasaba (DNA). Kwa kutumia sayansi ya kisasa kuziangalia hizi DNA wanasayansi wamegundua kuwa Hivi vinasaba vya viumbe mbalimbali vinafanana. Viumbe wa kundi moja (mfano mamalia) huwa na vinasaba vinavyofanana sana kuliko wale wa makundi tofauti. Hivyo huonesha viumbe vina chimbuko moja.
iii. Fossils
Mabaki ya viumbe wa zamani yamekuwa yakipatikana chini ya dunia. Mabaki mengi yameonesha kuwa hapo kale kulikuwa na viumbe ambavyo leo havipo tena duniani na mabaki hayo pia yameonesha kwa kiwango kikubwa jinsi viumbe vya leo vina chimbuko moja. Mfano ugunduzi wa Alesi pale Kenya umeonesha kuwa Alesi alikuwa ni kiumbe mwenye sifa za binadamu na nyani, hivyo alikuwa ni babu yetu sisi binadamu na nyani.
iv. Embryology
Hapa tunaangalia viumbe vikiwa ndani ya tumbo/Yai kabla havijazaliwa..Viumbe vingi katika ngazi za mwanzoni huwa vinafanana, mfano mimba ya mwezi mmoja ya binadamu, kile kijusi kinafanana na kijusi cha nyani,mbwa,papa,Ng’ombe nk. Ni katika ngazi za mbele za ukuaji ndipo vijusi huanza kutofautiana Hivyo inaonesha kuwa viumbe vyote vina chimbuko moja.

NB: Evolution imaonesha kuwa viumbe vyote duniani vina chimbuko moja, Yule kiumbe wa kwanza alitokanaje hilo ni swali na mada nyingine ambayo ni ya siku nyingine.

While Evolution haisapoti lakini pia haipingi uwepo wa Mungu (Unaweza kuamini kuwa Mungu aliumba kiumbe wa Kwanza ambaye aliendelea kuevolve na kuleta viumbe wote duniani)

View attachment 2230513

View attachment 2235709
It's common sense.Kama ingekuwa kweli Sokwe na Nyani wangegeuka watu,lakini wapo hivyo hivyo siku zote.Only a fool can accept that nonsense.Mwanadamu aliumbwa na Mungu,the Book of Genesis in the Bible makes it very clear.

Kwa nini wame-introduce huo uzushi?Nia ni kuwatenganisha Wanadamu na Mungu wao.
 
Jibu hili hapa
Kujibu swali moja common kuhusu evolution kabla halijaja ‘’Kama tumetokana na nyani, kwanini nyani wa leo hawageuki kuwa watu?’’
1. Hakuna mtu aliyesema tumetokana na nyani, lakini ni kuwa Nyani na sisi binadamu tumetokana na kiumbe kimoja (Babu yetu). Hivyo wajukuu wa hiko kiumbe wengine tumekuwa binadamu wengine wamekuwa nyani na miaka ijayo huenda binadamu tukabadilika kuwa kitu kingine na nyani wakawa kitu kingine (Evolution haina direction/goal) kwamba lazima nyani wawe watu. (Inawezekana baada ya miaka laki 2 ijayo nyani wakawa na mapezi kwakuwa dunia ilijaa maji ikabidi wajifunze kuogelea).

2. Evolution ni very slow process na inachukua miaka hata 50,000 mpaka mamilioni, kwahiyo kwa muda tuliokuwepo duniani mabadiliko kwa viumbe hutokea lakini katika nyanja ndogo sana (Mfano bacteria/virusi hubadilika kuzipinga dawa..ndiyomaana dawa nyingi hubadilika na muda). Hivyo ni ngumu kwa miaka 1000-6000 kuona nyani anabadilika kuwa mtu

Maisha yanabadilika sana, binadamu aliyeishi duniani miaka 2000 iliyopita sio sawa na binadamu wa leo. Leo binadamu anakula chakula kingi kwa wastani, anamulikwa na mwanga mwingi machoni (TV, Simu)..Kwahiyo binadamu anaweza kukua kiumbo kutokana na chakula(Binadamu wa siku hizi ni wakubwa kidogo tofauti na miaka ya 1700 kurudi nyuma) na pia anaweza kubadilika macho (Macho ya bluu kwa wazungu ni kitu cha hivi karibuni).
 
Vilikuwaje? Unaweza kueleza huyo "binadamu wa viungo simple" alikuwaje? Hivyo viungo rahisi vilikuwaje? Na utuletee data za chanzo chako cha hii habari.

Huu mfano wako dhaifu sana, so nitauacha tu!
Moyo primitive ulikuwaje? Kati ya ventricle na auricle kipi kili evolve kwanza? Je moyo primitive ulikuwa na veins?
Mapafu primitive yalikuwaje? Kati ya mapafu na moyo kipi kilitangulia? Kama ni moyo, ulihitaji oksijeni? Uliipataje? Kama ni mapafu, yalihitaji damu? Ilifikaje kwenye mapafu?

Ukiisha kujibu, naomba chanzo/data

Kwa aina ya argumentation from thin air kila argument inaanguka. Ila kitaalamu hamna kit kama primitive organ. Hazipo! Hazijawahi kuwepo!
Kama unakataa tupe mifano iliyokuwa observed!

Hizo primitive organs zikoje? Halafu hizi stori chanzo chake ni wapi? Ni nani aliye observe hizi mambo za primitive organs? Maana hakuna any scientific record ya organ yoyote kuwa primitive.

Kuna tofauti gani kati ya maelezo yako na hadithi za Alfu lela ulela?

Aisee, hii ni sayansi nayo? Inatokea wapi? Maana naona umepiga stori sana kuliko data na uhalisia. Umeongea abstracts kibao. Sijaona data ku support stori zako zote hizi.

Mpaka utakapoleta data, zitabakia kuwa hekaya, ngano na visasili!
Hakuna sehemu nimesema binadamu alikuwa na viungo simple, ila binadamu ametokana na Homo erectus alietokana na homo habilis alietokana na........yaani kadri tunavyorudi nyuma kiumbe kinakuwa simple zaidi ....tukirudi nyuma zaidi ndiyo tutakutana na kiumbe kilichokuwa na moyo simple (kinaitwa Pikaia)
Data zipo nyingi sana zimesheheni,nimekuonesha mpaka experiment mtu alifanya kufuga bacteria na kuangalia wakivolve in real time,,baada ya vizazi 50,000 wale bacteria wakawa na sifa tofauti kabisa na wale wa kwanza......Ila anzia hapa
Hapo wameweka ushahidi kibao mpaka wa genomics.

All in all ushahidi wa evolution ni mwingi sana tatizo wewe ni mvivu kugoogle tu kuutafuta.
Evolution ni FACT na facts waga hazijali hisia zako, FACT itabaki kuwa FACT hata kama kipo kitabu kilichoandikwa na wavuvi miaka 2000 iliyopita kitakataa hizo facts.FACT zitabaki kuwa facts
 
Hakuna sehemu nimesema binadamu alikuwa na viungo simple,
Kwa hiyo viungo vyake vilikuwa complex?
Maana kama havikuwa rahisi then vilikuwa tata
ila binadamu ametokana na Homo erectus alietokana na homo habilis alietokana na........
Hizi hadithi za kubumba bado unaziamini?
Shida yako toka mwanzo unatusomea tu standard evolution narrative bila kuleta evidence au data. Zi wapi data zinazoonyesha kuwa kulikuwa na hao homos?

Kwa sababu una assume kwamba waliwahi kuwepo. Kitu ambacho ni hekaya!
yaani kadri tunavyorudi nyuma kiumbe kinakuwa simple zaidi ...
Tunarudi wapi? Unaongea as if uko kwenye time machine unasafiri. Kwenye matamahuluku hatuoni hiyo simplicity. Kila kiumbe kwenye fossil record kipo kama kilivyo hakuna hiyo gradual simplicity. Hizo ni stori tu kama za mama na mwana!
.tukirudi nyuma zaidi ndiyo tutakutana na kiumbe kilichokuwa na moyo simple (kinaitwa Pikaia)
Hicho kiumbe lazima kwa hesabu zako kitakuwa kiliishi mamilioni ya miaka. Moyo hauwezi kudumu hata miaka 10. Sasa nani aliweza ku observe moyo wa huyo kiumbe wa kufikirika na hakukuwa na watu?

Halafu nikikwambia unaleta hekaya unagoma?
Data zipo nyingi sana zimesheheni,nimekuonesha mpaka experiment mtu alifanya kufuga bacteria na kuangalia wakivolve in real time,,baada ya vizazi 50,000 wale bacteria wakawa na sifa tofauti kabisa na wale wa kwanza....
Yaani ile stori yako ya bakteria kuwa bakteria nayo ni evolution? Ile ni adaptation. Mimi sina pingamizi na adaptation inatokea kwa viumbe kibao!

..Ila anzia hapa
Hapo wameweka ushahidi kibao mpaka wa genomics.
Ili mnyama mmoja aende kuwa mnyama mwingine lazima uongeze genetic information zinazotakiwa kubadilika. Genetic info zinapungua with time na sio kuongezeka. So genetically Speaking evolution ni chai. Haiwezekani
All in all ushahidi wa evolution ni mwingi sana tatizo wewe ni mvivu kugoogle tu kuutafuta.
Evolution ni FACT na facts waga hazijali hisia zako, FACT itabaki kuwa FACT hata kama kipo kitabu kilichoandikwa na wavuvi miaka 2000 iliyopita kitakataa hizo facts.FACT zitabaki kuwa facts
Evolution never happened anywhere except in minds of evolutionists. Evolution should be in same shelf as magic not science
 
Kwamba hii Corona kutokea huko ilipoanza mpaka kufikia Omicron haija-evolve ?
 
Back
Top Bottom