Je, GenZ wa Tanzania wanaweza kusimama kidete kama wenzao wa Kenya?

Je, GenZ wa Tanzania wanaweza kusimama kidete kama wenzao wa Kenya?

Bila shaka ni ukweli usiopingika kuwa maandamano dhidi ya serikali ni ya kwanza ya aina yake nchini Kenya.

Kwa nini?
Maandamano ya kupinga mswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2024 hayakuongozwa na Mwanasiasa yoyote Wala Chama chochote cha kisiasa; bali yaliratibiwa na vijana hasa wa kizazi Z kwa kutumia mitandao ya kijamii hususan wa X na TikTok.

Ni maandamano ambayo yalipelekea hata vyombo vya habari kubadili mbinu kwa kuwaalika studioni wageni kizazi cha GenZ, tofauti na ilivyozoeleka kualika wanasiasa na viongozi wakuu kutoka sekta mbalimbali.

Aidha kizazi hiki cha GenZ kilifanikiwa kuhamasisha watumiaji wa mitandao ya kijamii kutumia hashtag #RejectFinanceBill2024, na kuifanya trend hio kuwa nambari Moja duniani kwa zaidi ya posti milioni 2.

GenZ vilevile wanafanya michango mitandaoni kwa njia ya M-changa kulipa gharama za matibabu za wenzao waliojeruhiwa kwenye maandamano na kulipa gharama za mazishi ya wale waliopigwa risasi, mfano Rex Kanyeki Maasai, aliyeuwawa na polisi kwa risasi karibu na stendi ya Kencom Jijini, Nairobi.

Kizazi cha GenZ kimesisitiza kuwa hakina kiongozi na kuwa Kila mmoja ni kiongozi wa mwenzake.

View attachment 3022154
View attachment 3022156


Matukio ya Jana yameibua maswali mengi hasa hapa Afrika Mashariki:

• Wakenya wana uzalendo mkubwa kuliko wananchi wa taifa lolote lingine hapa Afrika Mashariki?

• GenZ wana athari Gani Kwa mustakabali wa siasa za nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

• Viongozi wa vyama vya kisiasa wajifunze nini kutoka kwa GenZ.

• Iweje ni Kenya tu ambapo kizazi hiki kinaweza kusimama kidete? Wako wapi Genz wa Tanzania, Uganda na Rwanda?

PIA SOMA
- Je, GenZ wa Tanzania wanaweza kusimama kidete kama wenzao wa Kenya?
Sidhani kama Watanzania wanaweza kuandamana kwa kuishinikiza serikali, haitatokea kwani hapa Tanzania wananchi haswa vijana wa Gen - Z bado ni mambumbumbu sana, wao wanachowaza ni kujiuza, kupiga picha za utupu na kusikiliza bongo fleva tu, hawana akili zaidi ya hapa.
 
Ni ishara kwamba Vijana wa Kenya sio MAZUZU/MAZEZETA kama huku kwetu.Huku kwetu tupo busy na Yanga,Simba,kumsifia mama yao,kubet,kuruka kwanja disko,ulevi na anasa nyingine kibao.Ile ripoti tu ya CAG ilitosha kabisa kuipeleka nchi kwenye uchaguzi mkuu lakini wapi...
 
Back
Top Bottom