Je, gharama hizi za ‘wiring’ zina uhalisia kwa nyumba ya vyumba vinne?

Je, gharama hizi za ‘wiring’ zina uhalisia kwa nyumba ya vyumba vinne?

Wdl

Senior Member
Joined
Jun 2, 2017
Posts
186
Reaction score
177
Fundi wa umeme amenipa hizi gharama. Hapo nilishavuta umeme na kufunga baadhi ya socket, na taa za nje.

Je, zina uhalisia kwa nyumba ya vyumba vinne?

Screenshot_20241208_202708_Adobe Acrobat.jpg
 
Fundi wa umeme amenipa hizi gharama, hapo nilishavuta umeme na kufunga baadhi ya socket, na taa za nje.....
Je zina uhalisia...nyumba ni vyumba vinne...
Chagua vya muhimu ingia dukani mwenyewe
 
  • Thanks
Reactions: rr4
Ahsante mkuu, but naomba ufafanuzi kwani 1.5 ameweka kuna pcs 14 na 10, pia 2.5 ameweka pcs 4 Red, blue & green....
Hizo ni rola, kwa ukubwa wa nyumba yako, anza kwa idadi hii:-
Waya 1.5 (kwa ajili ya taa)​
  • Nyekundu 3​
  • kijani 3​
  • Bluu 3​
Waya 2.5 (kwa ajili ya soketi, AC, jiko n.k)​
  • Nyekundu 3​
  • Kijani 3​
  • Bluu 3​
 
Mafundi umeme,ujenzi,madaktari lazima uwe na second opinion na quatation tofauti.Usiende kichwa kichwa.Nazungumzia uzoefu.
 
Fundi wa umeme amenipa hizi gharama, hapo nilishavuta umeme na kufunga baadhi ya socket, na taa za nje.....
Je zina uhalisia...nyumba ni vyumba vinne...
Hapo kwenye nyaya, makadirio yake ni zaidi ya mara 4 ya uhalisia. Roller moja ina urefu wa mita 100, kwa pc 14 ni sawa na mita 1400 sawa na urefu wa kilomita 1.4
Bila kupepesa macho, huyo fundi ni mdokozi wa material
 
Mimi sina experience ila hiyo bei kwa room 4 naona ni kubwa japo hajazidisha sana, labda kama anatumia vifaa ambavyo ni premium brands
 
Hapo kwenye nyaya, makadirio yake ni zaidi ya mara 4 ya uhalisia. Roller moja ina urefu wa mita 100, kwa pc 14 ni sawa na mita 1400 sawa na urefu wa kilomita 1.4
Bila kupepesa macho, huyo fundi ni mdokozi wa material
Sio mdokozi ni mwizi kabisa mana kwa nyumba ya kawaida kama iyo unaweza kutumia roller 3-4 za 1.5 na roller 1-2 za 2.5 hahaha
 
Uyo jamaa ni mwizi, cheki fundi mwingine akupe makadirio yake ya bei ili ulinganishe hizo gharama
 
Makadirio ya hiyo fundi ni Makubwa sana kuliko maelezo.

Kwa nyumba hiyo Eire ya 1.5 kwa makadirio ya juu zingekuwa 6 na waya ungebakia.

Ningeandika mengi lakini ningejua Mkoa ulipo ndo ningekushauri vizuri zaidi.
 
Back
Top Bottom