Kwenye idadi sijui umefunga vifaa vingapi. Ungetaja ukubwa wa nyumba tungeweza kushauri. Ila nilinunuaga 3x4 kwenye 2.5mm na 2x4 kwenye 1.5 nikafunga kwenye 2 appointments zenye vyumba viwili, sebule, jiko, choo, each.
Ila Kwa bei 2.5mm ni 75,000/-, na 1.5mm ni 45,000/-. Tena hii ni bei ya sie tulionunua pcs nne nne labda. Kwa wewe wa nyingi inaweza kushuka zaidi
Cha pili, waya za 2.5mm ni za kwenye sockets, na 1.5mm ni za kwenye bulbs. Sasa hizi 1.5mm nazo unanunua pea tatu tatu kwamba umefunga "earth" mpaka kwenye bulbs au??
Kingine hivi vifaa unampa hela akanunue mwenyewe? Au unaenda kununua wewe?
Na fundi akija saiti hua anakujaga na begi la kuwekea vifaa vyake vya kazi na kuondoka nalo kila siku? Au akija nalo siku ya kwanza haondoki nalo mpaka siku ya kumaliza??