Je, haki itatendeka sakata la Morrison na Yanga?

Je, haki itatendeka sakata la Morrison na Yanga?

kyemo

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2010
Posts
570
Reaction score
718
Kuna clip inatembea ikimuonyesha mchezaji Bernard Morrison akiwashukuru Hans Pope na Crescent Magori kwa kukamilisha usajili wake uku akiwa amevaa jezi ya Simba.

Kwa inavyoonyesha usajili huu sio wa Jana wala juzi bali toka zile sarakasi zilivyoanzishwa na Morrison,labda ni miez imepita.

Hans pope ambae amehusika kwenye usajili wa Morisson kwenda Simba inasemekana ni mjumbe wa kamati ya katiba,sheria na hadhi za wachezaji ambao watakaa kesho tarehe 10/08/2020 kutoa maamuzi juu ya sakata hilo.

Je mnadhan ni kweli haki itatendeka ilihali Simba washamtangaza kuwa ni mchezaji wao kabla ya TFF kupitia kamati yao hawajatoa maamuzi kama Morisson bado ana mkataba na Yanga au hapana.

Je maamuzi yashafikiwa na kuvuja kupitia Hans Pope ndio maana Simba wameamua kumtangaza kabisa kuwa wamemsajili Morrison.
Au kuna sarakasi imechezwa tayari ambayo Simba wanajua ni rahisi kuimudu?

Wajumbe tujadili!

Kesi kubwa hapa itakajua kama Yanga ni kweli wanamkataba na Morison, hiyo hata Hans yupo kwenye kamati hawezi kubadili mkataba ka ulikua halali. Suala la mkataba tusubiri kesho maana hatuwezi kuwaamini sana Yanga wakati yeye Mhusika anasema hana mkataba nao, tuwasubiri TFF
 
Inshu ni je yanga huo mkataba ulipo TFF ni halali wa miaka miwili hakuna janja janja? Suala litakuwa limekwisha! Ila ninacho hisi kutakuwa na shida juu ya uhalali wa huo mkataba! Kesho sio mbali.
 
Uswahili wa Yanga mwisho kesho mmezoea kudanganya wakina Ngasa kwa kiswahili. Kumdanganya Morrisoni kwa kiingereza chenu mnachoongea mkinywa pombe mmeshindwa!! Mpasuko ni kesho kwani Boss kumbe naye anataka ten percent na magumashi ha ha
 
Kesho ndo tutajua uswahili wa yanga na vile vizee vichawi,,, tatizo la yanga ni migogoro isiyoisha na vile vizee vipiga bao.
 
Kesi kubwa hapa itakajua kama Yanga ni kweli wanamkataba na Morison, hiyo hata Hans yupo kwenye kamati hawezi kubadili mkataba ka ulikua halali. Suala la mkataba tusubiri kesho maana hatuwezi kuwaamini sana Yanga wakati yeye Mhusika anasema hana mkataba nao, tuwasubiri TFF
Je Yanga kuwa na mkataba au kutokua na mkataba inahalalisha Simba kumsajili na kuweka hadharani kabla maamuzi hayajatoka?
 
Inshu ni je yanga huo mkataba ulipo tff ni halali wa miaka miwili hakuna janja janja? Suala litakuwa limekwisha!! Ila ninacho hisi kutakuwa na shida juu ya uhalali wa huo mkataba!! Kesho sio mbali
Kama hakuna dole gumba kutakua na tatizo kuthibitisha maana ndio kama hvyo anadai sahihi imefojiwa
 
CEO WA simba kajiuzulu leo kupisha wapumbavu na wenda wazimu akina manara waendelee na upuuzi wao
Inawezekana kajiuzuru moja ya sababu ni kutokubaliana na jinsi issue ya Morrison ilivyoenda
 
Hili nililitegemea hundred percent
IMG-20200809-WA0009.jpg
 
Je Yanga kuwa na mkataba au kutokua na mkataba inahalalisha Simba kumsajili na kuweka hadharani kabla maamuzi hayajatoka?
Simba imemsajili kwa sababu ni mchezaji huru, ko kisheria haitaji kusubiri hukumu
 
Kama hakuna dole gumba kutakua na tatizo kuthibitisha maana ndio kama hvyo anadai sahihi imefojiwa
Ninachofahamu siku hizi fomu zote za usajiri lazima ziwe na sehemu ya kuweka dole gumba!! Ili kuzuia uhuni uhuni!! Hapo kuna shida, kwani yeye si anatakiwa awe na nakala ya mkataba?!! Nakala yake inaonyesha vipi? Toka wafanye siasa kwenye sakata la shishimbi, cna imani nao tena!!
 
Hivi magori ana nafasi gani katika Simba SC kwa maana cheo?
 
Back
Top Bottom