ToniXrated
JF-Expert Member
- Sep 21, 2022
- 1,134
- 2,993
Habari zenu!
Jana wakati narudi zangu nyumbani usiku nikakatisha mtaa wa Nzasa unapokutana na Mtaa wa Morogoro hapa ilala ,jijini dar-es-salaam nikakutana na rundo la takataka .Ni muda takribani wiki sasa halmashauri ya jiji imeshindwa kazi ya kulifanyia usafi soko kuu la mbogamboga la ilala. Wanachojua ni kukusanya tu ushuru kila siku huku wakiwa hawafanyi usafi wala kuzoa takataka zilizolundikana mitaani.
Halamshauri ya jiji yapata miezi miwili hamjawalipa wafanyakazi wa usafi ,kitendo kilichopelekea wagome kusafisha soko na hivyo kusababisha kujaa kwa takataka mitaani. Kumbukeni kuwa hili soko la ilala ndio soko kubwa la wakulima, linalouza mbogamboga na matunda na kuna maelfu ya watanzania wapo wanaafuta riziki kila kuchwapo. Iweje kila siku mchukue ushuru wa shilingi 500 kwa maelfu ya wafanyabiashara wa soko hili halafu mshindwe kusafisha soko?
Sisi kama wakazi wa Ilala tunaiomba Serikali ya Mama Samia kupitia wizara ya TAMISEMI kuhakikisha kuwa wanaohusika na udhalimu huu waajibishwe na hii kazi muwape wazabuni watakaoweza kukusanya ushuru na kuhakikisha mazingira ya soko yanakuwa safi kila siku. Huu ni mwezi wa Desemba ,kuna taka nyingi za maembe masokoni, Je mnataka kutokee mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ndio mfurahi??? Je mnataka watu wafe!!
Tunaitaka Serikali ichukue hatua haraka sana kuhakikisha usafi unafanyika na usalama wa raia unakuwepo.
Pascal Mayalla