Je hapa Askari wa usalama barabarani hakuvunja sheria?

Je hapa Askari wa usalama barabarani hakuvunja sheria?

Good Father

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2014
Posts
10,321
Reaction score
18,574
Habari zenu wanajf kwa ujumla.

Nawapa kisa kimoja kilichotokea wakati niko kwenye daladala mali ya UDA, ilikua jumatatu ya wiki hii nilipopanda gari la UDA lililokua linatoka ubungo kwenda gongo la mboto, tulipofika kwenye taa za TAZARA kulikua na foleni sio ndefu sana ya kutisha.

Pembeni yangu kuna jamaa alionekana anaongea sana mara akamwambia konda anataka kushuka wakati gari linasubiri foleni ili likate kona kuingia nyerere road, konda akakataa hivyo wakabishana sana mwishowe konda akamwambia mwambie askari kama akikuruhusu utashuka, jamaa akamuita askari(traffic) akamsalimia kwa lugha ya kiingereza na kumwambia anataka ashuke, askari hakutoa neno alimuonyesha ashuke kwa ishara ya mkono kisha jamaa akashuka kwa majivuno huku anamcheka konda, yule askari akaondoka zake.

Mimi nikaanza kuwaza kwanini yule askari alimruhusu yule jamaa ashuke wakati sheria za usalama barabarani zinakataza mtu kushuka sehemu isiyo na kituo na istoshe magari yangeweza kuruhusiwa muda wowote.

Pili huyu traffic angemruhusu yule jamaa kushuka endapo yule jamaa angeomba kwa kiswahili??

Hivi sheria inafanyaje kazi au kama konda angemshusha yule jamaa je asingekamatwa? Na kama angekamatwa kwann akamatwe wakati hata traffic anaruhusu??

Wanasheria nisaidieni nijue hizi sheria zikoje au kwa kiingereza mambo yanabadilika
 
Ulikuwa wapi siku zote hizi mpaka unatuletea story ime-expire!

We jamaa vipi.
 
Samehe mkuu saba mara sabini ila ndicho nilichokiona

Umesamehewa, siku nyingine leta habari moto moto, sio kiporo!

Askari yeyote yule sitaki kumsikia, nimewaweka category moja na majambazi. Nikikuta anapigwa naongezea.
 
Back
Top Bottom