Je, hapa kuna kesi ya Wizi?

MKWANO

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2014
Posts
230
Reaction score
159
Nina ndungu yangu kashtakiwa mahakama ya mwanzo; kesi iko hivi.

Huyu ndugu alipelekewa simu (smart phone) na rafiki yake wa kike amsaidie kuaply kazi za Tamisemi badae sensa, amekaa na Ile simu Miezi 3, mara nyingine akawa anairusha kwa mwenye simu na ikitokea kazi sehemu anapelekewa tena.

Bahati mbaya ikapotea mikononi mwa ndugu yangu, akarepot police na Rb akapewa, then akaongea na yule dada namna ya kumfidia simu yake wakaelewana.

Sasa amejitokeza jamaa anayedai Ile simu ni yake, na alimpa yule Dada, yule jamaa kafungua kesi kumshtaki ndugu yangu, na yule dada aliyempelekea simu ndugu yuko Huru na atasimama kama shahidi wa mdai.

Je, ndugu yangu kisheria anakesi? Ushahidi wa mawasiliano baina yake na mdada kuhusu makubaliano ya kulipana upo.

Tushauriane
 
Ndugu yako amepoteza simu na kuripoti polisi tukio hilo, na kupewa RB (hapa pa RB fafanua kidogo).

Huyu mdai anasema alimpa simu dada, ila kesi amefungua anamdai nduguyo, kivipi?? Si amdai aliyempa
 
Amlipe simu yake mambo yamesha kua mengi na kama hana uwezo, ww ndugu yake msaidie kama mdai alivyo saidiwa kwa upande wake! Simu kitu gani! Nayo mpaka uombe ishauri!!? Ingekua ni hiyo yako imepotea kwenye mazingira hayo ungekubali!?
 
Ndugu yako amepoteza simu na kuripoti polisi tukio hilo, na kupewa RB (hapa pa RB fafanua kidogo).

Huyu mdai anasema alimpa simu dada, ila kesi amefungua anamdai nduguyo, kivipi?? Si amdai aliyempa
Siku simu imepotea kulikuwa na vitu vinginevyo kwenye bag lake,hivyo alilirepot Kituo Cha police kupata loss report,then akamjulisha yule Dada juu ya kilichotokea.

Kashtakiwa yeye kwa wizi na yule jamaa aliye mpa simu yake yule Dada. Kesi haijaanza kusikilizwa ila tuna hofu
 
Amlipe simu yake mambo yamesha kua mengi na kama hana uwezo, ww ndugu yake msaidie kama mdai alivyo saidiwa kwa upande wake! Simu kitu gani! Nayo mpaka uombe ishauri!!? Ingekua ni hiyo yako imepotea kwenye mazingira hayo ungekubali!?
Hataki kulipwa,huyu mlalamikaji ni askari lakini alimweka dogo ndani bahati nzuri tuliweza kumtoa kwa msaada wa Viongozi wake ( RCO+ RPC) na wao pia walipendekeza alipwe yule dada na amkabidhi mwenye simu,ila kaipeleka kesi mahakamani kimya kimya na kusudi lake hatuelewi
 
Huyo mshamba! Ndio bwana ake na huyo dada! Mshamba huyu! Mijitu kama hiyo anapo haribu nawewe unamuharibia! Tafuta details na wewe muweke hadharani! Ila kwa minajili hiyo kutakua na tatizo lingine linalo mpelekea huyo jamaa kufanya hivyo hiyo simu ni gear tu aliyopata
I
 
Sikiliza, jamaa kampa simu demu, demu kampa hiyo simu mdogo wako, simu ikapotea mikononi mwa nduguyo. Jamaa aliyempa simu demu, hawezi kumshtaki nduguyo kwa wizi, labda amshtaki kwa kosa la kununua mali ya wizi. Wizi maana yake ni kuchukua kitu kisicho chako kutoka mahali fulani na kukifanya chako.

Sasa mdogo wako hajachukuw simu kwa jamaa, hivyo jamaa hawezi mshtaki kwa wizi. Mkianza kusikiliza kesi mhojini simu iliibiwaje
 
Tumetoka mahakamani mida hii, tumeweka mwanasheria lakini inaonekana tumetibua mipango yao,maana Hakimu kaahilisha kesi bila sababu,kuna alafu ya mipango ovu ilikuwa imepangwa/ imepangwa.
 
Tumetoka mahakamani mida hii, tumeweka mwanasheria lakini inaonekana tumetibua mipango yao,maana Hakimu kaahilisha kesi bila sababu,kuna alafu ya mipango ovu ilikuwa imepangwa/ imepangwa.
Kama mna wakili basi atawaongoza ipasavyo.
 
Tumetoka mahakamani mida hii, tumeweka mwanasheria lakini inaonekana tumetibua mipango yao,maana Hakimu kaahilisha kesi bila sababu,kuna alafu ya mipango ovu ilikuwa imepangwa/ imepangwa.
Maana yake mchepuko alikuwa na mchepuko.
 
Story ya upande mmoja haimake sense kutolea uahauri wa kina.

Kaa nao wote wawili uwasikilize utapata cha kuwashauri
 
Ila serikali iangazie hizi mahakama za Mwanzo,watu wanabumbiwa kesi na kuumizwa sana,hii kesi imenifunza vitu vingi sana
1. Ni mwezi na wiki kesi inasomwa na Hakimu lakini kumbe kesi haijasajiliwa na haina namba.
2. Kesi ya jinai,lakini haina ile form ya HATI ya mashtaka,wala form ya malalamiko Bali ni plain paper iliyobumbwa tu
3. Mhe Hakimu kajitoa baada kuona kuna mwanasheria

Swali, (a) kwa nini ajitoe leo baada ya kuisoma kwa zaidi ya mwezi na wiki?
(b) inaruhusiwa Mhe Hakimu kumpigia mlalamikaji simu kumtaarifu kuwa mshatikiwa amefika ili nae afike mahakamani?

Nitayaweka majina yake na mahaka pindi kesi ikiisha
 
Story ya upande mmoja haimake sense kutolea uahauri wa kina.

Kaa nao wote wawili uwasikilize utapata cha kuwashauri
Huyu askari hawezi kukubali kunisikiliza, kwa sababu siku amemweka ndani huyu ndugu niliitumia nguvu ya Viongozi wake mkoa kumtoa,nikijua kaonewa,pia Viongozi wake walishauri tukae chini jinsi ya kumlipa yule Dada ili amkabidhi simu yake askari,na kesi kaipeleka mahakamani bila idhini ya kiongozi wake yoyote,wala hawajui
 
Nenda TAKUKURU maana huo ni utapeli unaofanywa na polisi.
Usijali kama atapoteza ajira au la.maana kumtoa polisi mmoja mhalifu ofisini umeokoa nafsi zaidi ya 200 zisizo na hatia.

Nenda Takukuru kawaelezee wata hunguza na watajua kama ni kesi ya kubambikizia au la
 
Huyo Askari kapeleka Kesi Mahakamani kwani yeye ndie Mpelelezi wa Kesi?? haiwezekani Mlalamikaji awe huyohuyo Mpelelezi wa Kesi
 
Na uyo jamaa kwann naye achukue simu ya watu
 
Huyo Askari kapeleka Kesi Mahakamani kwani yeye ndie Mpelelezi wa Kesi?? haiwezekani Mlalamikaji awe huyohuyo Mpelelezi wa Kesi
Mpelelezi yupo ila ni Kituo kimoja,na hata mpelelezi alikuwa anashinikizwa tu, kesi ilivyopelekwa mahakamani na mlalamikaji kumwondoa mchepuko wake kwenye kesi na kuwa Shahidi wake, Hakimu alimwambia mashtaka yaandaliwe upya na mpelelezi,
Hadi Hakimu anajitoa kwenye kesi hati ya mashtaka ilikuwa haijabadilishwa,maana yake ni kwamba mpelelezi haoni kesi kama ilivyokuwa kwa RCO NA RPC wake ila kulikuwa na mpango ovu waliupanga Kati ya mlalamikaji na Hakimu dhidi ya mshitakiwa

Kilichotibua yote ni kumweka Mwanasheria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…