Frumence M Kyauke
JF-Expert Member
- Aug 30, 2021
- 630
- 1,262
Mimi binafsi ni binadamu ambaye nikifika mwisho au nikisema inatosha, jua ama zako au zangu. Hakuna suluhu. Tafuta chaka lako la kujificha.
Moja ya sifa za msanii King Kiba ni kuhimili mikikimikiki. Ni kuhimili nyakati ngumu na kukimbilia kusema kwa mama yake.
Lakini ukweli msanii Harmonize sina hakika kama angeweza kuhimili visanga na vimbwanga alivyotendewa King Kiba. Wangekuwa wameshauana siku nyingi.
King Kiba ndiye msanii ambaye alipambana na kundi kubwa zaidi kuliko msanii yeyote Tanzania na kuendelea kuwa juu kimuziki.
Wengine wengi waliishia kurudi nyuma. Mtazame Belle 9, Shettah, Ommy Dimpoz, Ben Pol na wengine, wapo wapi baada ya mapambano mazito?
Kidogo kilichomnusuru Ommy Dimpoz ni ubalozi wa Kampuni ya GSM na ukaribu wake na King Kiba. Ile sumu aliyowekewa Ommy Dimpoz, wote tusio na koneksheni na matajiri tungeshakufa muda mrefu na kusahaulika.
King Kiba alipambana na watu walio na ushkaji wa muziki wa Bongo Fleva wenye sapoti ya kutosha. Huwezi kuacha kutambua nguvu ya marehemu Ruge. Nguvu hiyo yote iliwekezwa kwa mtu mmoja ili awe juu ya King Kiba.
Waliotaka kumpoteza walihakikisha wanafunga njia zote za King Kiba kufanya shoo nje ya nchi huku wakimchomekea mameneja ambao wanavujisha siri kwao.
Mameneja wote wa King Kiba katika historia ya muziki wake wamewahi kutoa siri na mikakati yake ya kimuziki.
Mameneja wote wa King Kiba waliopita wamewahi kutoa siri wakijua watafanya kazi vizuri. Kumbe wanatoa siri za kummaliza King Kiba. Umbumbu wa mameneja wa King Kiba waliopita ulikuwa kumuamini zaidi mtu mmoja ambaye ni mmiliki wa chombo cha habari. Kwa namna yeyote ile, mtu huyo hawezi kukubali msanii aliyeshiriki kumtengeneza aonekane msanii mdogo kwa sababu tayari amewekeza kwake.
Waliingia ndani zaidi na kuanza kushawishi ndugu zake wa karibu wawe upande wao, kundi hili walimpata ndugu mmoja wa King Kiba ambaye ni mtoto wa mama yake mkubwa na kuanza kumbomoa King Kiba kwenye familia yake. Bila shaka hadi leo upande wa mama yake King Kiba undugu wao umegawanyika.
Hatua hizi zote walizofikia mahasimu wa King Kiba hadi kwenye familia yake, hazijafikiwa hata robo kwa Harmonize.
Kila aliyekuwa karibu na King Kiba alijitahidi kumvuta awe upande wao ili kumfanya King Kiba ajione mkosefu. Marafiki wengi walianza kumuona King Kiba ni mkosefu na huyo mwingine ndiye mtu poa.
Kila studio ambayo King Kiba alitia mguu ili kufanya kazi walihakikisha nao wanahamia na kujenga urafiki na maproducer ili ngoma za King Kiba ziwe zinavujishwa kwao.
Tazama kwa uchache vita hii kama ungeweza kuhimili!
Je kwa mawazo yako Harmonize ataweza?