Je, hawa ndio wapo nyuma ya mkakati wa kutaka kutenganisha Uenyekiti na Urais?

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2021
Posts
1,505
Reaction score
4,427
Ni ajabu sana hawa vijana machachari wenye uwezo mkubwa wa kulinganisha na kufaninisha utendaji wa watu kushindwa kuzungumzia hata kwa kificho, tetesi zinazoenea mitandaoni za kutaka kutenganisha kofia ya Uenyekiti wa CCM na Urais wakiwa kimya mpaka muda huu na kushindwa kuongea chochote. Kwa kweli nimeshangaa sana?

Suala la utamaduni wa CCM wa kuvaa kofia mbili pamoja, vijana hawa wanalijua lakini kukaa kwao kimya wanafanya walete sintofahamu ya kinachoendelea baina yao. Pengine wana mpango na wapo nyuma ya mpango wa kitu fulani kwa sababu wahenga wanasema kimya kingi kina mshindo mkuu.

Swali: Je, hawa vijana wapo nyuma ya mkakati huo ovu? Tutafakari pamoja
 
Tanzania itabidi tubadilike,hoja za watu mara kofia ya uenyekiti haitusaidii,tutazame tunataka nini kama wananchi,hoja zetu ziwe maendeleo.

Na mnataka saa zote watu waongelee tetesi?na kama kuna mgawanyiko huko si ndio fursa sasa ya vyama vingine kujiimarisha.
Tunataka maendeleo,hiyo mambo ya kofia hatutaki kujua.

Mpeni mama muda afanye kazi.

Naamini hata mshaanza kumchokesha na madai kila siku.
 
Mpeni mama muda afanye kazi
Naamini hata mshaanza kumchokesha na madai kila siku.
Hata hayo ni maendeleo pia kwani ujui mambo ya kofia uathiri maendeleo pia.
 
Labda unieleze mimi kama Mtanzania kofia ya uenyekiti inaniathiri wapi.
Kofia mbili uzalishaji udikteta.Umeona madhara ya kuongozwa na dikteta.

Mwafrika hana uwezo wa kuongoza Jamii ni lazima awekewe mfumo wa kumdhibiti Ili asiumize jamii.Raisi anamuogopa mwenyekiti wa chama kwa maana akienda kinyume na katiba anafutwa uanachama na uraisi wake unakoma hapo hapo kama ilivyo ANC au ZANU PF.Kila mmoja anakuwa na nguvu eneo lake.
 
Ongeza nyama kidogo basi kwenye huu uzi. Nimekuja mkuku kusoma orodha ya waliopo nyuma ili nikawasemehe kwa mama lakini hakuna nilichoambulia.

Weka majina yao uzi uchangamke basi hata kama ni ya kutunga mkuu.
 
Hamjawahi kuongozwa na dikteta,unajua mnashangaza,kuna nchi huwezi jaribu hata kutusi Rais ukabaki safe.
 
Ongeza nyama kidogo basi kwenye huu uzi. Nimekuja mkuku kusoma orodha ya waliopo nyuma ili nikawasemehe kwa mama lakini hakuna nilichoambulia.

Weka majina yao uzi uchangamke basi hata kama ni ya kutunga mkuu.
Wale wapenda madaraka ndiyo wanaeneza uchochezi huu. Shida wenzenu watolewe uwaziri mpewe nyinyi. Wazazi wenu walikula mnataka mpaka wajukuu wale.
 
Kofia mbili ni lzm zitenganishwe Ili kuzuia udikteta nchini kwani madikteta still wangalipo.
Kwa msukuma mwenzenu mbona hamkuzuia ilo mbu.zi nyie, safari hii mtatiwa adabu,ngojea mama apewe uenyekiti wa chama
 
Tanzania itabidi tubadilike,hoja za watu mara kofia ya uenyekiti haitusaidii,tutazame tunataka nini kama wananchi,hoja zetu ziwe maendeleo.

Na mnataka saa zote watu waongelee tetesi?na kama kuna mgawanyiko huko si ndio fursa sasa ya vyama vingine kujiimarisha.
Tunataka maendeleo,hiyo mambo ya kofia hatutaki kujua.

Mpeni mama muda afanye kazi.

Naamini hata mshaanza kumchokesha na madai kila siku.

Mijadala ya hivi inazuia vipi maendeleo? Au uwezo wako wa kuchakata mijadala ya hivi na maendeleo ni mdogo?
 
mimi kama kijana Mzee naunga mkono hizi kofia mbili zitenganishwe.
 
Tanzania kuna vijana zaidi ya mil. 30, sasa wewe unaposema hawa vijana machachari tukuelewe vipi?
Katika hao vijana milion 30 toa vijana wa yanga waliobaki wote ni machachari
 
Mijadala ya hivi inazuia vipi maendeleo? Au uwezo wako wa kuchakata mijadala ya hivi na maendeleo ni mdogo?
Humu mara nyingi mijadala ya maendeleo hakuna,hata wewe pia labda uelewa wako ni mdogo zaidi huwezi nielewa.
Tunapoteza muda kujadili kofia ya uenyekiti what for?
Tunataka serikali itatue kero zetu,mambo ya ndani ya chama ni yao.
 
Kwa msukuma mwenzenu mbona hamkuzuia ilo mbu.zi nyie, safari hii mtatiwa adabu,ngojea mama apewe uenyekiti wa chama
Aliyepania kunyoosha watu,kanyooshwa yeye.Ukijua hii wenzio wanajua ile.
 
Back
Top Bottom