๐—๐—ฒ, ๐—ต๐—ฎ๐˜„๐—ฎ ๐—ป๐—ถ ๐—ฎ๐˜€๐—ธ๐—ฎ๐—ฟ๐—ถ ๐˜„๐—ฎ ๐˜‚๐˜€๐—ฎ๐—น๐—ฎ๐—บ๐—ฎ ๐—ฏ๐—ฎ๐—ฟ๐—ฎ๐—ฏ๐—ฎ๐—ฟ๐—ฎ๐—ป๐—ถ ๐—ฎ๐˜‚ ๐—ง๐—ฅ๐—”?

๐—๐—ฒ, ๐—ต๐—ฎ๐˜„๐—ฎ ๐—ป๐—ถ ๐—ฎ๐˜€๐—ธ๐—ฎ๐—ฟ๐—ถ ๐˜„๐—ฎ ๐˜‚๐˜€๐—ฎ๐—น๐—ฎ๐—บ๐—ฎ ๐—ฏ๐—ฎ๐—ฟ๐—ฎ๐—ฏ๐—ฎ๐—ฟ๐—ฎ๐—ป๐—ถ ๐—ฎ๐˜‚ ๐—ง๐—ฅ๐—”?

Mdude_Nyagali

Member
Joined
Dec 11, 2022
Posts
79
Reaction score
1,444
Jana tumepoteza watu 14 katika ajali iliyohusisha roli na magari mengine likiwemo basi la abiria mteremko wa Simike Mbeya. Kinachonisikitisha ni kwamba eneo hili lina askari wa usalama barabarani ambao badala ya kuongoza magari kutokana na hatari ya eneo hilo wao muda wote wako busy kukagua madeni ya faini.

Kwa sasa nchi nzima askari wa usalama barabarani hawako kwa ajili ya usalama barabarani tena, isipokuwa wamekuwa TRA kazi yao kubwa ni kukusanya fedha. Ndio maana wanajificha na tochi ya spidi ili madereva wakosee na wawapige faini wapate pesa badala ya kuwadhibiti wasikosee kupunguza athari za ajali. Huu ni upumbavu ndio maana tunahitaji #katibaMpya tuweze kubadili mifumo ya uendeshaji wa taasisi ikiwemo polisi.

Kuna siku pale Kitonga kulikuwa na foleni ya kubwa baada ya roli moja kupata break down. Ikalazimu tushuke kwenda kuongoza magari wenyewe ili tupite, baada ya kupita mita 600 tukawakuta wamejificha sehemu na tochi ya speed wakisubiri kuwavizia madereva wanaoshuka kwa spidi mlima Kitonga. Nilimshawishi my bro Mwabukusi asimamishe gari ili tuwape vidonge vyao kwa bahati mbaya eneo likikuwa baya hakuna parking unaweza kusimama.

Askari wa usalama barabarani sio TRA bali kazi yao ni kuhakikisha usalama wa vyombo vya moto na abiria wanaovitumia huko barabarani. Nafikiria kushauriana na mawakili wangu kama naweza kufungua kesi inayoweza kuwarejesha askari wa usalama barabarani kusimamia usalama barabarani badala ya kuwa TRA.

Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.
 
Sasa kiongoz gari limefeli breki apoo askari anauhisika vip kwenye hilo na mashuuda wanakwambia kabisa dereva alijitaid kukwepa baadhi ya magar mpaka kwenye iyo Costa ya abiria
 
Back
Top Bottom