Mzukulu
JF-Expert Member
- Feb 14, 2020
- 1,401
- 2,641
Ukipitia Vyombo vya Habari kama Clouds tv na Mwananchi bila kusahau na vinginevyo vichache utaona wameandika kuwa akina Mbowe na Wenzake wameshindwa Kulipa Faini leo Mahakamani katika muda uliopangwa na wameenda Segerea wakimaanisha Kuanza Vifungo vyao . (Mainstream Media)
Lakini hapo hapo tena ukipitia Mitandao ya Kijamii mbalimbali na hasa ile ya Wakosoaji (Critics) na ile ya Wanaharakati (Activists) bila kusahau ile ya Chama husika wanachotoka Washtakiwa utakuta Watanzania tunahimizwa tuendelee Kuchangia kila tulichonacho ili Wahusika watoke. (Social Media)
Kwa niaba ya Watanzania tuliopata huu Mkanganyiko wa Kitaarifa Mzukulu nauliza je, Faini inatakiwa ilipwe leo ( japo muda umeshakwenda ) au Mahamaka iliweka muda Maalum kwamba labda hadi Kesho wanaweza Kulipa na Wahusika ( Wapendwa Wetu ) Kidemokrasia wakatoka?
Kilichoniuma zaidi hasa ni kuona Vyombo kama Clouds Tv na Mwananchi nao wameshindwa Kuelewa Utaratibu mzima wa ulipaji Faini upoje hadi wameripoti ( hasa katika Kurasa zao za Mitandao ) kuwa akina Mbowe na Wenzake wameshindwa Kulipa na sasa wanaenda Kutumikia Vifungo vyao Segerea.