POTOSHI Je, haya ni magari aliyoyaacha Marehemu Genius "Ginimbi" wa Zimbabwe?

POTOSHI Je, haya ni magari aliyoyaacha Marehemu Genius "Ginimbi" wa Zimbabwe?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1

Video hii inasambaa sana huko kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha magari ya kifahari kama Lamborgini na rolls royce zinazodaiwa kuwa za Marehemu bilionea maarufu kule Zimbabwe aliyefahamika kama Ginimbi.
Screenshot 2026-10-03 110620.png
 
Tunachokijua
Ginimbi, jina lake halisi likiwa ni Genius kadungure alikuwa ni Milionea kutokea Nchini Zimbabwe akiishi maisha ya kifahari huku watu wengi wengi wakiyaona maisha yake hayo kupitia mitandao ya kijamii kabla ya kuaga dunia mwaka 2020 kwa ajali ya gari.

Madai

Kupitia mtandao wa X mtumiaji mmoja alichapisha video ikiambatana na ujumbe unaoleza kuwa kabla ya Wicknell Chivayo, Zimbabwe ilikuwa na Gonimbi ambaye baada ya kifo chake ameacha mali nyingi za kifahari ikiwemo magari ambayo yanaoza tu kwenye 'Yard'.

Uhalisia wa madai hayo

Madai hayo yanajiri mara baada ya kifo cha Wicknell Chivayo, tajiri kutoka Zimbabwe aliyefariki Septemba 30, 2026 kwa ajali ya helkopta nchini humo. Kifo cha Chivayo kimeibua upya kisa cha Ginimbi ambaye maisha yake ya utajiri hayakutofautiana sana.

Lakini je video inayosambaa na kudaiwa ni mali alizoziacha Ginimbi ni ya kweli? JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa kipande hicho cha video kimekuwepo mtandaoni kuanzia mwaka 2025 ambapo kilichapishwa katika mtandao wa TikTok.

Video hiyo ilirekodiwa katika Yard ya magari yasiyotumika huko Dubai ambapo kumekuwa na magari mengi ya kifahari ikiwemo Lamborghini na Rolls Royce, ufuatiliaji umebaini kuwa kumekuwa na video nyingi zilizorekodiwa kutoka katika eneo hilo kwa wakati tofauti mathalani hapa na hapa.

Kwa kutumia google earth eneo hilo linafahamika kama Copart UAE Auction.
1791103215068-png.3683482

1791103256352-png.3683487
Back
Top Bottom