Je haya yafuatayo yanaweza kufanya uchaguzi kufutwa?

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Naomba kuwauliza Wanasheria waliobobea kwenye sheria. Je haya yafuatayo yanaweza kufanya uchaguzi kufutwa:-
  • Mwenyekiti kutangaza matokeo kabla ya nyaraka zote hazijafika na yeye amekubal kuwa alifanya hivyo.
  • Kama kuna tofauti ya kura za vituoni na za Wilayani.
  • Kama sahihi zilizomo kwenye karatasi za kujumulishia kura za vituoni na Makao Makuu ya Wilaya siyo za wale walioteuliwa na Tume.
  • Kama kura za Rais zinazidi kura za wagombea wengine kwa idadi ili hali sheria inasema unapoingia kituoni LAZIMA mpiga kura apewe karatasi za wagombea wote ili awapigie kura.
  • Tume kuamriwa na Mahakama kutoa nyaraka au kuonyesha nyaraka lakini ikakataa kata kata.
  • Tume kutoa karatasi za kujumulishia zilizo na siri ndani yake LAKINI baadhi karatasi zilizotumika kujumulishia kura siyo za Tume na zimetengenezwa mahali pengine .
NAWASILISHA.
 
Moja kwa moja uchaguzi ulikuwa wa magumashi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wezetu wamefikia level nzuri sana ya kukuza demokrasia, Je ni nchi ngapi Africa ambazo unaweza kuhoji matokeo ya Tume ya uchaguzi kabla Rais mteule hajaapishwa??

Wakati wenzetu wanasonga mbele kidemokrasia, sisi ndiyo kwanza tulipofikia pahala pa kupiga marufuku hata mikutano ya vyama vya siasa - going backwards lakini eti tunajiona wajanja ndani ya EA, wakati kiuhalisia ni mambumbu wa demokrasia.
 
Chaguzi zote duniani ni danganya toto..!!
Hazijawahi kuwa na haki ndani yake..!!
Nipo tayari kukosolewa..
 

Hongera lakini Lazima wahoji uzalendo wako..
 
Sababu hizo zinatosha kubatilisha uchaguzi, tatizo kwa jaji gani anayeweza kufanya hayo maamuzi?
 
Chaguzi zote duniani ni danganya toto..!!
Hazijawahi kuwa na haki ndani yake..!!
Nipo tayari kukosolewa..
Utajikosoa mwenyewe nani apoteze muda wake watu wanaangalia mbele wewe ndio kwanza unapiga reverse.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…