Naomba kuwauliza Wanasheria waliobobea kwenye sheria. Je haya yafuatayo yanaweza kufanya uchaguzi kufutwa:-
- Mwenyekiti kutangaza matokeo kabla ya nyaraka zote hazijafika na yeye amekubal kuwa alifanya hivyo.
- Kama kuna tofauti ya kura za vituoni na za Wilayani.
- Kama sahihi zilizomo kwenye karatasi za kujumulishia kura za vituoni na Makao Makuu ya Wilaya siyo za wale walioteuliwa na Tume.
- Kama kura za Rais zinazidi kura za wagombea wengine kwa idadi ili hali sheria inasema unapoingia kituoni LAZIMA mpiga kura apewe karatasi za wagombea wote ili awapigie kura.
- Tume kuamriwa na Mahakama kutoa nyaraka au kuonyesha nyaraka lakini ikakataa kata kata.
- Tume kutoa karatasi za kujumulishia zilizo na siri ndani yake LAKINI baadhi karatasi zilizotumika kujumulishia kura siyo za Tume na zimetengenezwa mahali pengine .