Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na sasa kuna akina Dr. Mwaka wengi wamesambaa mikoani, yaani wao wanatibu kila kitu. Nimwestuka ndio wazo la kupata shuhuda toka kwa wadau likanijia.Niliwahi kutibiwa Kwa mjinga alikuwa anajiita Dr mwaka wakati sijamjua Hadi Huwa natamani nimtandike ngumi.mpuuzi sana huyo mtu na serikali nayo alikuwa inamwangalia tu anajitangaza kuwaaminisha watu.baada ya takataka zake kutokuniponesha nilitaka nionane Naye ana Kwa ana ili anieleze hizo takataka zake kama zinatibu kweli,lakini Kila ukienda unadanganywa na wasaidizi wake ameenda japani mara china ili tu uondoke.mwisho wa siku nikaachana Naye tu nikaenda mhimbili nikapona.Na nilipojihakikishia kuwa huyo mwaka ni tapeli ni pale Dr hamisi kingwangala alipoteuliwa na magufuli kuwa waziri wa afya akafanya ziara ya kushtukiza Kwa kichaa(mganga wa jadi mwaka)kwenye ofizi zake za kutapeli pale ilala bungoni.na kukimbia kupitia dirishani na Toka hapo akaacha na huo uganga wake wa jadi.Mjinga sana Huyu mtu.kala Hela za watu Kwa kutapeli na kuharibu afya za watu Kwa kuwanyesha mitakataka ambayo haifuate taratibu za kiafya.
Gharama zao ni za KUKAUSHA DAMU. Dozi zao ni kwa miezi 3-6 au hata mwaka 1.Kumbe ndio maana wanatumia nguvu kubwa kujinadi. Dah!
Hawa jamaa wanatumia Matatizo/Changamoto za kiafya kama Fursa kwao kujipatia Fedha/Kipato. Wanajua ni lazima watu huugua na huhangaika sana kupata matibabu. Wanachafanya ni kutumia vifungashio vizuri, kuandika majina ya dawa kwa mwandiko mzuri wa rangi za kompyuta na kuorodhesha magonjwa yanayotibika kwa dawa iliyomo ndani ya kifungashio(chupa ya plastik). Mtumiaji Ukifungua ndani utakuta ni unga /powder ya mimea iliyochanganywa e.g. mashonanguo + Mkunde pori+ Mbegu ya parachichi + maganda ya chungwa. Kwa kweli vitu hivyo ni dawa kweli lakini isingekuwa kwa bei ghali hivyo. Unalipia container, leaflet ya maelezo ya matumizi iliyobandikwa nje ya kopo na ndani tena utachangia mishahara ya Wahudumu, kodi ya pango n.k. Aidha maduka yao huwa ni mijini. Huku vijijini hutoyakuta kwani huku vijijini tunajichimbia mizizi wenyewe na kutafuna majani fresh sio hayo yaliyokaushwa fasta-fasta kuwahi soko.Tatizo la Dawa za Asili ni kutokuwa na Research. Watu wanauza Dawa kisa Waliambiwa Mti fulani huwa unatibu na Babu yake au Bibi huko Nyuma
Wakati wenzetu wakisema Dawa Fulani inatibu wanakuwa wamefanya. research kwa Watu hata 1000 ndio wanaileta sokoni
Sijamsikia tena Dr.Mwaka ila Star TV wanarusha (wananadi) tangazo la madawa Asili.Yule Mwaka Bado Yupo Yupo Kwenye Game
Hawana maabara za Utambuzi wa Tatizo - wao wanasikiliza maelezo kutoka kwa mgonjwa. Hawajui kwamba wagonjwa wengine kujieleza ni changamoto mojawapo. Ila wanajua fika kwamba dawa wanazouza haziwezi kumdhuru mtumiaji.Nenda na ugonjwa wowote hukosi dawa, na dawa moja inatibu magonjwa 50 kidogo, ukinunua usipo pona ukirudi una ambiwa uongeze dozi.
Sijamsikia tena Dr.Mwaka ila Star TV wanarusha (wananadi) tangazo la madawa Asili.
Chanel gani mkuu?Yupo Na Matangazo Hata Kwenye Television