- Thread starter
- #21
Ahsanteni sana wote, na wengine karibuni.Wizara ya afya imelala sana,Kuna madawa makali sana yanatolewa na haya ma-herbal clinic.
Ubaya wanasema wanatibu mpaka magonjwa makubwa kabisa,Tena wenye elimu hata ya Fundamental biology ya secondary nao wanadanganywa HIV,Sukari zinatibika .
Kuna dogo alihitimu sek. 2015, akapata ufaulu 0. Alikuwa na bidii kwa kazi za mikono na nidhamu kuu.
Kufikia 2017 mwishoni nikamkuta mkoa mwingine ananadi dawa za mitishamba kwenye noa.
Yeye ndio mtangazaji, na anatiririka balaa, yaani ukimsikiliza kwa sekunde chache unalipia dawa.
Amekusanya kijiji, na kinagombania dawa.
Walipohitimisha biashara kwa siku hiyo akanifuata, na kusimulia mafanikio yake:
Nyumba 3 zilizokamilika, usafiri wa kawaida wa kutembelea, viwanja kadhaa.
Waliofaulu na kundelea na shule ndio wapo Six au mwaka wa 2 kwa ngazi ya cheti. Dah!