Je, hii fursa ya Economy Driver plan 2.0 ni ya ukweli au matapeli?

Je, hii fursa ya Economy Driver plan 2.0 ni ya ukweli au matapeli?

Dullah694

Member
Joined
Jan 20, 2021
Posts
32
Reaction score
58
Habar nfugu zangu humu JF

Napenda niwaulize mwezi uliopita nilihudhuria seminar ya hii Project ya Economy Driver ambayo wana program ya Miliki maisha yako. Project nilikua ofisini Majengo Sokoni pale Dodoma alafu pia hii kampuni inadili na Afya na uchumi pia wana ofisi mikoa mbalimbali pale Dar wan ofisi pale mikocheni Mwai Kibaki road

Jamani mwenye uelewa mpana anisaidie siku ile tulielekezwa biashara pia tukapewa testimonies za waliofanikiwa ikiwemo na Billionaire Elias Muhoozi wa Uganda na vijana mbalimbali waliofanikiwa kupitia hii fursa

Naomben ushaur maana nataka kuanza biashara
 
Utapigwa. Mzee,
Miliki maisha yako kwa kutafuta kitu chako,
Wao hawaezi kukupa maisha ilhali wao hawana,
JARIBU KUCHUNGUZA WAFANYAKAZI WAO, NDUGU ZAO WAMO??
 
Utapewa shuhuda za uongo? Utaambiwa toa hela kisha watakupa madawa ukauze, yaani ukazungushe kama machinga. Halafu watakuambia lete watu wengine kisha utapata hela au kupanda cheo.
 
Jamani wana JF nina swali nataka kufahamu kuna yoyote anaeifahamu hii fursa ya biashara ya Economy Driver under Alliance in Motion Global wana ofisi pale Mikocheni nilihudhuria seminar yao nkaona wana mafanikio makubwa asa mm sielewi je nijiunge au vip maana nimepata shuhuda nyingi.

Kingine Je, hii Aim Global inatajirisha watu au ndo pyramid schemes?

Nisaidien wana JF
 
Ukishaona shughuli ya kifedha au biashara hautakuwa na control nayo au umiliki wa asset hata kidogo, achana nayo. anzisha yako hata kama mtaji ni kidogo
 
Si mda mrefu kuna mtu anaenda kuchezea nyundo ya utosi ...mtasikia Tu mamaaaaaa
 
Hao ni wakina Qunet, tu yaani kitu ni kile kile wana shuhuda za uongo tu za kumilik Magari makari wakati uhalisia hakuna.

Unakuta wanaongelea mafanikio ila wao wenyewe ni choka mbaya sana
 
Achana nao nao jamaa kama una hela katafute meza kariakoo pale weka biashara
 
Kuna mshikaji wangu tulisoma wote advance alikuwa qnet enzi hizo. Kuna siku aliniita cha ajabu akanipeleka qnet. Asee aliniuzi,
 
Nina wasiwasi kama hawa watu huwa hawatumii madawa. Kuna siku miaka mitano nyuma mtu kanitafuta vizuri. Akanialika nikajua naenda kuketishwa na wakuu. Eti "vaa vizuri..kutakua na watu wakubwa". Dah...asalalee kufika makumbusho kuingia kule...walinifurahisha mbona.

Haya nikasema em ngoja niangalie... Aisee nilijisikia vibaya sana mara ya kwanza. Mara nikapata usingiz wa ajabu na iv nilikua nimechoka basi hatari tupu.

Wakaanza semina wakajaribu kutuconvince sana. Ile siku nilikua nimetoka kuwekewa na mtu anayeniamini laki saba kwa ajili ya biashara yake.... Wale sasa wanakwambia "shuka chini.. kuna benki na wakala hapo..nenda katoe hiyo hela..usijiulize mara mbili" mwingine anakwambia " fursa ndo hii..pesa fasta..nani atatoa leo hii tumpashie"... Yani wale wanakujaza upepo ilibak kidogo niende kutoa ile hela.

Lakini baadae nikawaambia nitajiunga jumanne (ilikua jmosi). Nilivyosepa pale kwanza ndo akili yangu ikaanza kuwa rational. Nikatafakari nikaona huu us****. Nikamblock alienialika nikaendelea na my life. Nikaelewaga ndo maana wale mabosi kwenye mabendi wakitajwa kama wanajazwa upepo wanamwaga manoti, au wale wacheza vigoma wakinengua wakasifiwa huwa wanachizika hadi kutoa nguo waonyeshe shanga ili watu wapagawe zaidi..au hata bar watu wakishalewa...wanahonga hata bar nzima "mpe kila mmoja moja au mbili"...
 
Nina wasiwasi kama hawa watu huwa hawatumii madawa. Kuna siku miaka mitano nyuma mtu kanitafuta vizuri. Akanialika nikajua naenda kuketishwa na wakuu. Eti "vaa vizuri..kutakua na watu wakubwa". Dah...asalalee kufika makumbusho kuingia kule...walinifurahisha mbona.

Haya nikasema em ngoja niangalie... Aisee nilijisikia vibaya sana mara ya kwanza. Mara nikapata usingiz wa ajabu na iv nilikua nimechoka basi hatari tupu.

Wakaanza semina wakajaribu kutuconvince sana. Ile siku nilikua nimetoka kuwekewa na mtu anayeniamini laki saba kwa ajili ya biashara yake.... Wale sasa wanakwambia "shuka chini.. kuna benki na wakala hapo..nenda katoe hiyo hela..usijiulize mara mbili" mwingine anakwambia " fursa ndo hii..pesa fasta..nani atatoa leo hii tumpashie"... Yani wale wanakujaza upepo ilibak kidogo niende kutoa ile hela.

Lakini baadae nikawaambia nitajiunga jumanne (ilikua jmosi). Nilivyosepa pale kwanza ndo akili yangu ikaanza kuwa rational. Nikatafakari nikaona huu us****. Nikamblock alienialika nikaendelea na my life. Nikaelewaga ndo maana wale mabosi kwenye mabendi wakitajwa kama wanajazwa upepo wanamwaga manoti, au wale wacheza vigoma wakinengua wakasifiwa huwa wanachizika hadi kutoa nguo waonyeshe shanga ili watu kwapagawe zaidi..au hata bar watu wakishalewa...wanahonga hata bar nzima "mpe kila mmoja moja au mbili"...
 
Back
Top Bottom